Munkari
JF-Expert Member
- Feb 9, 2013
- 8,084
- 4,365
Dah nimekumbuka mbali kidogo aisee sijui miaka ya ngapi ile !! Kulikuwa na maflana yenye picha za wanamuziki wa kikongo kama BONGOMANI,BOZIBOZIANA,AWILO ,nilikuwa na la Bongomani aisee nilikuwa nalipenda balaa..yapo wapi nowdays ?...,........-.........,..... kulikuwa na mashati yanaitwa BAWAMA yana pesa pesa kibao ya ujiuji hayapo siku hizi.........haya ukija upande wa urembo sijui ndo madawa yalikuwa hayajaingia loh! Akina dada/mama walikuwa wanachoma nywele zao eti ndo relaxer haha! Usiombe wakati wa sikukuu !!................ Kwenye maharusi sasa biharusi alikuwa anavaa skuna na soksi mkononi ana gloves hahaha kweli tumetoka mbali!!.........kwenye vipaimara binti bila gauni ya mashelashela na soksi ndeefu bado hajatokelezea hahaha! Ule mtindo wakuweka blue mashati ya shule sijui kama siku hizi bado unaendelea eti uonekane msafi aisee...nikumbusheni na vingine.....