Visa vya matapeli na watoto wa mjini

Visa vya matapeli na watoto wa mjini

[emoji23][emoji23][emoji23]niliwahi kufanya biashara ya maiti... Nikapeleka maiti feki usiku wa manane eneo la tukio nikalipwa changu nikasepa kufika home nimelipwa pesa feki[emoji24][emoji24][emoji23][emoji23]

Jr[emoji769]
🤣🤣🤣
 
Ukisikia mjini shule, shamba darasa. Jiulize hao waliotunga huo usemi walikuwa na maana gani ama walikutana na masahabu gani!

Akili ya binadamu ni kitu cha kushangaza mno. Kina uwezo wa ajabu hasa pale mtu anapokutana na changamoto mbalimbali. Huko vijijini akili nyingi zimelala kutokana na kukosa changamoto za kimaisha.

Kijijini hata kama huna kazi huna pesa utaishi tu... Sio mjini! Mjini tangu kunapambazuka mpaka kunakuchwa kila kitu ni shekeli. Hakuna cha bure mjini. Lakini vilevile mjini kila mtu anatamani kuishi maisha fulani lakini changamoto ya elimu kipato na ajira ndio kikwazo.

Hivyo basi kuweza kukabiliana na changamoto hizo watu kila uchao hubuni mbinu mpya za kuingiza kipato. Kuanzia utapeli, wizi, ujambazi, kukaba, kurubuni nknk. Kila mmoja wetu hawezi kukosa kisa cha hawa jamaa wanaoishi kwa ujanja ujanja. Nitaaza mimi kwa kusimulia vichache

Kisa cha kwanza
Huyu jamaa yeye hakuwa na kazi maalum. Ila muda wote ni msafi akionekana kama afisa fulani hivi. Siku moja akawa kakosa nauli kabisa ya kurudi nyumbani kwake Tabata na yuko kijitonyama.

Alichofanya ni kuwarubuni wale jamaa wa magari ya majitaka kuwa anataka huduma hiyo Tabata... Wakapatana bei akaenda nao mpaka mtaa wa pili kufika kwake.

Akashuka huku akiwaelekeza uchochoro mmoja kuwa ndio kwake... Akaingia hapo akatokea upande wa pili akasepa mazima.... [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Kisa cha pili.
Ni wale jamaa wanaorubuni watoto kuwanunulia chakula ama chochote. Ataenda na mtoto hapo mahali ataagiza kama ni bidhaa ama chakula.... Kisha atasepa na kumuacha bond mtoto wa watu..

Karibu nawe kabla sijaendelea na visa vingine

Jr[emoji769]
Hili la gari la maji taka limenifanya nicheke kwa sauti.
 
 
Jamaa mmoja aitwaye Jones Bogonko Onchonga kutoka Kisii amekamatwa huko kaunti ya Turkana akijifanya ni Padre wa Kanisa Katoliki wa shirika la Missionaries of Charity (M.C.) akijitambulisha kama Rev.Fr.Jones Onchonga, M.C.

Padre ā€œfekiā€ Onchonga baada ya kuhojiwa na jeshi la Polisi amekiri kujifanya Padre karibia miaka miwili na kutoa huduma za kanisa zikiwemo sakramenti. Alifika Lodwar mwaka 2025 akiwa na nyaraka zinazomtambulisha kuwa ni Padre wa shirika la Missionaries of Charity (M.C.) ambaye ametumwa kufanya utume jimboni hapo. Kumbe nyaraka hizo zilikua za kughushi.

Alipokelewa ofisi ya jimbo na kupangiwa utume katika parokia ya Mtakatifu Maria Lodaraja iliyopo Lodwar na baadaye kituo cha huduma za maombezi cha Mtakatifu Thomas (St.Thomas chapel) kilichopo eneo la Kalokol huko Turkana.

Kwa ujasiri wa ajabu Padre huyo feki alimtembelea Askofu wa jimbo hilo Mwadhama John Mbinda (C.S.Sp.) mara kadhaa ofisini kwake na kula naye chakula cha mchana. Katika jambo la kuogofya zaidi Padre huyo feki amewahi kusalisha ibada moja pamoja na Askofu Mbinda katika Parokia Kuu (Cathedral) ya Mtakatifu Augustine iliyopo Lodwar.

Askofu Mbinda ametangaza kuwa sakramenti zote zilizotolewa na padre huyo feki ni batili na watoto wote waliobatizwa na Padre huyo watarudia kubatizwa upya kwa sababu alitoa sakramenti ya ubatizo bila kuwa na mamlaka ya kanisa (Potestas ordinis).

Taarifa ya polisi inaonesha kuwa Onchonga hakuwahi kusomea seminari ya Katoliki na hajawahi kupata mafunzo yoyote ya falsafa wala theolojia. Alijifundisha mwenyewe liturujia na utaratibu wa kuendesha ibada za kanisa kupitia vitabu mbalimbali pamoja na njia ya mtandao.

Alikutwa na vitabu 17 vya mafundisho ya kanisa ambavyo alikuwa akivitumia kujifunza mambo mbalimbali yakiwemo historia ya kanisa na utaratibu wa kuongoza ibada na kutoa sakramenti. Imebainika kuwa Onchonga ana mke na watoto wawili huko Kisii na amekuwa akiwatembelea mara kwa mara.

Kwa sasa anakabiliwa na kosa la kujifanya mtu mwingine (personation) kinyume na sheria ya kanuni ya adhabu (Penal Code, Section 382) na akikutwa na hatia anaweza kuhukumiwa hadi miaka mitatu gerezani.!
 
Back
Top Bottom