Vipepeo Weusi: Mkakati Namba 0034 (Simulizi)

Ilipoishia Episode 1

MIAKA MITATU ILIYOPITA

Ray, amefuatwa nyumbani kwao Mwembe Chai na watu wa kutatanisha na mmoja wao akiwa ni mwalimu wake wa chuo anayeitwa Dr. Shirima.
Watu hawa wanamuahidi kumsaidia kuweza kupata ufadhili kwa ajili ya kituo chake cha SOTE HUB, ufadhili ambao Ray ana uhitaji kuliko kitu chochote kile..
Wanampa ahadi ya kukutana nao, na Ray anafuata maelekezo na kuonana na watu hao na anshangaa kwani wanamchukua sampuli ya damu na alama za vidole na kisha wanampeleka sehemu vinapofanyika vikao vyao vya siri.! Watu hao waliojitambulisha kama The Board wanamshirikisha kuhusu walichomuitia, wanamkabidhi nyaraka yenye kichwa cha habari T.B.F.Q # 0034 aweze kuisoma na kuamua.!

Tuendelee..





Leo June 20, 2016. Morogoro

Kwa kawaida nikiamka asubuhi lazima nifanye mazoezi ya kukimbia walau kilomita tatu. Nilikuwa ndio nimerejea kutoka kwenye kukimbia na nimeshamaliza kuoga niko najiandaa kwa ajili ya kuianza siku nyingine ya utafutaji na kujenga taifa.

Kwa karibia miaka mitatu huwa najaribu kuishi siku zangu nikijitahidi kadiri niwezavyo niishi kana kwamba tukio lililotokea miaka mitatu iliyopita kana kwamba halikuwahi kutokea. Kikao changu na The Board. Siku niliyopelekwa katika jumba lao la kukutania na wakanionyesha nyaraka zenye kichwa cha habari T.B.F.Q 0034.
Kwa kiwango kikubwa nimefanikiwa kuishi kana kwamba siku hiyo haikuwahi kutokea, lakini ni siku kama ya leo ndizo ambazo zinanifanya nikumbuke kila sekunde ya siku ile miaka mitatu iliyopita, nikumbuke kila hatua niliyopiga kuelekea kwenye kikao kile. Ni siku kama ya leo ambayo natamani niifast forward nijikute nimeamka kesho yake pasipo kuiishi siku ya leo.

Nilikuwa nimeletewa Ujumbe na mtu kuwa Dr. Shirima anahitaji tuonane. Mara ya mwisho kuonana naye ilikuwa ni miezi mitatu iliyopita. Alinipa maelezo ya kufanya, na leo hii naamini naenda kupewa 'maelezo' mengine.
Toka siku nimehudhuria kikao chao kule Mikocheni B Dar es Salaam Dr. Shirima amekuwa akitaka tuonane anaandika kikaratasi na kumpa mtu aniletee. Niliwahi kumuuliza kwanini asinipigie simu, akanijibu kuwa kwa mtu makini kamwe usipitishe taarifa muhimu kwa njia za kielektroniki. Haijalishj unahisi kompyuta au simu yako iko salama kiasi gani, akipatikana mtu mwenye weledi wa kutosha anaweza kuidukua hiyo taarifa kwa urahisi tu.

Jana nililetewa kikaratasi nyumbani kwangu mtaa wa Mazimbu. Kikaratasi kiliandikwa kwa kifupi tu;

"Kesho. 10:00 PM. Nashera Hotel
D.S. 13"



Leo tukikutana kitakuwa ni kikao chetu cha kumi na tatu mimi na yeye Dr. Shirima (D.S) tangu siku nilipoingizwa kwenye mkutano wa The Board ingawa mpaka sasa bado nilikuwa sielewi wananihesabia kama nani kwao. Mwenzao, mshirika wao au kibaraka wao.
Binafsi siwezi kujihesabia kama mmoja wao kwa kuwa sijawahi kuhudhuria hata kikao kimoja toka siku ile ya kwanza au yafaa kusema sikuwahi kualikwa tena.

Kwa miaka mitatu yote mtu pekee ambaye nimekuwa nikikutana naye ni Dr. Shirima. Na kila nikionana naye alikuwa akinipa maagizo, fanya hiki, fanya kile.
Kila nilipomuuliza mimi wananichukulia kama nani, kama kawaida yake alitabasamu na kunijibu kwa utulivu "Wewe ni mwenzetu Ray"!
Bullsh*t.! Kama mimi ni mwenzenu kwanini na mimi sihudhurii vikao vyenu vya mafichoni, kwanini na mimi siji kwenye mikutano yenu nimevaa suti nyeusi na kipini cha dhambarau na kicha cha simba cha dhahabu kwenye ukosi wa koti la suti kama nyinyi?? Sikuwahi kumtamkia mdomono lakini hayo ndiyo yalikuwa mawazo yangu kila mara aliponijibu kuwa "wewe ni mwenzetu Ray".

Nilimalizia kujiandaa nifunga mlango ili nianze safari ya luelekea Nashera Hotel.

"Habari ya asubuhi Ray" Baba Bite alinisalimia.

Huyu alikuwa ni mpangaji mwenzangu. Nyumba yetu ilikwa imejengwa katika mtindo ambao, Kulikuwa na nyumba ndogo tatu (apartments) ndani ya uzio ila kila moja inajitegemea. Nyumba mbili zilikuwa ni nyumba za vyumba viwili na sebule, pamoja na jiko, na vyoo. Nyumba moja ilikuwa ni ya vyumba vitatu na sebule na jiko na vyoo.
Nyumba zote hizi Tatu zilikuwa ndani ya uzio mmoja wa ukuta.
Baba Bite na familia yake walikuwa wanakaa kwenye apartment ya vyumba vitatu. Alikuwa na mkewe, mtoto mmoja wa kike wa miaka minne aliyeitwa Beatrice lakini tulizoea kumuita Bite.

