Vipepeo Weusi: Mkakati Namba 0034 (Simulizi)

Vipepeo Weusi: Mkakati Namba 0034 (Simulizi)

'Musiba' wa Njama, Kikosi cha Kisasi (KK),Tutarudi na Roho Zetu na riwaya nyingine kazaliwa upya!!!
=====
Niliuchunia uzi wako fulani wa US na 'convert security branches '. Huu umeninasa kama ndege kwenye Tundu Bovu yaani nimeishakubali, sichomoki!
 
Mkuu the bold mm uku ni j2 tayari tena usiku sasa shida iko apa chalii kagoma kulala anasubiria episode 3
Niweke kwenye tag list meku
 
Sijui nilikuwa wapi..ngoja nitulie niusome kwa uzuri. Kwa kupitia comments chache tu inaonekana ni hatari kwako.
 
Kumbe imeendelea duuh..sikujua aisee kuwa ep 2 imetoka

Ngoja kesho leo nakunywa vyesto bday yangu
 
EPISODE 3 TEASER (FULL EPISODE KESHO J'PILI)


Kwa takribani dakika 20 ilinibidi nipaki gari pembeni ya barabara maeneo ya Interchik nikijiuliza nini cha kufanya au nielekee wapi. Niende nyumbani kwa kina Hasnat kumfikishia cheupe wangu habari hii ambayo hakuna mwanaume anaweza kumwambia mwanamke anayempenda au nirudi tena kuongea na wale maafisa usalama?

Sikutamani hata kwa sekunde moja kumtamkia Cheupe kile nilichokuwa nataka kukifanya, lakini je nilikuwa na chaguo lingine?
Au labda nirudi nikawaeleze wale maafisa wa Idara ya Usalama taarifa ambayo nilikuwa nayo moyoni lakini niliwaficha na sikuwaeleza? Lakini hili nalo lilikuwa gumu kulifanya, kwa maelezo waliyonipa leo hii nikajikuta nawaza kwanini Baba Bite alinigongea usiku ule na kunipa taarifa kuhusu kifo cha waziri? Yes ilikuwa ni taarifa ya kushtua lakini kwanini anigongee usiku wa manane kuniambia hilo, sina undugu wowote na Waziri kwanini anigongee kunipa taarfa usiku usiku? Je anafahamu hiki nilichoelezwa leo na Maafisa Wa Idara ya Usalama wa Taifa? Kichwa kiliniuma nikijaribu kuwaza hatua sahihi ya kupiga na kufanya nikitoka hapa.

Kichwani ilijirudia tena na tena kauli ya Afisa usalama yule ambaye tulikuwa tunamsikiliza kwenye simu mimi pamoja na maafisa walikuwepo kwenye nyumba yao pale Mbezi Beach, "tunahitaji kujua the exact location ndani ya wiki tatu". Damn it.. Kichwa kiliuma zaidi kila mara ambapo kauli hii ilijirudia kichwani mwangu, na akili yangu ilijitahidi nisiwaze option pekee iliyopo mbele yangu, lakini haijalishi ni kwa kiasi gani nilijilazimisha kutokuwaza option hiyo, nilijikuta najiambia mwenyewe ndani ya moyo wangu kana kwamba kuna mtu ananinongoneza sikioni, "natakiwa niende jela."

Kila nilipowaza hili nilitamani hata nipasuke vipande vipande maisha yaishe. Nawezaje kutekeleza hili, na nisipofanya hivi je ni option gani nyingine niliyo nayo?

Nilitamani nifanye kama wafanyavyo kwenye filamu na tamthilia wakionyesha wahusika wakitoroka magerezani kwa ustadi. Lakini hii haikuwa filamu, hii haikuwa tamthilia, haya yalikuwa maisha halisi na ubaya zaidi yanibidi kuingia jela sio kutoroka jela!

"Fu*k it" nilikasirika kweli kweli, nawezaje kulifanya hili. Kwa mara ya kwanza kwenye maisha nikagundua kuwa kuingia jela 'kimagendo' ni ngumu zaidi ya kutoroka jela. Na dhahiri nilijua hili suala haliwezekani! Lakini again, ni option gani nyingine niliyo nayo?? Hakuna.

Nikainamisha kichwa kwenye usukani, nikamuwaza cheupe wangu, nikawaza vijana wanaosaidiwa na Sote Hub, nikawaza familia yangu wote hawa wananihitaji, nawezaje kufanya jambo la kiwendawazimu hivi! Mbaya zaidi watu wa Usalama wa Taifa waliniweka wazi kuwa hawatajihusisha katika hatua hii, watabaki watazamaji tu kwa ninachokifanya ila wanachohitaji, "tunahitaji kujua the exact location ndani ya wiki tatu" kauli ya yule afisa kwenye simu ikajirudia na moyoni nikajikuta nikijisemea tena mwenyewe kama nanong'onezwa sikioni "natakiwa niende jela."

Nikawasha gari na kuanza kuelekea tegeta nyumbani kwa kina Hasnat.



--------------------------



Full episode kesho j'pili.!
87719d25fcc0db63a3ad21ea6fe9cf8a.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom