Vipepeo Weusi: Mkakati Namba 0034 (Simulizi)

Vipepeo Weusi: Mkakati Namba 0034 (Simulizi)

dah aseee hii story ninavosoma kama nacheki muvi vile.
big up bro
 
EPISODE 4


Issack alikuwa anaishi Upanga mtaa wa Mindu kwa wazazi wake. Tumefahamiana kwa miaka mingi sana tangu tunasoma sekondari Kibaha Boys. Tangu kipindi hicho alikuwa ni mtundu mtundu sana wa kompyuta. Nakumbuka siku za weekend tulikuwa tunatoka shuleni maeneo ya Tumbi mpaka Maili Moja kwenye hoteli ya Njuweni kulikuwa na Internet Café.
Wenyewe wamiliki wa Internet Café walikuwa na utaratibu unalipia hela ambayo ilikuwa shilingi mia tano kwa nusu saa kisha unakaa kwenye kompyuta iliyowekewa program ya 'time watcher' ambapo inasetiwa kujizima mara tu nusu saa ikifika.
Nakumbuka tulikuwa tunalipia nusu saa na tukisha wekewa muda na muhudumu kuondoka Issack anabonyeza bonyeza button za keypad na baada ya mda pale juu alama ya 'time watcher' inaondoka na tunatumia hata masaa mawili kisha anabonyeza bonyeza tena ile time watcher inarudi tena na kompyuta kujizima.! Uzuri kulikuwa na kompyuta nyingi hivyo hatukuwahi kushitukiwa na muhudumu.

Nilikuwa nimeshafika Nyumbani kwao na tulikuwa tumeketi kwenye meza ya chakula namsikiliza maelezo yake.
"Ujue muda ule ulikuwa upo na mtoto mzuri nikashindwa kukuliza nini tatizo mpaka unataka kuwachunguza wafadhili wako." Issack akauliza huku usoni akiwa na tabasamu la 'kikomedi' kama desturi yake.

"Its a long story Issack, ila kwa ufupi labda niseme siwaani! Nahisi kuna vitu wananificha, so tell me umeona nini?" Nikamueleza kwa mkato tu nikijihami kuepuka kumpa taarifa ambazo hazimuhusu.

"OK! Unajua kwenye system za bank kuhack na kufanya transfers ndio ishu ngumu, so nilitamani niwaibie ila itachukua muda kidogo hahahah." Issack akaanza utani.

"Come on, kuwa serious basi! Umeona nini?" Nikamuuliza nikiwa serious nikitaka aache utani tuongee mambo ya maana.

"Ndio nilikuwa nakuja huko, as i said kuhack na kufanya transfers ndio ishu ngumu so nilichokifanya ni kuhack na kuchukua statemnt yao kuonyesha transactions zilizofanyika, nikaangalia transactios walizozifanya kutuma hela sijaona chochote cha kushtua then nikaanza kuangalia transactios za kupokea fedha kutoka kwa donors hapo ndipo nikakuta maluwe luwe" akaongea huku ananipa karatasi.

Nikapokea karatasi na kuitazama tu nikiwa bado sijaelewa point yake. Karatasi ilikuwa na orodha ndefu sana ikionyesha miamala.
Issack nandhani akaona bado sijaelewa au sikuona alichotaka nikione kwenye karatasi hiyo.
"Cheki hapa!" Akanionyesha sehemu kwenye karatasi. Moyo ukanipasuka! Katika kati ya miamala kulikuwa na muamala wa kutumiwa fedha kutoka kwa NDESHEMA SAFARIS (UK). Moyo ukalipuka.
"Cheki na hizi" akanikabidhi karatasi nyingine kama tano hivi.. Zote zilikuwa ni bank statements zikionyesha miamala. Kwenye kila karatasi kulikuwa na miamala kadhaa kutoka kwa NDESHEMA SAFARIS (UK).

Kuna kipindi inatokea mtu unaona jambo mbele yako lakini ubongo wako unakataa kuamini! Ndio nilikuwa katika hali hiyo. Mikononi mwangu niliona jambo dhahiri kabisa lakini nilishindwa kuamini.

Ndeshema Safaris ikikuwa ni kampuni inayomilikiwa na Eric Kaburu. Licha ya kampuni yake kuwa kubwa ilijizolea umaarufu zaidi miaka miwili iliyopita baada ya yeye mwenyews Eric Kaburu kukabiliwa na kesi ya mauaji ya mpenzi wake. Mwishoni mwa kesi alikutwa na hatia ya kuua bila kukusudia na akahukumiwa miaka saba gerezani.

Kampuni yake ilikuwa na makao makuu nchini Tanzania, na ilijihusisha na kutoa huduma za masuala ya utalii lakini pia ilikuwa na matawi ya uwakala nchini marekani na nchini uingereza! Na tawi hili la Uingereza ndilo linaloonekana hapa kuwa moja ya donors wa Alice Cartz Foundation.

Nikapepesa tena macho kwenye zile karatasi. Kulikuwa na majina ya watu binafsi, makampuni ambayo yakikuwa yanachangia fedha kwenda Alice Cartz Foundation, lakini katika orodha yote hii Ndeshema Safaris ndio walionekana kuwa wachangiaji wakuu na wakitoa kiwango kikubwa zaidi cha fedha.
Nikajiuliza kichwani kama hii ilikuwa ni coincidence au ina maana gani. Sikuwahi kusikia au kuona kampuni ya kitanzania ikisaidia shirika la nje kwa kiwango kikubwa namna hii alafu shirika hilo hilo lije tena Tanzania kusaidia jamii. Nikahisi kuna jambo hapa.

"Hivi unakumbuka kaburu yuko gereza gani?" Nikamuuliza Issack ambaye muda wote huu alikuwa amenikodolea macho ananishangaa nilivyokaa kimya najaribu kuelew kinachoendelea


"Well, baada ya kukuta hayo mauza uza kwenye statement nikaanza kutafuta taarifa za Eric Kaburu, yuko gereza kuu Morogoro" Akanijubu Issack na kuongeza "Ray, unaweza kunieleza kinachoendelea hapa? Maana sielewi elewi hivi nahisi" akauliza akiwa ameacha kabisa utani kama kawaida yake na akikuwa serious kabisa usoni.

"Issack i promise nitakueleza kinachoendelea but its a long story naomba tuongee siku nyingine kwasasa naomba niende nikalifanyie kazi hili."

Nikamshukuru na kumuaga haraka haraka na kuondoka.
Tayari ilikuwa imeshafika saa kumi na mbili jioni. Nikampigia simu Cheupe kumuuliza wamefikia wapi na majadiliano na familia, na akanieleza kuwa walienda wizara ya mambo ya ndani na wakaelezwa kuwa hawawezi kupewa taarifa zozote kwa sasa kuhusu Mhandisi Jaffar kumbue lakini waliombwa kuwa watulivu na warudi baada ya siku tatu.
Baada ya yeye kunipa mrejesho huo na mimi nikamueleza kuhusu kikao changu na Issack na kitu ambacho amefanikiwa kukipata.
Pia nikamuekeza kuwa sitaonana nae kwani naelekea Morogoro usiku huu na nia yangu ni kwenda kuonana na Eric Kaburu gerezani. Nikamueleza kuwa nilikuwa na imani na hakika kabisa kuwa lazima kunaconnection kati ya Kaburu na The Board maana haiwezi kuwa conicedence kwa kampuni yake kusaidia shirika nchini Australia alafu shirika hili lije linisaidie mimi na taasisi yangu na ukizingatia kuwa wafadhili hao nimetafutiwa na The Board.

Tukaagana, nikakanyaga mafuta kuelekea Morogoro.

Niliingia Morogoro saa nne kasoro usiku na nilipofika nyumbani Mazimbu na kupaki gari ndani nikashangaa mabadiliko niliyoyaona. Kwanza nilifunguliwa geti na mla bata Tony tofauti na kawaida ambapo mara nyingi ni Baba Bite huwa ananifungulia geti. Pia ndani kuliwa kumepooza mno.