Apartment nyingine inayofanana na yangu yenye vyumba viwili na sebule, waliishi jamaa mmoja na demu wake. Yes demu wake kwa maana "wamewekana kinyumba" tu hawana ndoa. Walikuwa ni wahitimu wa Chuo miaka michache iliyopita. Hawa walikuwa wanaakisi kabisa maisha ya vijana wengi wa kitanzania waliomaliza vyuo na kufanikiwa kupata kazi. Walikuwa na ratiba ya kila 'bata' hapa mjini Morogoro. Kuna kipindi mpaka huwa najiuliza wanafanyaje kazi? Maana kila jumatatu wanaamka na 'hangover' sijui huko ofisini kwao wanafanyaje kazi. Ikifika ijumaa, bata linaanza mpaka jumapili usiku mnene. Kwahiyo siku pekee niliyokuwa na uhakika labda wanafanya kazi kwa uhakika ilikuwa ni Jumanne, Jumatano na alhamisi.
Mwanaume ni afisa mikopo FINCA na 'demu' wake yupo Ofisi za Tigo Huduma kwa Wateja hapa Morogoro.

Lakini Baba Bite na familia yake walikuwa tofauti sana. Walikuwa wanaakisi familia ambayo kila mtu angelipenda kuwa nayo. Walikuwa ni wacha Mungu pia. Sijawahi kumuona Baba Bite amechelewa kurudi kwake. Sikuwahi kuwasikia wanagombana, labda wagombane kimya kimya wenyewe kwa adabu. Tofauti na 'bwana yule' na demu wake, kila baada ya siku mbili utasikia anamfokea demu wake "we fala ntakuzibua ujue".


Baba Bite alikuwa na duka 'hardware" mjini na mkewe Mama Bite alikuwa mwalimu wa shule ya Sekondaei Kihonda. Ingawa walinizidi umri lakini hawakuwa watu wazima, Baba Bite mwenyewe kwa muonekano alikuwa hazidi miaka 36 na Mama Bite hazidi miaka 32.

"Salama kabisa, mmeakaje?" Nikaitikia salamamu ya baba bite.

Tukasalimiana na kuongea mawili matatu kisha nikawasha gari na kuondoka. Saa ilikuwa inaonyesha saa tatu kasoro robo. Nilikuna saa moja na dakika 15 kabla ya kikao changu na Dr. Shirima.
Nikaendesha gari huku nikiwaza kuhusu jirani yangu Baba Bite. Kuna jambo lilikuwa linanisumbua rohoni mwangu kuhusu yeye lakini sikujua ni kitu gani.
Labda ni kwasababu mara kadhaa nikiwa mjini nimewahi kupita kwenye duka Alilonielekeza kuwa ni lake, lakini karibia mara nne zote nilizofika ili nimsalimie nikajibiwa "ametoka".
Labada ni kwasababu sijawahi kumsikia ana pilika pilika za kwenda kununua mzigo mpya, kitu ambacho kilinishangaza. Tanzania hii wafanyabiashara wetu hata akiwa anauza soksi lazima akutambie "kesho nasafiri naenda kuchukua mzigo"
Sikujua ni nini kiliisumbua roho yangu kuhusu Baba Bite.

Labda ni kwasababu siku moja majirani zetu, yule jamaa na demu wake baada ya kuanzisha ugomvi huko kwenye bata zao, 'wazee' wakawasweka lock up. Kwa vile hawakuwa na ndugu hapa Morogoro, tukapigiwa simu sisi wapangaji wenzao. Nakumbuka namna ambavyo nilimbembeleza OCD awaachie nikafikia hatua mpaka ya kutaka kutoa rushwa, kwa ajabu OCD akanibadilikia na kutaka kunitia mimi pia lockup kwa kutaka kumuhonga. Nakumbuka dakika chache baadae akaja Baba Bite, akaingia ofisini kwa OCD. Sikujua waliongea nini, lakini kama dakika kumi baadae walitoka wakiwa wanatabasamu na OCD akiongea naye kwa heshima kubwa. Nakumbuka jinsi OCD alivyoamuri askari wake wawaachie mara moja wapangaji wenzetu wala bata na tukarudi nao nyumbani.

Kuna jambo lilikuwa linanisumbua sana rohoni kuhusu Baba Bite, lakini sikuweza hata kuhisi ni jambo gani.

Dakika kumi baadae tayari nilifika ofisini, ghorofa la Hajram mtaa wa Boma Road. Ofisi yetu ilikuwa gorofa ya tatu.
Dr. Shirima na wenzake walikuwa wametimiza ahadi yao ya kunitafutia wafadhili. Na kwa miaka miatu sasa ofisi yetu inekuwa inapokea funds kiasi cha dola laki mbiki kila mwaka kutoka mfuko unaoitwa Alice Cartz Foundation ya nchini Australia kwa ajili ya kuendesha projects za kusaidia vijana wajasiriamali na kuendesha ofisi, yaani kulipa mishahara, pango na kadhalika. Mpaka sasa ofisi ilikuwa na wafanyakazi wa kudumu nane.

Nikafika mapokezi na kumsalimia Dada Hadija, mdada wetu wa reception kisha nikafungua mlango wa kuingia ofisini. Ofisi yetu tuliitengeneza katika mtindo ambao ukiingia tu unakutana na ukumbi ambao kuna cubic za wafanya kazi, au yafaa zaidi kusema meza za wafanya kazi. Tulikuwa tunapata funds za kutosha hivyo pia tulijitahidi kuitengeneza ofisi ivutie haswa.

