Beauty Eva
Senior Member
- Jul 22, 2016
- 131
- 374
Kidooogo, kijijini kwetu ninaonekana nimesoma. Hivyo nikifika wazazi wengi huniona kama role model kwa wana wao hususani wa jinsia ya kike.
Wiki iliyopita, nilikuwa kijijini. Mwalimu wangu aliyenifundisha O-level hapo hapo akaja nyumbani kunisalimia.
Tuliongea mada nyingi sana, mojawapo ni kuhusu mmomonyoko wa maadili hasa kwa vijana. Uzuri wenyewe, hata mwalimu wangu huyu ni kijana tu wa makamo.
Katikati ya maongezi, wakapita mwanafunzi wake wakiwa wanatoka shule. Akaanza, Eve (Eva) hivi visichana vya siku hizi, vimeharibika kweli kweli. Visichana vidogo lakini vinafanya mambo ya Wakubwa. Mimi kama mwalimu wa nidhamu nimepambana lakini wapi!!!
Baada ya maneno hayo ya mwalimu, nilimuuliza "Je, hivyo visichana vimeharibika au vimeharibiwa?" Nani anaviharibu? Je, anaetakiwa kulaumiwa kwanza ni anayeharibu (Subject) au anayeharibiwa (Object)? "
Kwa nini lawama ziende upande mmoja?
Je, wanaume wasipoharibu, wanawake wataharibika wenyewe?
Eti MMU!!!?