"Vipi kiongozi wazima hapa?" Nikamsalimia Tony baada ya kushuka kwenye gari.
"Salama kabisa! Rafiki yako Baba Bite amehama leo ghafla tu hahahah" akaongea Tony huku anacheka.
"Whaaat? Baba bite si nimemuacha hapa leo asubuhi na hakunambia chochote kuhusu kuhama?" Nikauliza kwa mshangao mkubwa.
"Hata mwenye nyumba ameshangaa maana ghafla tu na kodi yake bado miezi minne hahahahah! Watu na mipango yao bhana huwezi jua" Tony akajibu huku anaingia ndani kwake.

Nikashangaa kweki kweli! Inawezekana vipi mtu ahame haraka haraka namna hii? Huyu baba bite ana nini anakificha? Nikazidi kuongeza mashaka juu yake.
Nikafungua mlango wa ndani kwangu na kuingia kulala tayari kwa kwenda kumuona Kaburu kesho gerezani.


***************************


Tayari nilikuwa nimefika gereza kuu la Morogoro. Gereza hili liko karibu kabisa na katikati ya mji njia ya kuelekea Kilakala. Nilikuwa sijaingia bado ndani, nilikuwa nje nawashawishi maaskari niingie na walikuwa 'wananikazia' kwa kuwa haikuwa weekend.

Nilitumia karibia nusu saa kuwashawishi maaskari magereza wamuite Kaburu na Kuniruhusu kuongea naye lakini wakanikatalia.
Baadae akaja askari mwingine ambaye alionekana kuwa na cheo kuliko wale niliokuwa naongea nao na akatuuliza nini tatizo.
"Mkuu nimekuja kumuona ndugu yangu hapa, natokea mbali sana, naishi dar na leo hii baadae natakiwa nisafiri kwenda nyumbani kigoma na nina maongezi muhimu sana na ndugu yangu! Nashangaa hawataki kuniruhusu kitu kidogo kama hichi wanataka nije weekend!" Nikaongea uongo huku najiamini kweli kweli.

Yule askari mwenye cheo cheo akawageukia kama anawashangaa hivi, "yani ishu ndogo hivyo ndio mnabishana mda wote huu, eboo! Hebu saidianeni bhana, mruhusuni kuonana na ndugu yake na wewe dogo hebu tuachie ya vocha." akaongea kwa makeke na kujiamni.

Nikazama mfukoni, nikachukua wallet na kutoa noti tano za elfu kumi na kumkabidhi yule askari mwenye cheo.
Akazikunja noti tatu na kuziweka mfukoni kisha akawapa noti moja moja wale maaskari mwingine.

Baada ya hapo, nikaruhusiwa kuingia ndani na kuongozwa mpaka kwenye kichumba cha wageni kuongea na wafungwa. Kilikuwa ni kichumba kidogo ambacho kilitenganishwa pande mbili katikati likitengenezwa kama dirisha kubwa la nyavu kutenganisha chumba hicho pande mbili ambapo mnakuwa ndani ya chumba kimoja na mnaweza kuonana lakini hamuwezi kugusana.

Nikasubiri kama dakika kumi hivi ndipo upande wa pili wa chumba akaingia mtu mzima wa makamo kwa makadirio ya kama miaka 54 hadi 56! Alikuwa na mwili wenye afya nzuri tu na kichwani alikuwa na mvi kwa mbali.
Alikuwa amevalia mavazi ya rangi ya chungwa, sare ya kifungwa!

Hatimaye Eric Kaburu alikuwa mbele yangu.

Nikamsubiri akae na awe comfortable kisha nikafungua maongezi.

"Shikamoo mkuu" nikaamkia kwa heshima.
"Sidhani kama nakufahamu!" Kaburu akajibu bila kuitikia salami yangu akiwa amenikazia macho.
"Yeah! Aaahh jina langu naitwa Ally l! Aaahh Ally Hassan Nina shida kidogo nataka kuzungumza nawe." Nikaongea tena kwa heshima.

Kaburu hakujibu chochote kile. Akiniangalia tu. Nikaelewa kuwa alikuwa anasubiria niongee shida yangu.

"Kampuni yako tawi la London linafadhiki Shirika ambalo linatoa msaada katika kampuni yangu na hivi karibuni nadhani ime….."