Kila meza moja ilikuwa na wafanyakazi wawili waliokaa huku na huku. Na kila meza ilikuwa ni 'department'. Ukiingia mbele yako mkono wa kushoto unakutana na meza yenye wadada wawili, hii ilikuwa ni department ya 'Marketing and Branding', mbele yake kuna meza yenye mkaka na mdada hii ilikuwa ni department ya 'Monitoring and Evaluation'.
Upande wa kulia mwanzoni kuna meza yenye mdada na mkaka pia hawa ndani ya ofisi tuliwatunga jina 'anchors', kazi yao ilikuwa ni kusaka vijana wenye Idea za tofauti na kuwaunganisha na ofisi yetu. Mbele yake kulikuwa na meza yenye wakaka wawili, hii ilikuwa ni idara ya fedha na uhasibu.

Nikawasalimia wote, tukataniana mawili matatu kisha nikaingia ofisini kwangu. Ofisi yangu ilikuwa inajitegemea, ina mlango wa kioo ambao unaweza kuona hata ukiwa nje na upande wa dirisha, ukuta karibia wote ulikuwa ni dirisha la kioo.
Nikaketi katika kiti na kabla sijafanya chochote akaingia Hadija mdada wa reception. Kama ilivyo kawaida alikuwa ameniletea magazeti ya siku ya leo.
"nikuandalie chai?" Akaniuliza baada ya kuweka magazeti kwenye meza. "Yeah, ya rangi, and ya mkono mmoja tu" nikamjibu nikiamaanisha anipe chai tupu ya rangi.

Alipotoka nikaanza kupitia magazeti, na cha kwanza nilichokiona kwenye magazeti yote ilikuwa ni kuungwa mkono kwa hoja binafsi ya Mbunge Zephania Zuberi huko bungeni Dodoma. Karibia wiki mbili zilizopita Mbunge machachari, Mheshimiwa Zephania Zuberi aliwasilisha bungeni hoja binafsi aliyoiita "Uwezeshaji wa kimkakati kwa Makampuni ya Vijana Wazawa".
Katika hoja hii Mheshiwa Zephania aliitaka serikali kupitia waziri mkuu, wakubaliane na hoja yake na kuweka mkakati wa makusudi kuhakikisha kuwa vijana waliothubutu kuanzisha kampuni ndogo za kibiashara wanapewa sehemu ya mikataba serikalini na katika sekta binafsi.

Hoja yake ilikuwa kwamba, kwa mfano tuseme kuna kampuni ya kichina imepewa tenda na serikali kujenga barabara, linapokuja suala la kununua kokoto kwa mfano, kampuni hiyo ipewe sharti kuwa lazima waingie mkataba na kampuni inayomilikiwa na vijana wazawa kwa ajili ya kusupply kokoto hizo.
Vivyo hivyo kwenye halmashauri za wilaya, Mheshimiwa Zephania akamtaka Waziri |Mkuu aiagize TAMISEMI kuamuru halmashauei zote nchini ziwe zinatoa walau 20% ya tenda kwa kampuni za vijana wazawa. Yaani kwa mfano halmashauri ikitaka kununua vifaa vya ofisi na kuna vijana wana miliki kampuni ya stationaries kwenye wilaya husika basi tenda hiyo wapewe vijana hao.

Hoja hii iliungwa mkono kila kona ya nchi na kila mtu. Asasi zisizo za kiserikali zikaandaa mijadala kuunga mkono hoja ya Mheshimiwa Zephania. Wanaharakati wakapaza sauti kuishinikiza serikali kukubaliana na hoja hiyo. Kwa mara nyingine tena mheshimiwa Zephania akawa shujaa katika nchi.

Nilipokuwa nasoma habari ya kukubaliwa kwa hoja hii na serikali, nilitabasamu. Nikacheka. Nikajisemea kimoyo moyo "kumekucha".

Kimsingi The Board kupitia Dr. Shirima walikuwa hawanitamkii moja kwa moja mipango yao. Lakini uzuri ni kwamba mimi mwenyewe sikuwa mtu wa mchezo mchezo kichwani. Niliweza "kuconnect dots".

Miezi mitatu iliyopita katika kikao chetu cha 12 mimi na Dr. Shirima alinipa maagizo kadhaa.
Katika kipindi hicho ndani ya SOTE HUB tulikuwa na mchakato wa kuchagua vijana ambao watapata ufadhili wa miradi yao kwa mwaka huu 2016.
Dr. Shirima alinipa maelezo kuwa kuna kuna "vijana" watatu wataomba kuwepo chini ya SOTE HUB natakiwa niwapitishe. Nakumbuka tulibishana sana kwani katika programu yetu tunachukua vijana watano pekee kila mwaka, hivyo akisema nichukue "watu wao" watatu hii inamaanisha tutabakia na nafasi mbili pekee kuweka vijana wenye uhitaji halisi.
Dr. Shirima akakomalia hoja yake kuwa tutafanya hivi kwa miaka miwili pekee kisha watatuacha tuendelee na mipango yetu vile tunavyotaka. Mwishoni sikuwa na namna zaidi ya kukubaliana kupitisha "vijana" hao wanaowataka.

