nimetega na alarm kabisa ili kipindi kisinipite kinaanza kati ya jumatatu mpaka ijumaa kina simulizi za maisha halisi ya mikasa mizito ambayo watu wamepitia kwenye maisha yao, unakipata EFM RADIO kuanzia kumi na mbili na robo jioni mpk na dk 50. ni kipindi kifupi sana lkn kitakufanya ujifunze mengi kwny maisha mfano mdogo tu nikupe,imezoeleka kwenye familia wanadai mama ndo anajua baba halisi wa kila mtoto wake lakini kwenye simulizi iliyopita baba ndo alikuwa anajua siri kwamba watoto anaowalea si wakwake mpaka siku akamuweka chini mke wake kumueleza ukweli kwamba yeye si baba halisi wa watoto wao hali iliyopelekea kuvunjika kwa ndoa hiyo iliyodumu kwa miaka 14.