"Sikiliza kijana, ukitaka msaada kwa mtu kwanza unatakiwa umuheshimu! Na dalili ya kwanza ya kumuheshimu mtu ni kuwa mwaminifu! Umeanza maongezi yako kwa kusema uongo, jina lako sio Ally Hassan! Nafahamu unaitwa Rweyemamu Charles Kajuna!! Na kabla hujaniuliza chochote naomba nikupe majibu kabisa… Sina explanation ya swali lako lolote na sitaki kukuona tena ukija hapa kuniona, kwa usalama wangu na wako."
Kaburu aliongea akiwa amenikazia macho na alikuwa serious kweli kweli. Hakusubiri niseme chochote, akainuka na kuondoka.

Nilipigwa na bumbuwazi na kubaki nimeganda kama nimemwagiwa maji. Mwili wote uliganda kama barafu.
Sikujua nilikaa namna ile kwa muda gani, nilikuja kuzinduliwa na askari magereza akiniita nitoke.
"Oya vipi umelala au niaje? Ndugu yako ametoka muda tu nashangaa wewe bado uko ndani."

Nikazinduka kutoka kwenye bumbuwazi na kutoka nje. Sikukumbuka kuaga wala kuwashukuru wale askari walioniruhusu kuingia. Nikatoka na kuingia kwenye gari moja kwa moja na kurudi nyumbani Mazimbu. Nilipofika nyumbani nikamkuta Tony nje, sikumbuki kama alinisakimia au vipi lakini nakumbuka kuwa sikuitikia kama alinisalimia.

Nikafunga mlango. Nikazima simu.
Sikutaka kuongea na yeyote, au yafaa kusema sikuweza hata kuongea chochote. Mshangao na mshtuko niloupata nilishindwa hata kuwaza kichwani. Eric Kaburu ananifahamu!! Inawezekana vipi??
Nikajihisi kama niko kwenye dimbwi lenye tope na kila ninapojaribu kukuruka kujiokoa ndivyo ninavyozidi kuzama. Kila hatua na kila ninachokifanya kinazidi kuniiingiza kwenye sintofahamu kubwa zaidi.
Nikafumba macho. Sikuweza kuwaza. Usingizi ukanipitia.

Nilikuja kushtuka mida ya jioni. Kuna mtu alikuwa ana gonga mlango nadhani alikuwa Tony. Sikuweza kumuitikia. Kitu pekee kilichokuwa kinajirudia tena na tena kichwani mwangu ilikuwa ni kauli ya Eric Kaburu gerezani. "Nakufahamu unaitwa Rweyemamu Charles Kajuna." "Naomba usirudi tena hapa kuonana nami kwa usalama wako na wangu"
"What the fu*k is going on??" Niliwaza. Nikatamani kulia lakini machozi hayakutoka.
Nikabaki na bumbuwazi tu. Nikafumba macho. Usingizi ukanipitia.


*************************


Nilipokuja kuamka ilikuwa ni saa kumi na mbili asubuhi. Njaa ilikuwa inaniuma kweli kweli. Nilikuwa sijala toka jana asubuhi.
Huwa sipendi kupika. Hata chai tu sipendi kupika. Nikawaza labda niwashe gari mpaka mjini maeneo ya Kaumba nikanunue chips maana maeneo hayo haijalishi ni saa ngapi watu wako macho na chips kibao zinapikwa.


Nikiwa katika kuwaza kuhusu kula nikakumbuka kuwa simu nimeizima toka jana mchana na nilikuwa nimeshasahau kama simu iko off.

Nikaichukua haraka haraka na kuiwasha. Baada ya kuiwasha tu meseji kama thelathini hivi zikaingia, nyingi zilikuwa za Cheupe. Jicho likaona moja ya meseji hizo.

"Baby am worried! Are you ok?"

"Sh*t" nikabofya simu kumpigia haraka. Nikagundua kiasi gani atakuwa na wasiwasi kwa kunikosa hewani siku nzima.

"Hey love" nikamsalimia baada ya kupokea simu.
"What the hell? Siku nzima sikupati, are you ok?"
"Niko poa kabisa, nitakupa mrejesho tukionana! Vipi huko nini kinaendelea?"
"Jitahidi ufike haraka kabla ya saa nne, tumeitwa wizara ya mambo ya ndani" akaongea cheupe haraka haraka.
"Duh! Am on my way"

Nikakata simu na kujiandaa haraka haraka. Nikawasha gari na kuanza safari ya kurejea tena dar.