Vijana hao walikuwa ni Maximilian Anga, huyu alikuwa ni "mchawi" wa kompyuta. Alikuwa ameanzisha kampuni yake ya teknohama aliyoiita Max tech.
Wa pili alikuwa ni George Ole Nangoi. Huyu alikuwa ni kijana wa kimasai aliyeanzisha kampuni ya ulinzi iliyohusisha ulinzi binafsi, na ulinzi wa mali. Kampuni yake ilijikita zaidi kutumia Morani wa kimasai badala ya walinzi wa kawaida wanao beba silaha za moto. Kamapuni yake iliitwa Moran Warriors Security.
Kampuni ya tatu ilikuwa ni ya kijana wa kike aliyeitwa Aisha Mzava, muhitimu wa chuo kikuu SUA shahada ya Agribusiness. Alikuwa amewachukua wahitimu wenzake wengine watatu na kuanzisha kampuni ha kutengeneza na kuuza madawa na mbegu za kilimo.

Hao ndio "vijana" watatu akionitaka niwapitishe miezi mitatu iliyopita tulipoonana na nikitekeleza hilo.

Leo hii nakutana na habari iliyopamba kurasa za mbele za kila gazeti kuhusu hoja ya Mheshimiwa Zephania "Uwezeshaji Wa Kimkakati Kwa Vijana Wazawa". Nikahisi hapa kuna kitu The Board wamelenga, ubaya ni kwamba hawawezi kunieleza. Pia nikashangaa jinsi habari hii ilivyopewa kipaumbele kwenye media zote. Nikawa na hakika lazima Mzee Bernad Shayo amehusika kuipatia umaarufu hii habari.
Swali nililojiuliza, wanalenga nini? What’s their plan??

Wakati nikiwa bado napitia magazeti na kutafakari hili na like, Hadija akarudi na chupa ya chai na kikombe. Nikaangalia saa, ilikuwa saa nne kasoro dakika tano.
"Sh****ttt" nikajikuta nimeropoka. "Sory Hadija sitaweza kunywa chai nina appointment na mtu saa nne kamili na nishachelewa". Nikaongea huku nanyanyuka haraka haraka na kutoka nje.

Dakika kumi baadae nilikuwa napaki gari ndani ya Nashera Hotel. Baada ya kushuka tu kuna gari ikaniwashia taa mara mbili. Nilipoiangalia nikagundua ni V8 ya Dr. Shirima.
Nikaifuata na kufungua mlango na kuingia ndani.

"Well, this is new! Leo kikao kwenye parking ya magari?" Nikaaanza kufungua maongezi kwa swali kabla hata ya salamu.
"Well, Ray mimi mtaalamu wa uchumi na uchumi is all about namna ya kumanage rasilimali na naomba nikwambie wengi wanadhani fedha ndio rasilimali kubwa zaidi lakini ukweli ni kwamba hakuna rasilimali adhimu kama muda!! Umechelewa dakika tano, nilikuwa nataka kuondoka." Dr. Shirima akiongea kama kawaida yake huku anatabasamu.
"Ok ok ok, nice speech! Am here now.. Shikamoo!"
"Marhaba, umesoma magazeti ya leo" akaniuliza.
"Yeah nimemsoma shujaa wenu jinsi alivyoishawishi serikali, i guess ndio sababu tunaonana hapa leo".
"Yeah na kwakuwa umechelewa naomba niende moja kwa moja kwenye agenda."
"Ok.." Nikamjibu kwa kifupi huku namuangalia nikisubiri maagizo kwa shauku kubwa. Nilikuwa natamani walau nipate clue ya nini wanakilenga.

"Ok, nadhani unafahamu kuwa kampuni za vijana zilizo chini yenu hawawezi kuomba kandarasi wala kusaini mkataba pasipo SOTE HUB kuridhia, so ninachotaka mfanye ni kwamba muombe kandarasi hizi kwa zile kampuni tatu nilizo kueleza uzipitishe kikao chetu kilichopita." Dr. Shirima akaongea huku anatoa makaratasi kwenye mkoba na kunikabidhi.
"Hizo ni tenda za serikali na kampuni binafsi hazijatoka bado lakini zinatangazwa wiki ijayo, hiyo ya kwanza ni tenda kutoka kampuni ya Swala Energy, naamini unaifahamu?" Akaniuliza.
"Yes, naifahamu" nikamjibu, naifahamu vizuri sana Swala Energy, kampuni inayofanya utafutaji wa mafuta katika bonde la ufa eneo la Kilosa.

"Ok, siku chache zijazo watatangaza tenda kwa ajili ya kuhitaji ulinzi katika maeneo yao huko kilosa nataka muombe tenda hiyo kwa niaba ya George Ole Naiko na kampuni yake ya Morani Worriors Security" Dr. Shirima akaongeza.

"Ok.." Nikamjibu kwa kifupi huku naipitia haraka haraka ile document ya tenda ya Swala Energy.

"Hiyo document nyingine ni tenda ya benki kuu pamoja na hazina, wanataka kampuni ya kuwasaidia kuboresha mifumo yao ya kompyuta." Akaongea huku anatabasabu akijua wazi nitakuwa na swali.
"Benki kuu na hazina wana wataalamu wao wa IT sijawahi kusikia wanatoa kandarasi kwa kampuni binafsi" nikamuuliza kwa mshangao.
"Usijali kuhusu hilo Ray, tenda itatangazwa wiki ijayo na unatakiwa umuombee Maximillian Anga Yule kijana wa Max tech."
"OK.." Nikamjibu tena kwa mkato.

"Hiyo tenda ya mwisho ni ya wizara ya kilimo, actually ni kama tangazo maana maombi yenyewe yanatumwa kwa mkuu wa mkoa, lakini wiki ijayo litatoka tangazo kwa kampuni za kilimo kuomba zabuni ya kusambaza mbolea na mbegu za kilimo, nataka umuombee Aisha na kampuni yake, na uombe mkoa wa Lindi."

