Vipepeo Weusi: Mkakati Namba 0034 (Simulizi)

Vipepeo Weusi: Mkakati Namba 0034 (Simulizi)

The bold naomba niwe mwanafunzi wako... huwaga naandika andika vijistory lakini sijafika level yako wish one day nivivae viatu vyako
 
Dah mkuu The Bold episodes za siku hizi fupiiiiiii....

Ile utamu unazidi kukolea ndio unakutana na maandishi "ITAENDELEA JUMATANO.."
 
VIPEPEO WEUSI: MKAKATI NAMBA 0034





Ilipoishia Episode 22 (highlights)

Ray amefanikiwa kumtorosha Kaburu kutoka gerezani na kaburu amemuambia siri kubwa kuhusu zilipo files za The Board zilipo.
Ray anapewa maelezo na mzee anayitwa Chief kuhusu jengo la Golden Jubilee Tower, na strong room ya makao makuu ya benki ya CRBB ambako ndiko file hizo zilipo.
Baadae Ray anang'amua kuwa hawezi kufanikiwa kuingia ndani ya vault, hivyo anakodi ofisi ili afanikishe kitu ambacho anakiita kuwa ni "long con"!!

Tuendelee..


EPISODE 26



APRIL, 1974: DAR ES SALAAM

Siku mbili zilizopita kijana wa Kitanzania, Charles Bernard Kajuna mwenye miaka 36 akiwa na mkewe Sophia Ndege waliwasili jijini Dar es Salaam wakitokea jijini Nairobi ambako Bernard alikuwa ni Mkurugenzi wa Kitego cha Ukaguzi wa ndani kwenye Bank ya Detta & Boyd Bank.

Ujio wake kutoka Nairobi kurudi Dar es Salaam ulitokana na wito wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wiki moja iliyopita.

Kutokana na staili ya uongozi wa Rais, ilikuwa ni ngumu kujua ni kwanini amekuita.
Kulikuwa na utani kipindi hicho katika maongezi ya Watumishi wa uuma wakipenda kusema "ukiitwa Dar, utarudi kichwa chini au utarudi unaruka ruka".! Wakimaanisha kwamba ukiitwa Dar kwa Rais, eidha unaenda kupandishwa cheo au kufukuzwa kazi.

Lakini Charles hakuwa mtumishi wa Umma, alikuwa ameajiriwa na kampuni binafsi, tena siyo kampuni ya kitanzania.. Alikuwa anafanya kazi kwenye benki binafsi, Detta & Boyd, Benki kutoka Africa ya Kusini iliyokuwa na matawi kadhaa nchini Kenya kwenye miaka hiyo ya sabini.

Hapa Dar walikuwa wamefikia kwenye Hoteli ya Kilimanjaro iliyopo katikati ya jiji.
Leo ndio siku ambayo alikuwa anatakiwa kwenda Ikulu kuonana na Rais.

"Sijui wanataka nini hawa watu" Charles akaongea huku akiwa mbele ya kioo anarekebisha tai vizuri.

"Labda Rais anataka kukupa Uwaziri!!" Mkewe Sophia akamjibu kwa utani.

"Hahahah natamani iwe hivyo" Charles naye akajibu kwa utani.

"Hivi mawaziri nao wanakaa Ikulu pale pale" Akauliza Sophia.

"Hahaha wewe mke wa Waziri mtarajiwa utanitia aibu sasa.. Ikulu anakaa Rais" Charles akajibu huku anatembea kumfuata mkewe aliyekuwa amekaa juu ya kitanda.

"Kwahiyo sisi tutakaa wapi??"

"Eeee taratibu mama, usianze kupiga hesabu kana kwamba naenda kupewa uwaziri kweli.. Kwanza mawaziri wote ni lazima uwe mbunge" Chales akajibu huku anamkumbatia mkewe na kupapasa tumbo lake la ujauzito.
"Mpaka mchana nadhani nitakuwa nimerudi"

"Jitahidi urudi haraka nimemwambia mpishi apike mboga za majani za kutosha, sitaki ule vyakula vyako vile vya kizungu huko unakoenda" Sophia akaongea huku anainuka akiwa amejishika kiuno 'kusapoti' tumbo lake kubwa.

"Mboga za majani za nini mkewangu! Umesahau ninavyokwambia kila siku?" Charles akaanza utani.

"Hahahaha sitaki huo msemo wako kuusikia tena"

"Ngoja niseme tu ilo usisahau tena!"

"Hahahahahah sitakiiii"

"Ukiwa na hela huitaji mboga za majani, vitamini zinakuja zenyewe automatic.!"

"Hahahahahahahah..!" Sophia akaangua kicheko.

Japokuwa miaka hii ilikuwa na mfumo dume uliokithiri, lakini kulikuwa na wanandoa wachache ambao mume na mke waliishi kirafiki kabisa, na moja ya wanandoa hao alikuwa ni Charles na mkewe Sophia.

