Visa na mikasa ya kusisimua duniani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Visa na mikasa ya kusisimua duniani

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Pasco_jr_ngumi, Jun 20, 2011.

 1. Pasco_jr_ngumi

  Pasco_jr_ngumi JF-Expert Member

  #1
  Jun 20, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 1,811
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Kisa na Mkasa na Salim Kikeke
  Media Player

  Cheza katika media player
  Osama kusakwa


  Osama Bin Laden


  Mzamiaji mmoja wa Marekani, anajiandaa kwenda katika bahari ya Uarabuni, na kupiga mbizi kuusaka mwili wa Osama Bin Laden

  Mzamiaji huyo, Bill Warren, ameahidi kuzama hadi katika ardhi chini ya bahari na kuutafuta mwili wa kiongozi huyo wa Al-Qaeda, ili kuuthibitishia ulimwengu kuwa aliuawa kweli, limeripoti gazeti la New York Post.

  Bwana Warren ambaye amewahi kusaka meli na vyombo vingine vya baharini vilivyozama vipatavyo mia mbili, amesema anataka kuweka wazi ukweli wa jambo hilo.

  Bin Laden aliuawa katika mji wa Abbotatabad nchini Pakistan, na wanajeshi wa Marekani, waliosema baadaye kuwa walimzika baharini.

  Mzamiaji huyo anatazamia kutumia dola laki nne katika kipindi cha wiki mbili, mwezi ujao atakapoanza msako wake huo.

  "Mbona waliuonesha picha za Saddam Hussein?" ameuliza bwana Warren, ambaye rafiki wake wa kike anatokea Urusi, na amemuambia kuwa nchini humo hawaamini kama Osama kweli amekufa.
  Majirani wagomvi  Majirani wawili nchini Malaysia waliokuwa wakizozana kila mara walilazimika kutia saini makubaliano ya amani, kama yale yanayotumiwa na nchi zenye migogoro.

  Shirika la habari la Reuters limesema mzozo wa majirani hao wanaoishi katika jimbo la kusini la Johor umedumu kwa miaka mitatu, na hata polisi walishindwa kuusuluhisha.

  Gazeti la Star limesema, mzozo ulianza kufuatia jirani mmoja kuwa na mbwa waliokuwa wakipiga kelele, na jirani mwingine kujibu mashambulizi wa kufungua muziki kwa sauti ya juu.

  Hata hivyo baada ya miaka mitatu ya mzozo uliokuwa ni pamoja na kurushiana taka na hata kugonga mageti kwa kutumia magari yao, wawili hao waliamua kutia saini makubaliano ya maelewano au -- Memorandum of Understanding-- kwa kimombo.

  "Ikiwa mmoja wao atavunja makubaliano hayo, mkataba huo wa amani utatumika polisi au mahakamani" amesema msuluhishi wa mzozo huo, Michael Tay.

  Bila shaka sasa wataishi kwa amani ameongeza msuluhishi huyo, ambaye pia ni jirani yao.
  Mbwa tajiri afariki dunia  Mbwa tajiri kuliko wote duniani amefariki dunia.

  Mbwa huyo, aliyejulikana kama Trouble, amekufa akiwa na umri wa miaka kumi na miwili ambao ni karibu sawa na miaka themanini na tano kwa binaadam.

  Trouble alifariki akiwa anaishi kifahari huku akihudumiwa kikamilifu na wafanyakazi wake huko Sarasota, Florida, nchini Marekani.

  Trouble alipata utajiri wake kufuatia kuachiwa urithi na aliyekuwa mmiliki wake Leona Helmsey aliyefariki dunia mwaka 2007, na kumuachia majumba yake ya kifahari na dola milioni kumi na mbili.

  Bi Helmsey alikuwa mjane wa tajiri wa mahoteli, Harry Helmsey, aliyekuwa bilionea.

  Katika maisha yake, mbwa Trouble alikuwa akipata vitisho vya kuuawa au kutekwa nyara kutokana na utajiri wake na kulazimika kuwa na ulinzi mkali muda wote.

  Fedha alizoacha mbwa huyo sasa zitapelekwa katika wakfu wa Bi Helmsey ambao unasaidia mashirika ya misaada.
  Posho yakatwa  Serikali ya Malawi imesimamisha kuwalipa posho maalum wafanyakazi wa serikali wanaoishi na virusi vya UKIMWI.