"Hahahah Dokta naheshimu sana weledi wako lakini lazima ukumbuke kuwa hizi kampuni bado ni changa hata kama serikali inataka kuanzaka kuzingatia hiyo sera mpya iliyopendekezwa na Mhe. Zephania lakini sidhani kama wanaweza kutoa zabuni kubwa hivyo kwa kampuni changa." Nikamueleza huku nikicheka kicheko chepesi.

"Ray, jukumu lako ni kuomba hizo zabuni suala la kukubaliwa liache kwetu." Akaongea akiwa serious. Baada ya sekunde kadhaa akaanza tena kutabasamu na aligundua nina swali. "Uliza Ray, najua una swali."

"What's your plan?? Najua hamuhitaji hivi vijihela vya chai, mna mpango gani?" Nikamuuliza basi tu kwa vile nilishindwa kukaa nalo rohoni lakini nilijua fika hawezi kunijibu.
"Ray, unajua siwezi kukujibu hilo swali or at leats nor here." Dokta akajibu huku anatabasamu.

"Ok kama huwezi kunijibu hapa unaonaje sasa mkiniruhusu nije kwenye vikao vyenu ili nami nielewe kinachoendelea?" Nikamjibu huku naonyesha kukereka.
"Ray, huwezi kuja kwenye kikao kwasababu Chairman hajakualika" Dokta akanijibu kwa kifupi.

"Chairman, chairman, kila siku chairman hivi mara chairman vile! Who is this guy anyway? Ndiyo yule aliyeingia na msafara na walinzi kama Mkuu wa nchi siku ile?? Who is this guy??" Nikaongea kwa kukasirika na kukereka.
"Ray, inabidi niende sasa tafadhali shughulikia hayo niliyokueleza ASAP." Dr. Shirima akaongea huku amerelax na kutabasamu huku anawasha gari.

Tukaagana nikashuka kwenye gari na kureje kwenye gari yangu. Nikasubiri kama dakika tano hivi baada ya dakika kama tano baada ya dokta kuondoka na mimi nikawasha gari na kuondoka.

Njiani nikawaza sana ni nini kilikuwa kinapangwa na The Board. Kwa hakika hawakuwa wanahitaji hizo zabuni kwa sababu ya pesa, kuna jambo kubwa walikuwa wamelipanga nyuma yake. Ni nini hasa lengo lao?? Nikawaza na kuumiza kichwa bila majibu. Nikaunganisha haya matukio bado sikupata jibu kabisa.
Katika kuwaza huku nikakumbuka tukio lililotokea mizezi sita iliyopita ambapo kwa wakati ule nililiona la kawaida lakini sasa lilianza kunitia mashaka kama lina mahusiano na kinachopangwa kufanywa na The Board.

Miezi sita iliyopita baba yake Hasnat, cheupe wangu, Mhandisi Jaffar Kumbea alichaguliwa kuwa mjumbe wa bodi ya TPDC, shirika la mafuta nchini.

Sikuona kama kuna uhusiano wowote na zabuni nilizoambiwa niombee vijana wetu wizara ya kilimo, benki kuu na hazina lakini sasa nilianza kuona uhusiano japo kwa mbali na maagizo niliyopewa na kumuombea George Ole Nangoi wa Morani Worriors Security, tenda ya Ulinzi katika kampuni ya utafutaji mafuta ya Swala Energy.

Nikarudi ofisini. Kazi zikaendelea. Wiki mbili zikapita, matangazo ya zabuni yakatoka. Tukawaombea vijana na kampuni zao, hapa niseme hata wenzangu walinishangaa kuomba zabuni hizo ila walishindwa tu kunizuia kwa kuwa nilikuwa bosi wao. Tukaomba, na kusubiri majibu.

*******************************************

Zilikuwa zimepita takribani wiki tatu toka nionane na Dr. Shirima. Kwa kiasi fulani maisha yalikuwa yamerejea katika hali ya kawaida.
Niliamua siku ya leo nitoke out na cheupe wangu na ili out yetu iwe ya kufana niliamua kuomba ushauri kutoka kwa majirani zangu pale nyumbani, yule jamaa na demu wake, wala bata 'profesheno'.
Nakumbuka kauli ya jamaa alivyo nijibu "ishu za kumpeleka demu wako kwenye 'nice dinner' hizo tabia za kike na umbulura. kama unataka dinner si mpike tu wali nyama mle mlale, kama tunaenda out inabidi iwe ni kula bata la uhakika".
Kwa kuwa yeye ndiye profesheno kwenye sekta hii nikafuata ushauri wake.
Kwa pamoja wote, mimi na cheupe na jamaa na demu wake tukaenda 'kula bata'. Jamaa anaitwa Tony na demu wake anaitwa Grace.

Tulipokuwa tunatoka cheupe, alianza kuwa na wasiwasi kama hili lilikuwa na wazo zuri! Lakini kadiri usiku ulivyokuwa unayoyoma nilimuona anaanza kuinjoi. Tulianzai Down Town Club, tukavuruga vya kutosha kisha presheno Tony akashauri twende Nyumbani Park au kama watoto wa Moro wenyewe wanavyopaita, "samaki samaki". Nako tukavuriga vya kutosha. Mishale ya saa saba kasoro ilibidi kuwalazimisha Tony na Grace kweli kweli mpaka wakakubali tuondoke kurudi nyumbani.

