Visanga vya BIBI WA MSIMBATI

Visanga vya BIBI WA MSIMBATI

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
78,823
Reaction score
168,048

Kikongwe Somoe Issa anayekadriwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka 90 ambaye ni Mkuu wa Kaya ya Msimbati kijiji ambacho gesi asilia inavunwa, mkoani Mtwara aliionya Serikali kutoendelea na mpango wake wa kusafirisha gesi kwenda Dar es Salaam na kwamba iwapo itapinga bomba hilo litasafirisha maji badala ya gesi. Juzi usiku alifuatwa kijijini na Gari na wananchi wakaamua kuliteketeza kwa Moto hilo gari


CURRENT NEWS:-
Huko Mtwara kamanda wa polisi mkoa amepooza, wananchi wanadai ni mkono wa bibi
​




Bibi aliyetishia kugeuza gesi kuwa maji afichwa

BIBI MSIMBATI ANUSURIKA ‘KUTEKWA' | KARIBU KUSINI
 
kuna wakati alilainika hadi akaruhusu itoke,
ona wakifanyiwa mazingaumbwe ili wakatoke gesi
voda.jpg
 
Kisa nini?

Gesi isitoke mkuu!!



[h=2] Bibi aliyetishia kugeuza gesi kuwa maji afichwa [/h] Jumapili, Juni 16, 2013 05:55 Na Gabriel Mushi, Mtwara

KIKONGWE Somoe Issa, anayekadiriwa kuwa na umri zaidi ya miaka 90, ambaye aliwahi kutishia kuigeuza gesi kuwa maji iwapo serikali itaendelea kulazimisha kusafirisha kwenda Dar es Salaam, sasa hajulikani alipo.

Taarifa zilizoifikia MTANZANIA Jumapili ambayo ipo mkoani Mtwara, zilidai kuwa bibi huyo baada ya kutoa tishio hilo sasa amefichwa, ili asiweze kutekeleza lengo lake hilo.

Bibi Somoe, anayeaminika kama Mkuu wa Kaya ya Msimbati, kijiji ambacho gesi asilia iligundulika, sasa hajulikani alipo, huku ndani ya kijiji hicho ulinzi mkali ukiwa umeendelea kutawala.

Ulinzi umeimarishwa katika kijiji hicho, lengo likiwa ni kuhakikisha hakuna mtu anayefika karibu na nyumba aliyokuwa akiishi bibi huyo.

MTANZANIA Jumapili, lilifika katika kijiji hicho juzi, ambako liliweza kuzungumza na Mwenyekiti wa Kijiji cha Msimbati, Salum Athuman Tostao, ambaye alikiri kuwa bibi huyo hayupo na wala haifahamiki alikopelekwa.

"Ni kweli bibi huyu hajaonekana tangu palipotokea vurugu na watu wa usalama waliokuwa wakitaka kumuiba, kama unavyofahamu kulikuwa na mtu aliyejifanya mwandishi wa habari alitaka kumuiba bibi huyu, lakini wanakijiji wakamshtukia na kuchoma gari lake moto.

"Kutokana na hali hiyo, mpaka sasa hatufahamu alipo na hatujui kama ni serikali au wanafamilia wamemficha, kwa sababu kwanza hawaturuhusu hata sisi ambao ni viongozi kufika maeneo ya nyumba aliyokuwa akiishi kwa sababu wanadhani tutaleta watu wengine wasiokuwa waaminifu kwa familia hiyo," alisema Tostao.

Gazeti hili lilipomtafuta mtoto wa bibi huyo, Manzi Faki, alikataa kuzungumza chochote kuhusu mama yake, lakini aliitaka serikali kutekeleza ahadi zake kwa Wanamtwara.

"Hilo suala la mama sitaki kulizungumzia kabisa… jambo la muhimu serikali inapaswa kufahamu kuwa sisi wana Mtwara tunataka itekeleze ahadi ilizotuahidi ndipo waje kuchukua hicho kidogo wanachokitaka, zaidi ya hapo kijumla gesi haitoki," alisema Faki.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Mtandi, Salum Waziri, alieleza kuwa bibi huyo anaaminiwa na wanakijiji wenzake kutokana na uwezo wake wa kuzuia mambo yasiyotakiwa ndani ya jamii, sambamba na kuleta riziki pale wanapokwenda kumuomba.

"Kwa kweli sasa ulinzi mkali umeimarishwa na wanakijiji, hakuna mtu anayefika nyumbani kwake, hata sisi wenyewe hatuthubutu, ndiyo maana hatufahamu alikopelekwa.

