Visa na Mikasa ya Mitaani..........!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Visa na Mikasa ya Mitaani..........!!!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Ligogoma, Jul 16, 2011.

 1. Ligogoma

  Ligogoma JF-Expert Member

  #1
  Jul 16, 2011
  Joined: Aug 27, 2010
  Messages: 2,137
  Likes Received: 851
  Trophy Points: 280
  Habari wana JF??

  Wewe ni kijana umeoa miaka kadhaa iliyopita na mnaishi mkoa mmoja na wakwezo, umebahatikam kupata mtoto mmoja katika hiyo ndoa yako! Mkeo yupo karibu saaaana na baba yake kiasi kwamba wakati mwingine wanakuvurugia faragha na mkeo maana anamthamini sana baba yake!! Hilo si tatizo kumthamini mzazi ni jambo jema ila imepitiliza kiasi mkweo anaweza kaa kwako hadi saa sita usiku anaongea na baba yake we umelala!!!

  Hivi karibuni unapata taarifa kuwa baba mkwe wako anatembea na mwanae (kimapenzi) kwa maslahi ya utajiri wa familia yao, kwamba pindi wanapokutana kimwili utajiri unaongezeka kwa kasi kubwa.

  Wewe unajaribu kupata picha ya maisha halisi, wanasafiri wote nje ya nchi kama Nairobi, HongKong, Dubai n.k kuchukua biashara na wanakwenda wawili tu kisingizio mtoto (mkeo) ndiye mhasibu mkuu wa biashara zao! Awali hukuwa na hofu ukijua hapo ni baba na mwana!!

  Pili, huyu mtoto umemuoa lakini ishu zake zote za ndani ya ndoa ni kwa baba!! Mfano mkijadili kurekebisha nyumba mtapopata hela utashangaa kesho yake mkweo asubuhi asubuhi yupo hapo kwenu na mafundi wanaelekezwa namna ya kufanya marekebisho. Yaani matatizo yake kifupi hayaji kwako yanaenda kwa baba yake ukimuuliza kwanini kafanya hivyo ni ugomvi na msuluhishi ni baba na anamtetea mwanae kwa kila hali. Magari, anapewa leo hili, akiona kwenye internet jipya kalitaka na anapata bila tabu yoyote toka kwa baba na si wewe na hasa ukizingatia wewe ni mfanyakazi wa serikali unaetegemea mwisho wa mwezi!!!!

  Yote tisa, kumi mtoto wako kafanana vibaya mno na babu yake (mkweo) na hana elements zozote kuelekea kwenu, si mbaya ila baada ya kupata taarifa hizi unamwomba mkeo mwende DNA kumpima. Baba mkwe akaja juu vibaya kuwa kama humtaki mwane mwache ye atamlea lakini si kumnyanyasa nyanyasa mtoto na mjukuu wake.

  Mwisho ukawabana shemeji zako, ndugu wa mkeo wakakwambia waziwazi kuwa hilo lipo tena kabla ya wewe kumuoa (tangu binti akiwa form two) na ndo maana ndoa yako baba mkwe wako ndiyo anaicontrol na wakisafiri wanalala chumba kimoja kama mke na mume.

  Mama mkwe akakwambia waziwazi vumilia tu mwanangu maana mi mwenyewe nilisema nimechoka, nikajiona nitakufa kwa presha bure nimekaa kimya mradi maisha yanasonga sina neno na wewe uwe hivyo hivyo!!!

  Kama ndiyo wewe mwana JF utachukua hatua gani za haraka??? Kwa maelezo ya ndugu zao wamethibitisha sasa wewe utege mtego uwafumanie? Ujiondokee?? Au ufanyeje? Na nyumba unayoishi uliijenga wewe ila baada ya kumuoa huyu binti mkweo akaikarabati vikali ikawa nyumba moja nzuri sana!!! Utaiacha au??

