Vipi tangazo lililo jamiiforums la modem ya Airtel kwa 30,000/- na free internet kwa miezi 6? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vipi tangazo lililo jamiiforums la modem ya Airtel kwa 30,000/- na free internet kwa miezi 6?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Magobe T, Jun 30, 2012.

 1. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #1
  Jun 30, 2012
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,743
  Likes Received: 248
  Trophy Points: 160
  Wadau, kuna tangazo hapa jamiiforums linasema: "Buy for only 30,000 Tsh and get free internet for 6 months. Visit any airtel shop." Naona hili tangazo linasema uongo maana jana nilinunua modem kwa 30,000/-, nikalipia bundle ya wiki moja lakini sikupata hiyo "free internet". Badala yake hela nilizolipia kwa bundle ya wiki moja 2,500/- ziliisha muda mchache baada ya kuweka. Sasa hiyo "free internet" kwa miezi sita iko wapi? Je, hawa njemba wanatudanganya ili watulie hela? Pia kuna offer ya Vodacom Tsh 7500 kwa 500MB. Je, waliokwishatumia mnashauri nini hapa? Nihamie Vodacom?
   
 2. SHIEKA

  SHIEKA JF-Expert Member

  #2
  Jun 30, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 7,997
  Likes Received: 753
  Trophy Points: 280
  Kuna mwanaJF mmoja alishaleta habari hapa kuhusu hizo modem za airtel. Hayo maneno ya internet bure miezi 6 ni changa la macho - hakuna kitu kama hicho - ni lugha ya biashara tu kukuvutia! Wee endelea na bundle zao tu.
  Kuhusu bendle za Vodacom, mimi natumia ile ya 2500 ya MG125. Lakini kama unadownload mavitu mengi inaisha kabla ya hizo siku 7. Kwenye hii ya vodacom huwa nabadilishabadilisha na BOMBA7 MB 750 kwa sh 10,000 kwa siku 7.

  Ni hayo tu ndugu kwa leo.
   
 3. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #3
  Jun 30, 2012
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  ....ni kwa sababu tu wahusika ni DHAIFU ndio maana makampuni yanaruhusiwa kutangaza uongo wa kuibia watu...!!
   
 4. paty

  paty JF-Expert Member

  #4
  Jun 30, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 1,212
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  HYGEIA bomba 7 inahusika sana mkuu , ndo inatuweka mjini
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. don-oba

  don-oba JF-Expert Member

  #5
  Jun 30, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 1,383
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Vigezo na masharti kuzingatiwa. Kidogo tu namimi niingie mkenge kununua. Ila nikatafakari, kweli ununue kwa alf 30 halafu upewe miezi 6? haiji akilini. Dingi yangu akanunua na anadai bora ile ya zamani. Natumia ya Voda, nanunua BOMBA7 buku ten raha mstarehe.
   
 6. manuu

  manuu JF-Expert Member

  #6
  Jun 30, 2012
  Joined: Apr 23, 2009
  Messages: 4,026
  Likes Received: 9,390
  Trophy Points: 280
  don-oba Wacha kutukosea heshima wazazi tulio humu jamvini hilo neno DINGI unamaanisha kitu gani?
  Ebu njoo kwa magoti na ututake radhi wazazi wote humu.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. Brightman Jr

  Brightman Jr JF-Expert Member

  #7
  Jun 30, 2012
  Joined: Mar 22, 2009
  Messages: 1,234
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  .........ndio waliwao! We hujui kuwa hiyo ni biashara ya watu? Funguka mkuu utafilisika...!
   
 8. l

  lubagash Member

  #8
  Jun 30, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 97
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 15
  kila kampuni inafanya itakvyo,hata kusema uongo kwani.hakuna wa kuwauliza.watetezi wa wananchi wote THAIFU.
   
 9. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #9
  Jun 30, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,014
  Likes Received: 558
  Trophy Points: 280
  Wao ndo wanatulipia tuwe hewani au tumekosea jamaa wa airtel watajibi
  Kubba msemo wa kichama wanatuomba tuhamie
   
 10. Borat69

  Borat69 JF-Expert Member

  #10
  Jun 30, 2012
  Joined: Jun 17, 2012
  Messages: 2,536
  Likes Received: 1,211
  Trophy Points: 280
  Nilishaleta hii mada pia lakini post yangu ikaishia kuhamishwa kwenye Jamvi la malalamiko na hakuna kilichofanywa na wahusika. Mleta mada ni mmoja wa wadau waliopigwa changa la macho kwa kununua hiyo modem kwa tangazo hili..it's a shame kwa wizi unaofanywa na AIRTEL huku wakipata hifadhi humu Jamii Forum.
   