Labda hii ilitokana na Charles kupata fursa ya kukaa nchini Uingereza kwa masoma kwa miaka kadhaa, labda ndio sababu alikuwa na "uzungu", kwani licha ya tofauti kubwa ya umri, Charles akiwa na miaka 36 na Sophia akiwa na miaka 22 tu, lakini walipendana na kuishi kirafiki kabisa.

Charles akamuaga mkewe na kusuka chini ya hoteli.
Kuna gari ilikuwa inamsubiri na akapanda, safari ya kwenda ikulu ikaanza.

Kama dakika kumi baadae walikuwa tayari wako nje ya geti la Ikulu.
Baada ya kuandikisha jina na walinzi kuangalia kumbukumbi zao kama Rais anategemea mgeni huyo leo hii, hatimaye wakaruhusiwa kuingia.

Baada ya kushuka tu kwenye gari akaongozwa na wasaidizi wa Rais mpaka kwenye ofisi.
Katika miaka hiyo kabla ya kubadilishwa hapo baadae, ilikuwa ukiingia Ikulu ofisi ziko upande wa kulia mwa jengo kuu.
Kulikuwa na vyumba kadhaa vya maofisi ya wasaidizi wake, kisha kuna mlango wa kuingia ofisini kwa rais. Ukiingia tu unakutana na 'sebule'. Subule hii ilikuwa ni mapokezi ambapo kulikuwa karibia na viti vinane ambavyo vimepangwa upande mmoja viti vinne na mwingine viti vinne na katikati kuna meza, kisha baada ya kutoka mapokezi unakutana na korido yenye urefu kama wa Mita nne au tano kisha unakutana na mlango mwingine ambao nao ukifungua unakutana na sebule nyingine yenye 'masofa' ya fahari kidogo na meza kubwa.

Hii haikuwa mapokezi. Hii ilikuwa ni sebule ya rais kupumzika au kungea na wageni endapo kama wakiwa ni kikundi cha watu au ugeni mzito.
Ukikatana kona kushoto kutoka kwenye sebule hii ndio unakutana na Ofisi yenyewe ambayo yumo Rais.

Walipofika hapa ndipo Sekretari wa Rais, akamuambia Charles asubiri hapo Rais ana mgeni ofisini kwake.

Mara kwanza Charles hakuelewa kwanini hakuambiwa asubiri kwenye ile mapokezi ya kwanza na matokeo yake ameletwa sehemu hii ya Rais kupumzika, lakini baadae alikuja kuelewa kuwa walikuwa hawataki mtu mwingine amuone Charles pale mapokezi.

Sekretari huyu wa Rais aliyeitwa Frederick Ndunguru, alimletea chai Charles na wakawa wanakunywa pamoja huku anampa kampani ya maongezi ya hapa na pale wakisubiri huyo mgeni aliye ndani ya ofisi atoke.

Kama dakika kumi baadae mgeni huyo alitoka, na alikuwa ni Waziri wa Fedha Bw. Abdul Aziz, mtanzania mwenye asili ya kiarabu.

"Hujambo kajuna" Wazidi Aziz akamsalimia Charles.

Charles akasimama kwa heshima, "Sijambo, shikamoo Mzee"

Waziri akaitikia na kuobdoka. Charles alishangaa kidogo kwa kutambuliwa mpaka jina na Waziri Aziz.

"Rais anaweza kukuona sasa!" Sekretari wa Rais Bw. Frederick Ndunguru alimkaribisha Charles baada ya kuingia na kutoka ofisini kwa Rais ambako alienda kumpa taarifa juu ya uwepo wa Charles.

Charles akafungua mlango kwa heshima zote na kuingia Ofisini.

Ofisi ya Rais ilikuwa maridhawa kabisa. Haikuwa na vitu vingi sana lakini ilipendeza. Kulikuwa na kabati la vitabu mkono wa kushoto, mkono wa kulia ukutani kulikuwa na michoro kadhaa ukutani pamoja na picha. Nyuma ya kiti cha Rais kulikuwa na dirisha kubwa ambalo lilikuwa lina mapazia murua kabisa.
Mbele ya Rais kulikuwa na meza ya ofisi ya saizi ya kati ya mti wa mpingo na upande wa pili wa meza kulikuwa na viti viwili kwa ajili ya kukaa mgeni kuongea na Rais.
Rais, alikuwa ananiangalia na kutabasamu nilivyokuwa naishangaa ofisi yake.. Hakuna mzee japokuwa tayari mvi zilianza kwa mbali kuonekana kichwani mwake. Ndio athari ya "mzigo" wa Urais. Mwili unaanza kuzeeka kabla ya muda wake.

"Karibu sana Kajuna, keti kwenye kiti" Rais, akamkaribisha Charles.

"Asante sana mzee, shikamoo" Charles akaitikia kwa heshima huku akiketi kwenye kiti, akitoa tabasamu fulani la kama aibu hivi baada ya kugundua Rais amegundua jinsi anavyoshangaa ofisi.