  Ushauri wana JF
   
 2. maishapopote

  maishapopote JF Gold Member

  #2
  Jul 16, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 2,000
  Likes Received: 957
  Trophy Points: 280
  achana na huyo mwanamke kabisa ni laana hiyo
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Jul 16, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,465
  Likes Received: 19,847
  Trophy Points: 280
  navunja ndoa siku hiyo hiyo ...sitaki hata maelewano mna mtu.. mwanaume yoyote independent hawezi kuvumilia upuuzi kama huu
   
 4. First Born

  First Born JF-Expert Member

  #4
  Jul 16, 2011
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 5,315
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Baba anakula mke wangu basi na mimi nitafanya liwezekanalo nimle mke wake.
   
 5. s

  siwalaze Senior Member

  #5
  Jul 16, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 124
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  crapp crap!! Hilo sio suluhisho kaka!!
   
 6. s

  siwalaze Senior Member

  #6
  Jul 16, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 124
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Dah!!nimehisi kama maini yanakatika hivi!! Yaani si haba huyo mzee ni mchawi mkubwa!! Bila shaka kifuatacho ni KUONDOKA!!!
   
 7. Sokwe Mjanja

  Sokwe Mjanja JF-Expert Member

  #7
  Jul 16, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Sasa utaogopa kuachana nae sababu ya nyumba nzuri? Kwani hiyo nyumba si ulijenga mwenyewe kwa kazi hiyo hiyo ya serekali jama, achana nae tu na nakuhakikishia baada ya nusu mwaka utakuwa umeshakaa sawa kisaikolojia na Mungu atakufungulia njia. Huna haja ya kutaka kufumania sijui kuweka mtego, kwani si umeshahakikishiwa hadi na mama mkwe kuwa mzee anampakata mwanae? sasa unataka kufumania ili iweje, au upate habari ya kupeleka kwa Shigongo.
  Achana nae usiwe mtumwa wa nyumba au mali
   
 8. s

  seer Member

  #8
  Jul 18, 2011
  Joined: Apr 2, 2009
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ondoka wasije wakakutoa kafara na wewe!
   
 9. m

  mdhama Member

  #9
  Jul 18, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 48
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Wonders will never end! Chapa mwendo, mwache huyo mwanamke, waache na ushetani wao wanajua wanachopata! wasijekuingiza kwenye matatizo!
   
 10. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #10
  Jul 18, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  .....mh hii story mbona inafanana sana na story moja ipo pale Sinza kumekucha? lkn yule mzee alikufa mwaka jana au juzi km sikosei lkn mzee alikuwa anakula binti akamsomesha Uganda. baba mtu alikuwa anamsindikiza mtoto mpaka Uganga wanakwea pipa. alipomaliza mtoto akanunuliwa RAV4 short chasis wakati mama mtu anauza ubuyu nje ya nyumba, mzee ana pesa ukimwona mkewe utadhani hg, ila huyo binti alikuwa anathaminiwa vibaya mnoo. binti anatoka nyumbani kwa masharti, binti anamkoromea mama yake km mtoto mdogo, anamtukana mama yake, lkn mama ni mama tu akawa anamuachia mungu. binti akapata ujauzito mzee akaruhusu binti aolewe na bf wake. huyo mtoto jamani alivyofanana na babu yake khaaaaa. si mchezi. binti anamuita baba yake kwa jina lake la kwanza!!!! yule jamaa aliyeoa nadhani mpaka usawa huu atakuwa anaimba haleluya maana binti ana kiburi hakuna mfano. kaka wa binti alikuwa anaoa, huyo binti ndo alikuwa mwenyekiti wa kikao, imagine binti anamwambia mama yake mbele za watu, huyu mwanamke mbona mbishi hivi ntamchapa vibao, wewe huna pesa mimi ndo nai control hii harusi. dah iliniuma saana
   
 11. m

  mjasiria JF-Expert Member

  #11
  Jul 18, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 3,790
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Hizi stori zipo kweli?? Maana mi huwa nazisoma tu nakuzisikia kiasi huwa ninaona ni kama paukwa pakawa fulani hivi.
   