 11. m

  mkupuo JF-Expert Member

  #11
  Jun 30, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1,219
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Mkuu magobe t. Mi naona liwalo na liwe! Pole sanna kwa zengwe walilokufanyia.
   
 12. congobe

  congobe JF-Expert Member

  #12
  Jun 30, 2012
  Joined: May 31, 2012
  Messages: 482
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  hawa jamaa wa airtel ni wezi tu kama wezi wengine nimenunua modem yao hadi leo ni siku 50 hivi zaidi ya mwezi wanodai wanatoa offer ya 6 miezi sijapata kitu
   
 13. R

  Rebel volcano JF-Expert Member

  #13
  Jun 30, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 404
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jf ipo juu,hilo tangazo safi sana linaendana na hali halisi ya mtanzania hahahahahahahahahahahhaahha,
   
 14. R

  RC. JF-Expert Member

  #14
  Jun 30, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 446
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kuna jamaa yangu nilijaribu kumuulizia kuhusu hizi modem akaniambia kua hiyo ofa ya miezi sita inaanza kila ikifika saa sita za usiku nikaudhika sikufatilia kama ni kweli labda mjaribu.
   
 15. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #15
  Jul 3, 2012
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,743
  Likes Received: 248
  Trophy Points: 160


  Du! Hwa njemba kiboko!Ni kama anayeenda baa kupta huduma na kukuta pombe bei Sh2,500 kwa halafu mhudumu wa luringa na choo hakivisafishwa karibia mwezi na bado wateja wanamiminika kuchapa maji na kumpa mwenye baa picha kuwa baa yake ina huduma nzuri. Ni kama daladala pia - gari chafu, konda mchafu na hajawahi kuoga kwa sababu ya kukosa nafasi kwa vile anatafuta 'chenji' ya mwenye gari na anapakia watu wanajaa mpa hakuna anayeweza kupimua vizuri. Halafu akisema: "wewe mwenye miwani sogea nyumba" unakuta mtu anasogea hata kama anajua hakuna nafasi. Hivi Watanzania tukoje? Tuna tatizo kichwani?
   
 16. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #16
  Jul 3, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 22,995
  Likes Received: 12,516
  Trophy Points: 280
  Pole Mkuu Magobe, airtel ni wezi!. Nashauri tupeleke rasmi malalamiko yetu TCRA kwa huu sio tuu ni wizi, bali ndani yake kuna ujambazi na utapeli!.

  1. Kwanza unaambiwa "nunua moderm kwa 30,000 utapata internet bure kwa miezi 6!".
  2. Ukishalipia, unakutana na 1st surprise eti kumbe hiyo 30,000 ni moderm tuu!, lazima ununue bundle!, nikadaiwa 14,000!. Nikalipa nikijiaminisha kama kweli ni miezi 6, bado inalipa!.
  3. Kwanza iko slow, pili within a week, hakuna cha bundle wala miezi 6!.

  Nimetumia moderm mbalimbali!.
  1. Vodacom wako expensive na sio fast sana!.
  2. Sasatel unalipa 30,000 wanakupa moderm bure with 4 GB tatizo hawajaenea sana!.
  3. TTCL ndio fastest, unalipa bundle ya 8 kwa wiki wanakupa 2GB, tatizo recharge voucher zao ni issue na ukisafiri hawana mtandao uliosambaa ni makao makuu ya mikoa tuu!.
  4.Zentel pia wako fast, cheap ila nao hawasambaa sana.
  5. Airtel ndio cheapest kwa ile bundle yao ya 2,500 kwa wiki, mimi nimewanunulia watoto wangu wakubwa 4, nikifikiri ndio nawasaidia kumbe kwao hata siku hawamalizi na hawa wadogo wawili nao wanajisogeza kwenye laptops za kaka zao kuzama kwenye net games hivyo naumizwa sana.

  ushauri kama uko fixed dar tumia TTCL au Zantel, ukisafiri njiani tumia Voda iko kote ila lazima utoboke au zain ila utasuasua!.
   
Loading...