Viroja vya BOLKIAH, Mfalme wa BRUNEI

Viroja vya BOLKIAH, Mfalme wa BRUNEI

Pia ni nchi inayoongoza wananchi wake kuwa na furaha, ni nchi inayoongozwa kufwata misingi ya kiislam, hakuna kuuza pombe lakini ukipatikana umelewa hufanywi chochote, kuna ka kisiwa kimojawapo kinachowatenganisha na Malaysia ni kama kilo mita 2 ndipo watu wanaenda kuburudika then wanarudi, kila raia anapewa mshahara na sheria zao zina kataza mtu wa nje kupewa uraia wa nchi. Na asilimia 80 ya wakazi wa kisiwa hicho ni wasomi wa kuanzia degree, ina wakazi 440,000 na huyo sultani ndiye kiongozi tajiri duniani.
Jina lake halisi ni (Sultan Haji Hassanal Bolkiah Mu'izzaddin Waddaulah ibni Al-Marhum Sultan Haji Omar Ali Saifuddien Sa'adul Khairi Waddien Sultan and Yang di-Pertuan) wa Brunei taifa lilopo mashariki kusini mwa bara la Asia.

Amekuwa sultan wa 29 wa Brunei yenye mji wake mkuu uitwao Darussalam kwa miaka 52 sasa tangu alipoingia madarakani mwaka 1967 kwa kumrithi baba yake.

Mwaka 1980 alitajwa na gazeti la Forbes kuwa mtu tajiri zaidi duniani akiwa na utajiri wa Dollar Bilioni 12.

Mbali na kuwa sultan pia ni waziri mkuu wa Brunei, pia ni waziri wa ulinzi, amiri jeshi mkuu, waziri wa fedha, waziri wa mambo ya nje na biashara.

Anamiliki magari mengi zaidi duniani. Kwenye yadi yake Kuna Ferrari 452, Koenigeggs 134, BMWs 209, Jaguars 179, Aston Martin 11, McLaren F1s 11, Lamborghini 21 na Rolls Royals 600. Kwa hivyo pia ana garage kubwa zaidi duniani.

Anamiliki na kukaa kwenye jumba kubwa zaidi duniani lenye ukubwa wa ekari 49, Vyumba vya kulala 1788 na mabafu ya kuogea 257.

Ni msomi wa hali ya juu akijikusanyia jumla ya shahada za awali (bachelor degree) 6, shahada za uzamili (Masters degree) 6 na shahada za uzamivu (PhD) 2.

Ameifanya nchi yake kuwa ya kwanza kwa wananchi kutokulipa kodi. Huduma zote za afya ni bure kwa watu wote. Hazina ya mafuta na utalii ndizo zinalisha nchi nzima.

Anamiliki ndege iliyotengenzwa kwa dhahabu yenye thamani ya pesa za kitanzania Shilingi Bilioni 520. Ndege hiyo ina sebule, vyumba vya kulala na bafu na choo. Yeye mwenyewe ndiye rubani wa ndege hiyo.

Anamiliki viwanda vya kusafisha mafuta zinazomuingizia kiasi cha Dollar 6,000 kila dakika sawa na Shilingi milioni 13 za kitanzania.
#Sky_videos_production_tzView attachment 1394689

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lamborghini
Kuna watu wengine wanakula
Pepo hapahapa duniani
Inshaallah

Sent using Jamii Forums mobile app
Madudu yote hayo anayaona saa ngapi? Yeye ameshakuwa babu, wanaoponda raha na vimwana ni wapambe waliomzunguka kumwimbia sifa.

Hata hiyo ndege huenda anapanda mara moja au mbili kwa mwaka. Wanaoponda maraha na anasa ni wapambe always.

Ndiyo maana wapambe wapo tayari kuua na kufanya unyama wowote ili waendelee kuponda raha.
 
Ninakupinga kwenye huduma za afya, kila mwananchi wa Brunei analipia US$1 kumuona daktari na gharama za dawa. Kama ugonjwa wako hautibiki Brunei, unapelekwa Malasia, Singapore au India kwa gharama za serikali.
 
Back
Top Bottom