Kwa kawaida huwa sinywi pombe wala cheupe wangu naye hatumii, lakini usiku huu nilijikaza nikabugia Windhoek mbili, na shots kadhaa za whisky nisiyoijua ninachokumbka ni profesheno Tony alikuwa analeta kila baada ya dakika kadhaa. Cheupe naye alikunywa bia mbili ila pombe kali nikampiga marufuku asiguse. Nikakumbuka jinsi alivyo na "kichwa chepesi" asije akaanza kuharibu.
Tony na demu wake sijui walimaliza kreti ngani, sijui ndio nilikuwa nimelewa au maluwe luwe tu, maana nilimuhesabia Tony na demu wake karibia kreti mbili kasoro walimaliza.
Siku ikaenda vizuri kabisa.

Tukaanza safari ya kuondoka Samaki Samaki kurejea mazimbu. Japo kuwa nilikuwa na pombe kiasi kichwani lakini huwa simuamini mwingine yeyote aendeshe zaidi yangu katika mazingira ya namna hii, walau mimi nilikuwa na afadahali. Dakika kama kumi na tano tayari tulikuwa Tumefika Mazimbu FK mtaani kwetu. Kana kwamba Baba Bite alikuwa anatusubiri, alifungua geti hata kabla hatujapiga honi.

"Asante sana Mkuu." Nilimshukuru Baba bite nikiwa naingiza gari ndani. Baba Bite hakuitikia. Sikujua kama ni pombe ama nilikuwa naona sahihi, nilipoangalia usoni kwa Baba Bite niliona hali Fulani hivi ambayo sijawahi kumuona nayo tangu nimfahamu. Alikuwa kama na hali ya wasi wasi, Iliyochanganyika na huzuni pamoja na hasira. Nilitamani nimuulize lakini kwa kuwa tunaheshimiana sikuona vyema kuongea naye nikiwa na pombe kichwani.

Nikapaki gari tukashuka wote, Tony na demu wake wakaingia ndani kwao na ndani ya dakika chache tu nikasikia wanaanza kutukanana.
Na mimi na cheupe wangu tukaingia ndani. Nikajitupa juu ya sofa na cheupe wangu akanirukia akakaa juu yangu. Na macho yenye ulevi kwa mbali akaniangakia moja kwa moja ndani ya macho kwa muda mrefu sana, "thank you kichwa" hatimae akaongea..
"For what?" Nikaongea nikijibalaguza kama sielewi. Moyoni tu nikitamani kusikia anayatamka maneno yale tena na tena.

"For today, for every day, for being my man! Nakupenda sana kichwa?" Akaongea huku anashusha kichwa chake taratibu mdomo wake ukikaribiana na wa kwangu.
"Nakupenda zaidi cheup…" Kabla sijamaliza midomo ilikuwa imekutana.
Kabla sijafaidi zaidi utamu wa lips na mate yake Mara akainuka "hey, ngoja nijimwagie maji kichwa chepesi kinoma usije ukaniua hahahah" akainuka kutoka juu yangu na kuanza kuondoka sebuleni. Nikamsindikiza kwa macho yenye ulevi kwa mbali huku natabasamu. "What?" Cheupe akasimama na kuniukiza.
"Leo utajuta kunifahamu" nikamwambia kwa utani huku nikijitahidi kuongea kimahaba.
"Hahahaha dooh" cheupe akacheka na kuingia bafuni.

Baada ya cheupe kutoka kwenda kuoga sijui ni kiherehere gani kikanikuta nikachukua simu na kuanza kuperuzi mitandaoni. Nikaingia instagram, hakuna kilichonivutia, nikaingia facebook, yale yale. Nikaingia mtandao wa jamii forums.. Baada ya kuingia tu nikaenda moja kwa moja kwenye 'Recent Posts'. Juu kabisa kama kawaida nikaona mada za "kila siku", sikumbuki vizuri lakini nahisi kulikuwa na mada "Natafuta Mume", chini yake kulikuwa na nyingine "Mkewangu ana wivu sana nifanyaje?". Nikaendelea kushuka chini. Kama post ya nne au ya tano hivi nikaona post ilifanya moyo wangu ulipuke. Iliandikwa "BREAKING NEWS: Waziri ameuwawa mda huu".

Kwa haraka sana nikaifungua. Ndani ilikuwa imeandikwa mistari aliyepost alikuwa na nia ya kuwa wa kwanza kuleta habari hiyo; "Habari za uhakika nilizo nazo, Waziri wa Nishati amevamiwa na watu wasiojulikana na kupigwa Risasi mda huu hapa Ubungo mataa, source: Mimi mwenyewe”

Nikashusha chini nione 'comments' za watu na comment ya kwanza iliandikwa na mtu ambaye nilishindwa kulisoma jina lake lote, niliambulia herufi za kwanza tu, GENTA….. aliandika "mods ondoeni huu uzushi"!
Nikashuka chini kuangalia comments nyingine, zote zilikuwa na mtazamo huo huo.

Ikabidi nirudi juu nione jina la mleta habari, nikakuta anajiita MSAGA SUMU.
"Pumbavuuuuuuu" nikajikuta naongea mwenyewe na kuanza kucheka. Moyo wangu ukatulia, presha ikashuka. Maana nilishaanza kuwaza mengine kabisa kichwani.

Mara nikasikia mlango unagongwa. "Nani?" Niliuliza huku bado nimeketi kwenye Sofa.
"Baba Bite" alijibu aliyekuwa anagonga.
Nikaangalia saa kwenye simu, ilikuwa saa saba na dakika ishirini. Nikajiuliza jirani yangu anataka nini au ana shida gani usiku wote huu. Nikaenda kufungua.