 12. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #12
  Jul 19, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Tembea uone ndugu yangu!
   
 13. m

  mjasiria JF-Expert Member

  #13
  Jul 19, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 3,790
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Nitembee wapi? Hebu nipe direction mkuu.
   
 14. fikramakini

  fikramakini JF-Expert Member

  #14
  Jul 19, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 247
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ningepigia nyumba bei na kuanza mdogo mdogo ...
   
 15. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #15
  Jul 19, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Jibu easy....Haiwezi tokea hiyo!
   
 16. Kwamex

  Kwamex JF-Expert Member

  #16
  Jul 19, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 378
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hizi story zipo kiongozi, Iringa nimeisikia moja ya dingi mmoja mfanyabiashara mkubwa iringa mjini kumla mwanae ila kilichotokea jamaa aliyeoa mtoto nadhani aliwafumania dingi na mtoto japo kitambo yalikuwa yanaongelewa dingi na mtoto wanamalizana jamaa akaona 'wana wivu hao' matokeo yake alikufa 'kiainaaina'. Watu wanatembea hadi na mama zao kisa utajiri haya mambo nasikia ukanda wa Iringairinga yapo sana.
   
 17. TECHMAN

  TECHMAN JF-Expert Member

  #17
  Jul 19, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 2,677
  Likes Received: 162
  Trophy Points: 160
  Kutokana na alie andika post hii si kwamba yeye yamemtokea ni simulizi tu. ILA naamini kuwa haya katika jamii yapo sana, kama alivyo andika, mara zote jambo kama hili lina kuwa na uhusiano wa kishirikina, katika matakwa binafsi si rahisi kwa mzazi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na binti alie toka katika viuno vyake hata awe mzuri na mna gani. Pia hutokea kwa wazazi wa kike kushiriki na watoto wao wa kiume katika mfumo huu huu. Japo kuwa nikweli wanafanikiwa katika maisha kama yalivyo malango yao, lakini panakuwa na mapungufu fulani katika maisha kutokana na asharti wanayopewa. Mara nyingi inapotokea wakavunja msharti hayo mali hupotea kiajabu au wanaweza kufa kabisa. Kwa wale ambao hawaamini hili, ni kuwa asilimia kubwa ya matajiri wanatumia nguvu mbadala ili kuweza kufanikisha mambo yao, nirahisi sana kuwajua kutokana na masharti waliyopewa. e.g unafanya kazi kwa tajiri, lakini akikulipa pesa anatumia mkono wa kushoto, au kama unadai pesa anauda maalum wa kutoa pesa mfano ukienda zaidi ya saa 12 jioni hatakupa pesa au kuna siku maalum hawezi kutoa pesa, hata kama unashida atakwambia mpaka kesho, duka likifungwa jiona wakati wa kuondoka hata kama wewe ufanyakazi wake umesahau ufunguo wa nyumbani kwako, duka halifunguliwi paka kesho, au akifungua duka asubuhi lazima yeye awe wa kwanza kuingia ndani kabla ya wote, nimeona wengine wanatabia ya kuchoma udi au ubani mara tu wafunguapo biashara zao.

  USHAURI. kama ikikutokea inabidi kuwa mwangalifu kwa uamuzi wowote utakaochukua, kwasababu ukiamua kuachana na huyo mwanamke au kama ni mwanaume, fika watajua kuwa umegundua mambo yao na wanaweza kukutoa kafara. CHAKUFANYA. tafuta sababu yeyote ambayo itasababisha yeye kukuacha, ukiamua mwenyewe kuacha, jaribu kumuepuka na kukaa mbali nae sana. kuna namna nyingi ila nashidwa kuandika nisije chosha wasomaji.
   
Loading...