"Nakumbuka bibi aliwahi kutumiwa na kampuni ya Artumas kukwamua mashine iliyokuwa imenasa katika mchakato wa uchimbaji wa gesi hiyo baharini, ambapo wazungu hao walihangaika kuita wahandishi nje ya nchi, lakini wote wakashindwa, ndipo waliponong'onezwa kuhusu bibi huyo wakamwendea na akaja kunasua.

"Wakampa zawadi ya kumjengea nyumba, haya ni mambo ambayo yalitokea mwaka 1994, kiujumla yapo mengi ambayo yametufanya tumwamini sana," alisema Waziri.

Januari mwaka huu, Afisa usalama mmoja anayedaiwa kufahamika kwa jina la babu alijikuta katika wakati mgumu kiasi cha gari lake kuchomwa moto huku yeye mwenyewe akikimbilia kusikojulikana baada ya kuzuka vurugu kubwa wakati akimshawishi bibi huyo asizuie gesi kwenda Dar es salaam.

Inadaiwa kuwa mwanausalama huyo alitumwa na viongozi wa juu wa serikali baada ya bibi huyo kutamka wazi kuwa gesi haitoki Mtwara kauli ambayo iliwafanya viongozi kupata wasiwasi na hivyo kumtuma mtu huyo ili amshawishi bibi huyo.

Wakati bibi huyo akizungumza na mwanausalama huyo inadaiwa kuwa aliwaita wajukuu zake wamsikilize ndipo vurugu kubwa zilipoibuka na kusababisha mwanausalama huyo atimue mbio huku akilitelekeza gari lake.

Juzi na jana baadhi ya wakazi wa kijiji hicho wakizungumza na gazeti hili walisema wao hawazuii gesi kutumiwa na Watanzania, ila wanataka gesi hiyo ichakatwe hapohapo mkoani Mtwara na ndipo isafirishwe kuelekea sehemu nyingine.

Vurugu kuhusu gesi hii ya Mtwara zilianza kuibuka Novemba mwaka jana, wananchi wa mkoa huo walikuwa wakipinga ujenzi wa bomba la gesi kwenda Dar es Salaam.

Pamoja na vurugu hizo kuzimwa mara kadhaa na Jeshi la Polisi, ambao sasa wanashirikiana na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), lakini bado MTANZANIA Jumapili imeshuhudia hali ya amani haijaweza kurejea mkoani humo.

Baadhi ya watu mkoani hapa, bado wanaendeleza visasi kwa kuchoma nyumba za wenzao, huku JWTZ wakidaiwa kuwapiga raia kila mara hata inapotokea kuwa wamezomewa.

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
===================================================================================================


[h=1]KARIBU KUSINI[/h] KITOVU CHA FIKRA PEVU, UWELEDI NA UPASHANAJI HABARI.



[h=2]BIBI MSIMBATI ANUSURIKA ‘KUTEKWA'[/h] January 24, 2013
wakazi wa Msimbati wakiangalia mabaki ya gari

