Visasi vya JK kwa watu wa Arusha? Ahamishia mkutano wa wakuu wa EAC Dar



Duuh!! Hiyo noma, bora kutembea kama ungekuwa unaishia Millenium tower!!!!!!!
 
.....Enzi JK akiipenda Arusha alikuwa akija almost kila weekend kwa safari binafs..ikiwemo kupumzika ngurdoto na dogo dogo zake .....lakini he has made a big U turn ...just kwa sababu za kisiasa...

hata alipoenda kutoa kamisheni za jeshi alitua na ndege monduli na kupaa moja kwa moja...hakuingia arusha ambapo si kawaida yake....

bado nawalaumu watu wa usalama....how does such personality enter the holy place------state house?
 

Ndugu Philemon
Huyu Banduka alijaribu kutuma Wazee wa CCM kwenda DSM kwa JK (Mwenyekiti CCM Mkoa Lindi na wengine) kuomba msamaha kwa kosa ambalo alikuwa hajui lakini Kikwete alicheka na kusema hana tatizo naye!!!!! Huyu ndiye Rais (smiling president) anayesifiwa.
Anayekataa kuombwa msamaha ni SHETANI. Tuombeni jamani tumevamiwa.
 
 
Comment kama hii inatoka kwa msomi na ambaye ni mshauri wa Raisi. Tuna safari ndefu sana.....

Jamani kama huyu ni mshauri wa rais yumo humu janvini kwanini hawamwambii bosi wao kuwa JF ni ya kila mwenye nia njema na Tanzania na wao pia wamo humu na sio ya chadema kama consultants wao wanavyowambia. Acheni unafiki hiyo njaa yenu itawafikisha pabaya. Semeni kweli tupu kwani msema kweli ni mpenzi wa Mungu.
 

Tumechoka na mambo ya uvumi na ya kufikirika yasiyo hata na msingi. Kwanza kama kupingana na JK ndiyo uadui basi Mwandosya, Mwakyembe, Mary Nagu, Magufuli, Kagasheki na wengine wengi wasingekuwa mawaziri au Njoolay asingekuwa RC, maana hao wote walipinga ugombea wake. Haya ni mambo yasiyo na msingi na hata hili la kuhamisha mkutano kutoka arusha kuja dar es salaam ni porojo zisizostahili hata kutupotezea muda. Kama ingekuwa hivyo basi hata vikao vya Council of Ministers ambavyo vimekuwa vikifanyika mpaka mwisho wa wiki iliyopita vingekuwa vimehamishwa. Suala la mkutano ufanyikie wapi ni suala la convenience na ingewezekana kufanyikia hata Tabora. Hivi Arusha kuna nini cha ajabu alichofanyiwa JK ,mpaka awalipizie visasi maana kama ni wabunge wa upinzani basi Mkoa wa Mwanza una wapinzani wengi kuliko Arusha. Hoja nyingine ni potofu mpaka inakera.
 

Logically huu ndiyo ukweli kwamba anajua swala la umeya bado ni tata na kama president atajisikia embarased kama lolote litatokea kutoka kwa raia wake against yeye ukizingatia media za kimataifa zitakuwepo, so politically it could be difficult kwake kuja kufanya mkutano hapo AR hasa wakati huu ambapo CHADEMA wana utilize fully any political opportunity. Chakujiuliza atakimbia huo ukweli hadi lini?
 

Mmh I doubt kama kweli unapenda kuelewa ukweli ama kwa personal reasons unataka kuleta ushabiki usioweza kuutetea kwa nguvu za hoja. Kumbuka ni rahisi kum contain adui akiwa karibu yako kuliko akiwa mafichoni. Unadhani angewaacha hawa watu angeweza kutawala kwa urahisi huku hawa wakiwa na wafuasi wao sehemu sehemu na bado wako katika system? Ukimwondoa Mwandosya na Mwakyembe Mbeya angeweza kuitawala? Je bila Magufuli na Kagasheki kanda ya ziwa ingekuwaje, angalia tu sasa mambo yalivyo mazito je hao pia wangekuwa ndiyo opposers ndani ya chama ingekuwaje? Impact ya Nagu plus Sumaye ukamweka na Slaa wawe against the government kwenye siasa za mkoa wa Arusha na Manyara unazifahamu na huku Kilimanjaro yote under influence ya Mbowe, Mtei na Ndesamburo mguu wake ungekanyaga huko kaskazini kweli? Kama alivyo sema PM aliangalia wale maadui wasio na impact kubwa lakini pia ambao watapunguza tention sehemu hizo kwa manufaa yake binafsi which is politically accepted any way. Siasa ni mchezo waajabu na wenye ku involve very dirty games kama wanaofanya siasa siyo watu ambao wanaongozwa na morals.
 

