Virai vya Kiswahili

mikedean

JF-Expert Member
Mar 15, 2018
3,255
4,599
Ni moja ya mada zinazochanganya sana. Baadhi ya sifa za virai ni kwamba hazina muundo wa kiima na kiarifu. Ndani ya kirai kunaweza kuwa na kirai kingine ndani yake. Mfano "watoto wanacheza kwenye mvua kwa mbwembwe".

Kwa kawaida kuna aina 5 za virai
1. Virai nomino (KN)
2. Virai vitenzi (KT)
3.Virai vielezi (KE)
4. Virai vivumishi (KV)
5. Virai vihusishi (KH).

Baadhi ya waandishi wanasema kuwa kuna virai viunganishi hiyo sio kweli.bali vile vinavyoitwa virai viunganishi ni virai vihusishi.mfano "Juma alisafiri kwa basi".kwenye sentensi hii kirai - "kwa basi". Ni kirai kihusishi sio kiunganishi.wengine wanasema kuna virai vihisishi.mfano masalaaale!, la hasha!loo! N.k.

Kirai ni neno au kikundi cha maneno ambacho hakina muundo wa kiima na kiarifu na pia kinaweza kutoa taarifa kamili au isiwe kamili.

Kuna utata mkubwa zaidi katika miundo ya virai. Mfano KN kinaiundwa na nomino 2.mfano "baba na mama/wanalima shamba". Hii haitakiwi inatakiwa useme kN inaundwa na nomino mbili zilizounganishwa na kiunganishi au unasema KN=N+u+N.

Kuna wengine husema kuwa kN inaundwa na N+T mfano."Juma anakula."Hii sio moja ya KN kwa sababu hapo kwenye sentensi kuna kiima na kiarifu.

Unajua nini kuhusu kirai tiririka hasa kuhusu utata mfano kategoria za virai na miundo mingine ya virai.



Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom