Pole Mkuu Magobe, airtel ni wezi!. Nashauri tupeleke rasmi malalamiko yetu TCRA kwa huu sio tuu ni wizi, bali ndani yake kuna ujambazi na utapeli!.
1. Kwanza unaambiwa "nunua moderm kwa 30,000 utapata internet bure kwa miezi 6!".
2. Ukishalipia, unakutana na 1st surprise eti kumbe hiyo 30,000 ni moderm tuu!, lazima ununue bundle!, nikadaiwa 14,000!. Nikalipa nikijiaminisha kama kweli ni miezi 6, bado inalipa!.
3. Kwanza iko slow, pili within a week, hakuna cha bundle wala miezi 6!.
Nimetumia moderm mbalimbali!.
1. Vodacom wako expensive na sio fast sana!.
2. Sasatel unalipa 30,000 wanakupa moderm bure with 4 GB tatizo hawajaenea sana!.
3. TTCL ndio fastest, unalipa bundle ya 8 kwa wiki wanakupa 2GB, tatizo recharge voucher zao ni issue na ukisafiri hawana mtandao uliosambaa ni makao makuu ya mikoa tuu!.
4.Zentel pia wako fast, cheap ila nao hawasambaa sana.
5. Airtel ndio cheapest kwa ile bundle yao ya 2,500 kwa wiki, mimi nimewanunulia watoto wangu wakubwa 4, nikifikiri ndio nawasaidia kumbe kwao hata siku hawamalizi na hawa wadogo wawili nao wanajisogeza kwenye laptops za kaka zao kuzama kwenye net games hivyo naumizwa sana.
ushauri kama uko fixed dar tumia TTCL au Zantel, ukisafiri njiani tumia Voda iko kote ila lazima utoboke au zain ila utasuasua!.