Visiwa vya Chagos: Koloni la mwisho barani Afrika

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
Chagos ni visiwa visivyojulikana sana ambavyo vipo katikati ya Bahari ya Hindi. Kwa miaka 150, vilikuwa sehemu ya nchi ya Mauritius iliyotawaliwa na Uingereza. Hata hivyo, miaka kadhaa kabla ya Mauritius kujipatia uhuru mwaka 1968, serikali ya Uingereza iliamua kuvitenganisha visiwa vya Chagos na Mauritius, na kuanzisha koloni jipya wakati dunia nzima ikifikiria kuwa enzi ya ukoloni imemalizika, na kuviita kuwa Ardhi ya Uingereza katika Bahari ya Hindi BIOT.

Waingereza walisitisha kutoa huduma za maji na chakula ili kuwafukuza wakazi wa visiwa hivyo, na kukodisha kisiwa cha Diego Garcia kilicho kusini kabisa ya visiwa vya Chagos kwa Marekani ili kiwe kambi yake ya kijeshi. Historia hiyo ya kuaibisha imefanya visiwa vya Chagos kuwa koloni la mwisho barani Afrika, pia imefichua unafiki wa nchi hizo mbili wa kudai kuheshimu na kulinda sheria ya kimataifa.

Mauritius siku zote inadai kurudishiwa visiwa vya Chagos, na juhudi zake zimeungwa mkono na Umoja wa Mataifa, Mahakama ya Kimataifa na mashirika na nchi mbalimbali za ndani na nje ya bara la Afrika ukiwemo Umoja wa Afrika. Mwezi Februari mwaka 2019, Mahakama ya Kimataifa iliyopo the Hague iliamua kuwa kitendo cha kuvitenganisha visiwa vya Chagos na Mauritius ni haramu, na kimekiuka haki ya kujiamulia ya Mauritius na ukamilifu wa ardhi zake.

Uamuzi huo ulitangazwa kutokana na dai la mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa, japo hauna nguvu ya kisheria kwa nchi wanachama wa Umoja huo, lakini umetoa taarifa muhimu ya kisheria. Miezi mitatu baada ya Mahakama hiyo kutoa shauri hilo, mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa ulipitisha azimio kwa kura 116 za ndio dhidi ya kura 6 za hapana, likiidhinisha kuwa visiwa vya Chagos ni sehemu isiyojitenga ya Mauritius na kutaka Uingereza ijitoe kwenye visiwa hivyo kabla ya mwezi Novemba mwaka huo. Lakini Uingereza na Marekani zilifumbia macho uamuzi huo na sheria ya kimataifa.

微信图片_20210409092051.jpg


Katika ripoti ya sera ya mambo ya kigeni iliyotangazwa na serikali ya Uingereza mwezi uliopita, serikali ya Uingereza ilitoa ishara ya kuhama kutoka Ulaya hadi sehemu ya Bahari za Hindi na Pasifiki, na pia kusema “hakuna uhusiano wowote unaothaminiwa sana kama kuanzisha ushirika wa kijeshi na Marekani”. Ripoti hiyo pia imesisitiza kuwa daima Uingereza inalinda “Mkataba wa Sheria ya Bahari wa Umoja wa Mataifa” katika pande mbalimbali. Naye rais Joe Biden baada ya kuchaguliwa, alisema “utawala wa sheria” ni moja ya thamani za kidemokrasia zinazolindwa zaidi na Marekani, pia ni kiini cha sera yake ya mambo ya kigeni. Hata hivyo, kabla ya kufanya utawala wa sheria kama silaha, nchi yoyote inatakiwa kufanya shughuli zake vizuri kwanza, ikiwemo kuhakikisha mshirika wake mkubwa analinda utawala wa sheria. Ni wazi kuwa kwa Uingereza na Marekani, suala la kulinda ama kutolinda utawala wa sheria, linaamuliwa kama linaendana na maslahi yao ya kisiasa.

Kwa muda mrefu, Uingereza na Marekani zinatumia sheria ya kimataifa kama chombo cha kupambana na China. Miaka mitano iliyopita, mahakama ya kimataifa iliunga mkono rufaa iliyotolewa na Ufilipino dhidi ya China bila ya msingi wa kisheria katika suala la Bahari ya Kusini, kisha wizara ya mambo ya Marekani mara moja ilikaribisha uamuzi huo, huku upande wa Uingereza ukiitaka China ifuate uamuzi huo. Hadi leo, nchi hizo mbili zinaendelea kukuza suala la Bahari ya Kusini ya China katika bahari ya Pasifiki na kuharibu utulivu wa kanda hiyo, huku zikifanya njama katika Bahari ya Hindi na kukalia kiharamu ardhi ya Mauritius. Je, hizi ni juhudi zinazoitwa na nchi hizo za kulinda amani ya kanda ya Bahari za Hindi na Pasifiki?

Uingereza na Marekani zinatakiwa kulinda kwa vitendo “utawala wa sheria”. Ramani rasmi ya Umoja wa Mataifa imeonesha kuwa visiwa vya Chagos kikiwemo Diego Garcia vinamilikiwa na Mauritius, wala sio Uingereza. Ndio maana, Uingereza inatakiwa kushusha bendera yake katika koloni la mwisho barani Afrika, Marekani nayo pia inatakiwa kuondoa wanajeshi wake. Hadi hapo, shutuma kuhusu unafiki na ugeugeu dhidi ya nchi hizo mbili zitapotea.

微信图片_20210409092229.jpg
 
Back
Top Bottom