Visa vya mapenzi na simu: Kisa hiki kinanikumbusha mbali

Visa vya mapenzi na simu: Kisa hiki kinanikumbusha mbali

Mr. Django

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2014
Posts
1,830
Reaction score
2,434
Tumekua tukisikia visa vingi sana vinavyotokana na mapenzi, yani pale Mwanamke au Mwanaume anakuta msg za ajabu baada ya kuchukua simu ya mpenzi wake, ila hii ya Brazil ilivunja rekodi.

Ilitokea kwa binti mmoja kumeza simu muda mfupi tu baada ya boyfriend (Renato) wake kutaka kusoma msg ambapo msichana alikimbia na simu kutoka kwenye mikono ya boyfriend na kuimeza kwa kuhofia angeikamata simu.

Ilibidi akimbizwe hospitali na kufanikiwa kutolewa hiyo simu tumboni ambapo haikujulikana ni nini ambacho mrembo huyu alikua anakificha kwa boyfriend wake ila iliripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari duniani kwamba tayari mrembo huyu alikua na mwanaume mwingine nje ya uhusiano.

Source MillardAyo

Nimeisoma hii habari nikakumbuka mwaka 2011, nilikuwa na mchumba alikuwa akipigiwa simu na namba ambayo hajaisave, kila mara tunapokuwa pamoja na akipokea hajiamini anachokiongea. Mara nyingi anakuwa ni mtu wa mmh..., ndiyo..., hapana..., haya... and the like. Baada ya kumuuliza huyo anaekugipia simu unakosa kujiamini ni nani na kwanini hujamsave, nipe namba yake nimpigie.. Akafungua simu harakaharaka akatoa line na kuivunjavunja!!

Hebu na wewe tupe kisa chako kama imewahi kukutokea.
 
mapenzi bwana si bora angetupa au kuivunja kabisa aisee..

mimi sina kisa ni mwoga sana kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja so nikiona nimekuchoka nakutema naanza upya sipendi presha mimi
 
mapenzi bwana si bora angetupa au kuivunja kabisa aisee..

mimi sina kisa ni mwoga sana kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja so nikiona nimekuchoka nakutema naanza upya sipendi presha mimi

Hahah nawapenda sana wadada wenye hako katabia.. Anakuambia ukweli tu ili uchukue hamsini zako kuliko kupotezeana mda
 
mapenzi bwana si bora angetupa au kuivunja kabisa aisee..

mimi sina kisa ni mwoga sana kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja so nikiona nimekuchoka nakutema naanza upya sipendi presha mimi
Nahisi alikuwa anampenda sana boyfriend wake ila hawezi kuacha michupko au hawezi kusema NO kwa kila anaemwaproach.. Ikabidi ajilipue!
 
Kuna watu hawapo smart kabisa, kama unacheat be smart. huwezi kukamatwa kamwe.
 
unbelievable,kameza simu???kwa wanaojifunza unaweza kuwajua kirahisi ila waliobobea they know how to play their cards vizuri
 
unbelievable,kameza simu???kwa wanaojifunza unaweza kuwajua kirahisi ila waliobobea they know how to play their cards vizuri

Huyu itakuwa alikuwa mgeni kwenye game
 
asome tu yani nimeze simu na hizi simu za sikuhiz sijui inapitaje mdomon had ifike kwa koo niimeze
 
Back
Top Bottom