Nungunungu ..umerudi ...??,mswahili na mwenzake wako wapi......ile SI UNIT ya kuchemcha..du i remember those old days here at JF..............WELL THESE IS CRAP .....unahalalisha visasi kwa kina mashishanga....?.........ni kawaida ya watu wajinga wakiiishiwa hoja huja na sababu za kuwa wanaonewa kwa ajili ya dini..hakuna kitu kama hicho ..fanya kazi!!
 
maneno hayooo kama nikweli basi ni hatari. Ila kwani ni J.K. anayepanga eneo au ni watendaji wake?
 
Sasa kumekucha,asante mkuu sina comment.
 
Iligeuzwa na nani?na lini na kupambana na nani na mapambano yanaendeleaje?Kwa upeo wako unataka kutushawishi kuwa wageni waliohudhuria mkutano wangeweza kushambuliwa na wanasiasa walioko kwenye mapambano ya kisiasa?ebu tazama kinachotokea ng'ambo ya mto ili kupanua fikira,uondokane na fikira butu kama rangi nyeusi usiite nyeupe,maamuzi yaliyofanywa na jk ni mabaya.LKN NIVIBAYA ZAIDI KW KIJANA KM WW KUYAUNGA MKONO HUKU UKIJUA WAZI KUWA NI YA HOVYO.
 
nashangaa wanaokuja na hoja za protest..watu wanaandamana kwenye mikutano ya G8 Itakuwa huku..tena maandamano ya amani yanaonesha level ya civilialization ipo juu.
 
Mwanakijiji na wewe unaingia kwenye mtego huu??? Kwamba ni kisasi?? This is too low. Inamaana Arusha ndio sehem pekee nchi hii panapostahili mikutano yote? Na mikutano haijawahi kufanyikia DSM? Hizi ni hoja za kitoto

Kwa JK anything is possible!!!
 

du hili nalo ni limsumari nini limepigiliwa hapa kwenye hread ya PM
 
Kweli KIKWETE ni mtu sumu sana kama alimfanyia Mkuu wake wa mkoa hivyo ,ana visasi vibaya sana,hivi huyu Banduka yupo hai au alikufa hajawahi kusikika tena wakati alikuwa mtu maarufu

Kikwete ni mtu hatari saana akijua unampinga. Nakumbuka alivyokua anapigania uraisi na waziri wa maji (Mwa...) alikwenda Kilimanjaro wakati huo Hilda Ngoye alikua mkuu wa mkoa. Hilda alikua ana msapoti waziri wa maji hivyo hakumpa mapokezi makubwa sana kama alivyompa Mwa.. Kikwete alivyoshinda akamuondoa Hilda Ngoye akamuhamishia Mbeya kwa Mwa... Watu wa Kilimanjaro waliumia saana na toka siku hiyo Kikwete na CCM kilimanjaro haziivi sana. Kikwete amechangia sana kugawanyika kwa wana CCM kwaajili ya fitina na visasi.
 
Logic pekee ni kusema mkutano huo umefanyikia Dar kwa sababu ya Investment Forum na viongozi hao walitakiwa kuhudhuria. Vinginevyo suala la usalama halipo. Ingekuwa hivyo basi viongozi wa EaC na IcTR waliopo wangeondolewa!
 
Wale Makamishna walistaafishwa kwa manufaa ya Mkapa ili mteule wake mpya wakati huo, Omar Mahita, aingie kazini. Imran Kombe alistaafishwa, akafananishwa na jambazi, akapigwa risasi, akafa.

Kwa maana hiyo jk anafanya sahihi kwa sababu mtangulizi wake alifanya hivyo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…