Vipimo vya posta vinadanganya au wanakisia?

Mlalahoi Mlalahai

JF-Expert Member
Jul 20, 2015
399
146
Mimi ni mmoja ya vijana ambao hutuma maombi ya kazi kwa njia ya posta hasa hii njia ya kawaida na vitu ambavyo huwa naambatanisha ni certified copies za vyeti, yaaani cheti cha kuzaliwa, cha O level, A level na cha chuo, pia passport size moja, na CV yenye pages 3 vyoote hivi huwa naviweka katika bahasha ya shilingi mia mbili.

Kinachonishangaza ni gharama za utumaji kwa njia hii ya kawaida katika vitu vile vile ninavyoambatanisha kila siku, yaani naweza kwenda nikaambiwa 1000, kesho 1500 keshokutwa 2000.

Sasa huwa najiuliza huwa inakuwaje hii, nilijaribu kuwauliza hawa jamaa wa hii posta ninayoitumia wakaniambia wao huwa wanapima ndo wananiambia gharama, lakini mi hubaki najiuliza inakuwaje katika viambatanisho vile vile ninavyoenda kutuma maombi bei zitofautiane?

Sijawahi kutuma maombi ambayo hayana mahitaji hayo niliyoyataja hapo juu. Sasa napenda kuwauliza ndugu zangu je vipimo vya posta vinadanganya au jamaa huwa wanakadiria tu?
 
Posta ni mojawapo ya majipu yaliyokwishaiva.Yanasubiri kumbuliwa hivi karibuni.
 
Leo tu nimetuma karatasi tatu zenye maandishi upande mmoja kila karatasi A4 songea to kigoma Tshs 13100, Wakati mwezi uliopita nyaraka hizo hizo 12500 kwa EMS
 
Ndio maana ntakomaa kubeba boksi huku kwa mda mrefu sana. Sababu zitakazomfanya Jesus arudi upesi sana kabla ya mda aliopanga ni sisi mitanzania
 
Back
Top Bottom