"Vipi mkuu salama?" Nikamuiliza baada ya kufungua mlango.
"Salama tu, vipi umepafa taarifa?" Akanijibu huku akiwa anaonekana amepaniki kiasi.
"Taarifa gani?"
"Waziri wa Nishati amepigwa risasi ubungo mida hii" akanieleza huku ana hema juu juu.
Nikatabasamu na kumuuliza "umesoma jamii forum?"
"No hapana nimepigiwa simu na rafiki yangu yuko gazeti la Mwananchi, ni habari ya uhakika" Baba Bite akanijibu huku yuko serious kabisa.
Nilijihisi kama nataka kuanguka. Nikatoa simu yangu tena na kurejea kwenye ile habari Jamii forum nikakuta imeongezewa 'link' na maneno mbele yake "source: Millard Ayo.”

Nikajishika mlangoni, nilitaka kuanguka mwili wote uliishiwa nguvu. Sikuamini nilichokiona na kukisikia. Sikujua hata ni mda gani Baba Bite aliniaga na kurudi ndani kwake.
Kama mtu aliyenyeshewa mvua nikarudi na kuketi kwenye Sofa. Kichwani dots zilianza kuungana. Kama kweli Waziri wa Nishati ameuwawa nilianza kuhisi mkakati wa The Board ulihusu nini na ulikiwa unaelekea wapi. Niliogopa hata kukiwaza nilichoanza kukielewa.
Upande mwingine, nilijuta kwanini sikuwahi kumwambia cheupe kuhusu The Board na jinsi ninavyoshirikiana nao. Toka siku ya kwanza nilivyomueleza kuwa kuna watu wanataka kunitafutia wafadhili ila siwaamini, sikuwahi kuongea nae tena suala hili. Sasa nilijisikia kujuta kwanini sijawahi kumwambia, kwasababu kadiri dots zilivyokuwa zina connect kichwani mwangu nikang'amua kuwa hata baba yake aliyeteuliwa kuwa mjumbe wa bodi ya TPDC miezi michache ikiyopita alikuwa hatarini.

Sikumsikia hata cheupe alipotoka bafuni, nilikuja kugundua tu amesimama mbele yangu.
"Ray, are you ok?" hatimae nilimsikia anauliza, nahisi alianza kuongea mda tu lakini sikumsikia.
"Waziri Japhet kipanju amepigwa risasi mda huu ubungo.!" Nikamjibu bila kumuangalia.
"Ooh my god, una uhakika."
"Asilimia mia" nikamjibu
"Aisee, inauma na naihurumia familia yake, but sielewi kwanini imekugusa kiasi hiki." cheupe aliniuliza kwa mshangao.

Sikujua nimjibu nini au nianzie wapi. Sikujua nianze vipi kumuelezea kosa kubwa nililolifanya, sikujua nianze vipi kumuelezea nilichokuwa nahisi kimepangwa na The Board na ambacho nilikuwa na hakika moyoni kilikuwa ninaelekea kutokea.

"Am so sorry hasnat" ndicho pekee nilichoweza kukitamka. Hasnat alikuwa amesimama mbele yangu na alikuwa na mshangao mkubwa usoni na alikuwa ameanza kutetemeka kwa woga.

"Sorry for what?" Aliniuliza huku bado akiwa kwenye mshangao mkubwa.

Kabla sijamjibu simu yake ya mkononi ikaita. Hasnat alikiuwa na mazoea ya kuongea na simu ikiwa kwenye "loud speaker" hivyo alivyo ichukua simu mezani na kuanza kuongea nayo nikawa nasikia kila kitu.

"Shikamoo mama! Vipi kwema? Mbona usiku usiku." Hasnat aliongea haraka haraka akiwa na woga mkubwa.
"Wamemchuka baba yako Hasnat!" Sauti ya upande wa iliongea ikiwa na mtetemo ikionekana dhahiri alikuwa analia.

"Nani aliyemchukua mama, na kwasababu gani?" Hasnat aliuliza sauti ikitetemeka kuashiria alikuwa anajikaza asilie kwa sauti.

"Polisi wamemchukua baba yako kama nusu saa iliyopita, wanasema anahusika na tukio la kupigwa risasi Waziri Mpanju usiku huu" mama yake hasnat aliongea na kushindwa kuzuia kilio chake.

Hasnat akishindwa kuendelea kuongea na simu, alipigwa na butwaa akabaki ameganda amenikodolea macho kana kwamba ni mara yake ya kwanza kuniona. Kuna kitu alikuwa anataka kusema lakini anashindwa ila ni machozi tu yakaendelea kutoka. Nikabaki nimesimama tu mbele yake sijui nifanye nini au niseme nini! Sikumbuki mara yangu ya mwisho kulia ilikuwa lini, lakini hii inaweza kuwa mara ya kwanza kwa miaka mingi. Nikajikuta machozi yananitoka bila kuelewa.

"Ray, whats going on here?" Hasnat aliongea huku anatetemeka kwa woga na hasira.

Nikajikuta nainua uso na kuangalia juu na kufumba macho kwa uchungu. Kisha nikafumbua macho na kumuangalia Hasnat moja kwa moja.

"Hasnat ma love, nataka nikwambie kitu but you are not going to like it."





Ray alielewa nini kuhusu mkakati wa The Board baada ya kuconnect dots?? Baba yake Hasnat anahusikaje na kinachoendelea?? Ray atajikwamua vipi kutoka katika mikono ya The Board??



Itaendelea Jumapili. Episode 3





The Bold.
 