Nilipofika maeneo ya Nane Nane kwenye kituo cha mafuta cha Camel Oil nikaingia ili kujaza mafuta. Wakati najaza mafuta nikaona gari ya kijivu aina ya Land Cruiser ikapaki pembeni yangu nayo ikawa inajaza mafuta.
Baada ya kumaliza nikaendekea na safari na masaa mawili na nusu baadae nikwa nimefika ubungo. Niliposimama kusubiri taa ziruhusu nilipotizama katika kioo cha dereva nikaliona tena lile gari land cruiser niliyoiona Nane Nane Morogoro.

Nikahisi gari hiyo inanifuatilia. Kwahiyo taa ziliporuhusu nikanyoosha moja kwa moja Morogoro Road kuelekea mjini.
Nilipofika maeneo ya Magomeni Kagera nikaangalia tena nyuma, ile Land Cruiser ilikuwepo.
Nikakata kushoto bara bara ndogo inayoenda kutokea Magomeni Popobawa. Nikaongeza mwendo na kuangalia nyuma ile Land Cruiser bado ipo.
Nilipotokea Popobawa, nikakata kulia kufuata barabara inayotoka sinza kwenda kukutana na barabara ya Ali Hassan Mwinyi. Nikatazama nyuma, ile land cruiser ipo na sasa zilikuwa mbili. Ile ya kijivu na nyingine nyeusi.

Nikaongeza mwendo lakini ile Land Cruiser ya kijivu ikanizidi kasi na kuja kuniziba mbele yangu ikipunguza mwendo taratibu na kunilazimu na mimi kupunguza mwendo. Mwisho ikasimama na kuniziba njia mbele na mimi nikasimana.
Haya yote yanafanyika "mchana kweupe" au tuseme asubuhi kweupe maana ilikuwa ni majira ya saa nne asubuhi.

Baad ya magari yote kusimama, wakashuka watu wawili kutoka ile Land Cuiser ya kijivu, mmoja amevaa suti nyeusi na mwingine amevalia suruali na shati amechomekea.
Wakaja mpaka kwenye gari yangu na kunionyesha ishara nishuke. Nikajiuliza sana nifanyeje. Kama ilivyo desturi yetu waswahili tayari watu walianza kushangaa na kujikusanya. Moyoni nikapata ujasiri. Nikafungua mlango nikashuka.

Yule mmoja aliyevaa suti akanisogelea karibu na kunionyesha kitambulisho.

"Afisa Usalama wa Taifa, naomba ufuatane nasi" akaongea haraka, na hakusubiri jibu langu akanishika mkono kwenye kiwiko na kunipeleka kwenye ile land cruiser ya kijivu, tukapanda ndani akafunga milango.

Yule Afisa mwingine akaingia kwenye gari yangu. Kisha nagari yote matatu yakageuza kwa kasi kuifuata Barbara inayoelekea sinza.

Nikajisemea kimoyo moyo, "nimekwisha!!"



Itaendelea..
 
Boss wetu Bold aisee tufanyie mambo ntasinzia mwenzako maana natoa macho hapa kama mjusi alobanwa mlango au mtu alofumaniwa na nisipoisoma ss hv itanibidi hadi kesho jioni tena daaaa
Jitahidi basi fanya mambo mkuu
 
Mkuuuuuuu asaanteeeeeeeeeee
 
Impossible my sista.
Jamaa akitaja viunga vya Kilosa ananikumbusha madafu wakat nasoma huko,na ndo nilikozaliwa,akitaja Kilombero ndo kwa mama naendaga kula KAMBALE NA KITOGA.
Akitaja Dark City nakumbuka maisha yangu wakat naish Mazimbu Campus.
Hahahaha hapo Dark City pameshindika aisee. Mkubwa ndevu mdogo ndevu. Yaani siku ya kwanza tu kuna dogo wa kama 4 years hivi kanatusalimia 'Oya washkaji mambo vipi?'. Hapo ndio nikajua siko eneo salama.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom