mahirtwahir
JF-Expert Member
- Jan 12, 2013
- 614
- 322
Vikuba vya asumini,kaniletea tamasha
Mapenzi ya utotoni,leo kaja yakumbusha
Yanamwenda midomoni,kwa furaha na bashasha
Kaja omba samahani,vipi nimkatalie?
Hakosi kunahibika,yuko kwangu mikononi
Uso ameuvubika,yuko kwangu kifuani
Kama mwana amefika,kwa mama mwenye imani
Kaja omba samahani vipi nimkatalie
Naipenda sura yake,mzuri hana maringo
Mchesh hulka yake,atembea kwa mikongo
Apendeza kwa mwanya wake,tabasamu la maringo
Kaja omba samahani,vipi nimkatalie
Tatizo wazazi wake,ndio wanotuhasimu
Hawataki awabanduke,awe kwao dama dawamu
Asema ni mboni yake,kuichocha hajatimu
Kaja omba samahani,vipi nimkatalie?
Mapenzi ya utotoni,leo kaja yakumbusha
Yanamwenda midomoni,kwa furaha na bashasha
Kaja omba samahani,vipi nimkatalie?
Hakosi kunahibika,yuko kwangu mikononi
Uso ameuvubika,yuko kwangu kifuani
Kama mwana amefika,kwa mama mwenye imani
Kaja omba samahani vipi nimkatalie
Naipenda sura yake,mzuri hana maringo
Mchesh hulka yake,atembea kwa mikongo
Apendeza kwa mwanya wake,tabasamu la maringo
Kaja omba samahani,vipi nimkatalie
Tatizo wazazi wake,ndio wanotuhasimu
Hawataki awabanduke,awe kwao dama dawamu
Asema ni mboni yake,kuichocha hajatimu
Kaja omba samahani,vipi nimkatalie?