  Kwa mujibu wa BBC, serikali ya Malawi imesema imeacha kuwalipa pesa taslimu, kwa sababu wafanyakazi hao hutumia fedha hizo kwa ajili ya kununulia pombe na makahaba.

  Afisa mmoja wa serikali amewatuhumu watu hao kwa kusambaza zaidi virusi vya UKIMWI.

  Serikali hiyo imesema, badala yake, wafanyakazi hao wapatao elfu arobaini, sasa watakuwa wakipewa chakula chenye virutubisho kila mwezi badala ya fedha taslimu.

  Inakadiriwa kuwa karibu asilimia kumi na tano ya wananchi wa malawi wanaishi na virusi vya Ukimwi.
  Nyoka nyumbani  Familia moja nchini Marekani imelazimika kukimbia makazi yao kutokana na nyoka.

  Mtandao wa Cnews.com umesema bwana Ben na mkewe Amber walinunua nyumba hiyo mwaka 2009, katika mji wa Idaho.

  Hata hivyo nyumba hiyo ilikuwa ina nyoka wengi kiasi kwamba kuna wakati wenye nyumba walikuwa wakihisi ikitikisika kutokana na nyoka hao kuzurura.

  Taarifa zinasema mamia ya nyoka walikuwa wanaishi ndani ya ukuta wa nyumba hiyo, na katika maeneo yanayozunguka hapo.


  Siku moja bwana Ben aliua nyoka arobaini na wawili.

  "Yaani tukasema sasa basi" amesema Ben, ambae wamelazimika kutangaza kufilisika, kwa sababu walinunua nyumba hiyo kwa mkopo wa benki.

  "Utadhani tulikuwa tunaishi katika nyumba ya shetani" Amesema Ben.

  Benki iliyowakopesha wawili hao hiyo nyumba, imeichukua nyumba hiyi sasa, na tayari imeingizwa sokoni, kwa yeyote anayetaka kuinunua...Na kupafanya nyumbani..
  Nywele zaibwa  Polisi nchini Brazil wamesema mwizi mmoja amemuibia nywele mwanamama mmoja wakati amesimama kituoni akisubiri basi.

  Polisi wamesema nyewe la bibie huyo zilikuwa za asili, na ambazo hazijatiwa dawa.

  Inspekta wa polisi Jose Carlos Bezerra da Silva amekiambia kituo kimoja cha Televisheni kuwa, mwanamama huyo alikuwa amesimama akisubiri basi katika jiji la Goiania, alipopatwa na mkasa huo.

  Mtandao wa Canadian Press umesema mwizi huyo akitumia kifaa kama kisu, alikata nywele za mwanamama huyo, ambazo zilikuwa ndefu kiasi zilikuwa zimepita hata usawa wa kiuno chake.

  Mwanamama huyo amesema, alikuwa akidhani mwizi huyo anataka kumuibia mkoba wake.

  Polisi wamesema, huenda nywele hizo zimeenda kuuzwa, ili kutengenezewa nywele bandia.

  Inspekta Silva amesema hajawahi kuona wizi wa aina hii.

  Amesema mwanamama huyo alilazimika kuripoti sakata hilo polisi, kwa sababu za kidini, kwa kuwa angelazimika kumuelezea kiongozi wake wa dini, kwanini nywele zake sio ndefu tena.

  Na kwa taarifa yako...... Bundi ana kope tatu za macho.

  Tukutane Wiki Ijayo.... Panapo majaaliwa...
   
 2. Wa Nyumbani

  Wa Nyumbani JF-Expert Member

  #2
  Jun 20, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 432
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Nimevipenda visa hivi
   
 3. Helper

  Helper JF-Expert Member

  #3
  Sep 27, 2017
  Joined: Dec 13, 2011
  Messages: 915
  Likes Received: 318
  Trophy Points: 80
  Huyo mzamiaji alifanikiwa?
   
 4. ze-dudu

  ze-dudu JF-Expert Member

  #4
  Sep 27, 2017
  Joined: Jul 26, 2014
  Messages: 6,097
  Likes Received: 4,675
  Trophy Points: 280
  mbwa tajiri hahahahaha
   
 5. s

  song 16 Member

  #5
  Sep 28, 2017
  Joined: Sep 10, 2016
  Messages: 61
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 25
  Àa
   
 6. Janma

  Janma JF-Expert Member

  #6
  Sep 28, 2017
  Joined: Sep 30, 2015
  Messages: 244
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 60
  wazungu bhana et mbwa tajiri kuliko wote
   
Loading...