Mhariri KUSINI nashuhudia

Asha Hamisi ni mtoto wa pili wa Bibi Mtiti

Fatuma Tom, shangazi wa Babu

MKUU wa Kaya ya Msimbati ambako gesi asilia inachimbwa mkoani Mtwara, Bibi Somoe Mtiti (106) amenusurika ‘kutekwa' na mtu anayedaiwa kuwa ni ofisa usalama wa Taifa baada ya wananchi kuvamia gari lake na kuliteketeza kwa moto jana usiku.
Hivi karibuni Bibi Mtiti aliionya serikali juu ya mpango wake wa kusafirisha gesi ghafi kwenda Dar es Salaam kwa madai iwapo serikali itapuuza onyo hilo bomba hilo litasafirisha maji badala ya gesi kusudiwa.
Kwa mujibu wa wanakijiji hao, Mtu huyo ambaye ana asili ya kijiji hicho waliyemtambua kwa jina la Seleman Babu aliwasili kijijini hapo jana saa 10 jioni akiwa na gari ndodo aina ya Mark II na kwenda nyumbani kwa shangazi yake.
Habari zinadai kuwa saa 2 usiku Babu, alikwenda nyumbani kwa Bibi Mtiti akiwa na gari pamoja na shangazi yake aliyetajwa kwa jina la Fatuma Saidi Tom.
"Unajua yule bibi tunamlinda, sasa ilipoonekana ile gari usiku pale, watu wakaanza kujiuliza linafanya nini…wakaanza kusogea , kadiri mda ulivyokuwa unakwenda ndivyo watu walivyozidi kuongezeka" alisema Juma Ayoub mkazi wa kijiji hicho.
Asha Hamisi ni mtoto wa pili wa Bibi Mtiti, akihadidhia juu ya tukio hilo alisema yapata saa 2 usiku wakiwa wanakula chakula alipokea wageni wawili ambao baada ya kumaliza kula waliomba kuongea na mkuu huyo wa kaya.
"Alikuja kijana na mama wakaniomba kuongea na bibi…alimuliza bibi kama ana uwezo wa kwenda Mtwara, bibi akajibu hawezi…wakaniuliza mimi kama naweza kwenda badala yake nikawaambia siwezi…akasema ametumwa na Rais Jakaya Kikwete na Hawa Ghasia..wamjie bibi wakazungumze nae mambo ya gesi" alisema Hamis
Aliongeza kuwa "Alisema kama bibi yupo tayari Jumanne ijayo watamfuata kwa gari…mimi nikasema sitaki…nilipochungulia nje nikaona watu wengi wamezunguka"
"Kwa kuwa tunamfahamu tulimwambia aondoke mpango aliojia haufai, akawa anabisha, tukaendelea kumsihi..wakati huo watu wanazidi kuongezeka…alipotoka akakosea njia, alipotita hakukuwa na njia…watu walimfuata wakaanza kumrushia mawe…aliacha gari akakimbia…ndipo wananchi walipoliteketeza gari kwa moto" alisema Manzi Mohaedi Faki mtoto wa tano wa Bibi Mtiti
Fatuma Tom ambaye ni shangazi wa Babu amethibitisha kumpokea mwanae huyo na kumsindikiza kwa Bibi Mtiti na ambako alimuomba mkuu huyo wa kaya akubali kuondoka nae kwenda Dar es Salaam kwa maelezo kuwa ametumwa na viongozi wake wa juu.
"Ni mwanangu mtoto wa kaka yangu, alikuja akaniomba nimepeleke kwa bibi akamsalimie tuliondoka saa 2 usiku…watu walituzingira na hali ilipokuwa mbaya niliondoka na kumwacha mwanangu pale, nae alikimbia na ndipo walipochoma moto gari" alisema Tom
Alifafanua kuwa "Huyu mwanangu anaishi Dar es Salaam, anafanya kazi usalama wa Taifa…nadhani alirudi jana hiyohiyo Mtwara"
Mwnyekiti wa kijiji cha Msimbati, Salum Tostao alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa ofisi yake haikupokea mgeni yeyote kutoka serikalini kwa siku hiyo.
"Ni kweli gari imechomwa lenye namba za usajili T 609 BXG mali ya Mussa Babu…taarifa hii ni kwa mujibu wa nyaraka tulizookota kutoka ndani ya gari hilo" alisema Tostao
Selemani Babu alikanusha madai ya yeye kwenda kijijini hapo jana na alisema "Hapana, hapana labda umekosea…na..na..na..umekosea…sijakwenda maimbati jana…kwanini asiwe Mussa, umekosea sio mimi kwa heri"
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mtwara, Maria Nzuki alisema hana taarifa zozote kuhusiana na tukio hilo kwa kuwa mhusika hajakwenda polisi kulalamika.
Mwisho.
Katavi umeelewa sasa eeh?
 
Last edited by a moderator:
Arushaone..............mie bado sijaelewa kabisa
kwanini ban sasa?
 
Last edited by a moderator:

Kikongwe Somoe Issa anayekadriwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka 90 ambaye ni Mkuu wa Kaya ya Msimbati kijiji ambacho gesi asilia inavunwa, mkoani Mtwara aliionya Serikali kutoendelea na mpango wake wa kusafirisha gesi kwenda Dar es Salaam na kwamba iwapo itapinga bomba hilo litasafirisha maji badala ya gesi. Juzi usiku alifuatwa kijijini na Gari na wananchi wakaamua kuliteketeza kwa Moto hilo gari


CURRENT NEWS:-
Huko Mtwara kamanda wa polisi mkoa amepooza, wananchi wanadai ni mkono wa bibi
​




Bibi aliyetishia kugeuza gesi kuwa maji afichwa

BIBI MSIMBATI ANUSURIKA ‘KUTEKWA’ | KARIBU KUSINI

Nashukuru and iam proud kuwa Mzawa wa Mtwara.
 
Nchi yetu inaongozwa na mazingaombwe.
Nasikia umeme nao kutoka Ubungo kwenda Makumbusho unaishia kwenye kanisa la Kakobe, kutoka hapo hamna kitu ndio maana hadi leo wameshindwa kufungua sub station ya Makumbusho
 
Back
Top Bottom