NEW EPISODE (EPISODE 2) POST # 282


Divine... glory to yhwh Nifah BansenBurner Alisen Papushikashi Magazine Fire miss chagga succinate coA hydrogenase SANCTUS ANACLETUS mngony Excel Mussolin5 Jimena Inferiority Complex gwijimimi wambura marwa Hoshea Shareef Conscious wambeke The Boss deejay Nasmile gkileo Juma chief Mangi flani hivi Ngongo makaveli10 KENZY kadada wa pili Root aretasludovick jonnie_vincy Clkey KAFA.cOm mbewe makedonia Afande Nyati peterchoka Leonard Robert Nchi Kavu STUNTER Chrizo jully van persie Khalidoun Tetramelyz punje haradari Mazigazi Alybaba babu na mjukuu platozoom jimmyfoxxgongo Nicodemas Tambo Mwikozi Ls man Heaven Sent sifongo Infantry Soldier haa mym 20acres MTS MarkHilary compos Tembo2 Erick the future nancy1983 Bulah binsaad Fazzaly The Wolf Firegironsa everhurt Melvine Mgibeon kijana wa leo samsun Coolant Jagood pacesetter apologize payton George Betram kisengeli Kiranga Jiwe Linaloishi Madame B jay john Guasa Amboni Dinazarde Juma chief Analyse Diva Beyonce snowhite Mmanu Expected Value onechromosome Missy rose Innocenthezron Immortal_MH Ficus sunola Robot la Matope mamaafacebook II JEKI likikima Compact scorpio me G'taxi gambada ynwa adna yuzo ntamaholo Otorong'ong'o naan ngik-kundie kandukamo1 AFRICA101 mwalidebe Kobe Blaki Womani kalendi savius The Great Emanuel r2ga Ntaluke.N. Transcend Msemachochote Mchumiajuone mwampepec MTOTO WA KUKU Fukara proto cute kawombe zinginary MLALUKO JR Vupu barafu BlackPanther Ntuzu Matola impongo ntamaholo Mkoroshokigoli Deadbody King Easy mahoza Msolo kkenzki deborah1 Mazigazi KIDUDU buffalo44 winlicious RIZIKI ALLYS MUHUNZI Moses2015 nacktary Liuumi dochivele Renzo barbers hmjamii mbere TATIANA famicho LUCKDUBE mwanadome StraTon MemPhis GhaZar Graph Theory Honey Faith Shunie Slave ddcmanesto zinginary pacesetter Nkanaga haa mym KOMUGISHA mikatabafeki johnsonmgaya lee empire wigo MJINI CHAI Asprin mtzmweusi Blaki Womani Erasto kalinga Chrizo kichakaa man kulubule FORTALEZA poleni Mshuza2 shibumi ZE DONE gkileo umande Edger Sr sir joshua sammoo Roram Password Bavaria hambiliki mwanangu Clkey Asili100 Evarist Massawe nice1 Jumong S Rogie babake nasreen uberito baest dustless Kilemachocho Tumosa mtembea kwa miguu Debbs Joe scorpnose musacha shibumi seeker of knowledge Simuchi Veni Vidi Vici T-King gkileo mij TUJITEGEMEE abuu garcia Hon Nkundwe Festo Mwangungulu marion09
 
Mkuu The bold kuna uwezekano wa kuzipandisha iz Episode kwenye ile post yako ya kwanza ili kuwe na mtiririko mzuri
ama tuombe hawa @Moderators watu saidie kwa hili.

[/b]BTW Asante na hongera kwa kutupa hivi vitu adimuu[/b]
yes nadhani ni vizuri mods wakizipandisha pale page ya kwanza.. ila zisikae kwenye post moja.. ingekuwa vizuri post # 1 ikae episode 2, post # 2 ikae episode 2 na kuendelea..

mods tusaidieni kwenye hilo.. JamiiForums Maxence Melo Mod 1 Mod 2 Mod 3 Mod 4 Mod 5
 
Aiseee!!! Usiku wangu utakuwa mzuuriii leo hongera kwako mwana board mwenzangu, alafu huyu max tulimwambia atupe details za msaga sumu maana anakihere here kama nini usiku wote huo anawekaje taarifa kama hyo, ,,,
GENTYMINE hapendagi shida aisee bingwa wa kushitaki kwa mods hata bila ya ku verify,,
Alafu mkuu unawasema wenzio wamechukuana wanamega kisela wakati na ww ndo hvo hvo tu, asante jf kwa kufanya ndugu RAY asifanye dhambi ya kuzini ....... tchao tukutane jpili,,,,
 
Mkuu The bold naomba nitoe utabiri fake!

Wakuu its just imagination! Dont take me serious...

1.Ray (Ally Hassan) ni The Bold
2. Hasnat (cheupee) ni Nifah
3.Mb. Zepahia zuberi ni Zitto kabwe
4. Mmiliki wa vyombo vya Bw. Rostam Aziz
5.Max ni maxence Melo Founder wa Jamiiforum
6. Waziri wa madini na nishati alieuwawa ni Waziri alietumbuliwa ( kaachishwa uwaziri ) hajauwawa kikwelikweli..




Weka episode ingine! Afu usisahau kunitag tena
 
The bold nice job
Bernard Shayo=Regnald M.e.ng"i?
Zuberi Zephania=Kigoma mjini moja?
Ila asante kwa stori
Ameishasema ni majina yakubuni tu sasa wewe nae unaleta mambo gani?Kila mtu muache abaki na lake kichwani ndio maana hakuna aliyesema kuhusu wahusika toka mwanzo wa story mpaka sasa
The bold nice job
Bernard Shayo=Regnald M.e.ng"i?
Zuberi Zephania=Kigoma mjini moja?
Ila asante kwa stori
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom