Zero IQ
JF-Expert Member
- Dec 21, 2016
- 13,985
- 25,204
Vipi ulishawahi kuchukia kwa lipi?
Binafsi kuna siku nilikuwa na shida kweli kweli nikamcheki mshikaji wangu kumuomba aniwezeshe na akanihakikishia ndani ya dakika 10 atakuwa tayari amenitumia hela,
Sasa basi kwa kuwa nilikuwa na shida kila dakika nilikuwa naangalia simu kama kuna sms yeyote imeingia maana ndani ya dakika hizo nilikuwa na uhakika lazima muhamala ungesoma,
Nimekaa kwa pressure kubwa nasubiri mtonyo mara pap sms hiyo kwa bashasha kucheki ili nijue kanitumia ngapi nakutana na Sms hii '' MIMI NI MGANGA KUTOKA SUMBAWANGA TUNATOA MIKOSI NA KUKUPA UTAJIRI,
TUNANG'ARISHA NYOTA ILIYOFIFIA, PIA TUNATIBU NGUVU ZA KIUME UKITAKA HUDUMQ ZETU NITAFUTE KWA NAMBA 0712________."
Aisee nilichukia sana siku ile japo pesa yenyewe niliipata kama masaa 2 mbele.
CC Zero IQ