"Usijali, kila mtu akiingia humu mara ya kwanza lazima ahakikishe anapata kumbu kumbu kamili kichwani juu ya ofisi inayoendesha nchi hahahah" Rais akaongea kwa utani.

Rais alikuwa na staili adhimu kabisa ya uongozi. Licha ya kuwa moja ya viongozi wenye ushawishi zaidi barani Africa alikuwa na namna ya kumfanya mtu awe 'comfortable' anapoongea naye.
Akaanza maongezi kumuuliza Charles habari za Nairobi, humo humo akatumbukizia stori za hapa na pale anazozijua kuhusu Nairobi, na baada dakika kadhaa akaanza kuongea lengo la kumuita hapo.

"Charles, Kuna jambo nataka utusaidie" Rais akaongea akiwa serious.

"Ndio Mzee.." Charles akaitikia.

"Siki si nyingi tutaivunja East African Currency Board.!" Rais akaongea huku akiangalia 'reaction' ya Charles.

"Aisee! Sijawahi kusikia hilo Mzee ingawa niko kwenye nyanja ya banking" Charles akaongea kwa mshangao.

"Ni taarifa ya siri sana huwezi kuisikia"

"Aisee italeta mtikisiko sana kwenye sekta ya benki" Charles akagusia.

"Charles.. Unajua kipindi tunaanzisha East Africa Community, lengo letu ni kwamba ndani ya muda mchache tuwe na political federation.. Na ndio hii ikatufanya kuanzisha East Africa Currency Board tukiwa na lengo baadae ije kuwa East Africa Central Bank.. Sijui unanielewa sawa sawa Charles..?"

"Nakuelewa Mzee.!"

"Sasa miaka ya karibuni kitu hiki kinaanza kuonekana kama ndoto ambayo haitatimka... Kila nchi imekuwa na lwake sasa.. Vikwazo vimekuwa vingi, hasa wenzetu wa Kenya.. na tunataarifa kuwa wameanza michakato ya kuanzisha benki kuu yao.."

"Haiwezekani mzee! Watafanyaje hivyo ilhali wote tunatumia sarafu moja.." Charles akashangaa.

"Tuna taarifa kuwa wako na huo mchakato.!"

"Aiseee.!" Charles bado alikuwa na mshangao.

"Sasa kuna suala tunataka utusaidie Charles.." Rais akaongea akiwa amemkazia macho Charles.





*****************





WIKI TATU MBELE


Charles na Mkewe Sophia walikuwa wamepatiwa nyumba ya serikali maeneo ya Mikocheni A, nyumba ikiwa karibu kabisa na bahari.

Mkewe alikuwa analaani sana kupewa nyumba naeneo haya kwani harufu kutoka baharini ilikuwa inamkera sana ukizingatia ni mja mzito.

Siku hii majira ya kama saa nne usiku walikuja kugongewa mlango.
Charles akaenda kuwafungulia.

Kwa mshangao mkubwa ugeni huu ulikuwa ni wa waziri wa fedha Bw. Abdul Aziz na mzee tajiri na maarufu jijini Dar es salaam aliyeitwa Chifu Sekioni.

Baada ya kuwakaribisha sebuleni hawakupoteza muda, wakaenda moja kwa moja kwenye lengo la kufika hapa nyumbani kwa Charles.

"Ndugu waziri, vipi kuna dharura gani mbona usiku usiku hivi?" Charles akauliza baada ya wote kuketi.

"Hakuna dharura, ila kuna 'ofa' tumekuletea" Akaongea Chifu Sekioni.

"Ofa??" Charles akaongea kwa mshangao.

"Ndio! Tunataka kukufanya kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania ambayo itaundwa miezi michache ijayo" Waziri Azizi akaongea bila kuzunguka mbuyu.

"Wat?? Haya maelezo unayonipa ni ya kiserikali au??" Akauliza Charles kwa mshangao.

"Hapana, siongei kama waziri hapa! Naongea mimi binafsi kama Abdul Aziz"

"Ok! Nawasikikiza" akaongea Charles.

"Kama utaoendezwa na ofa yetu, kesho atakuja kijana muda wa usiku kama huu kukuchukua na piki piki.. Kama utakuwa tayari njoo naye mpaka atakapokuleta ili upate maelezo kamili." Akaongea Chifu Sekioni huku wanaanza kunyanyuka.

"Sijawaelewa ati mnachokiongea!"

"Una masaa ishirini na nne kutafakari" akaongea waziri Aziz kisha wakaondoka.

Wakamuacha Charles akiwa amechanganyikiwa. Hajui ni nini kimetokea pale. Huu ulikuwa utani au suala gani??

Akarudi kulala.


Kesho yake muda kama ule, kweli akaja kijana na piki piki. Bila Hiyana, charles akakwea piki piki na kuondoka na huyo kijana.
Alikuwa na sababu mbili za kumfanya aende.. Moja ni ofa aliyoambiwa kuwa wanaweza kumfanya kuwa Gavana wa Benki Kuu.! Hakuna ndoto kubwa ya 'banker' yeyote kama kupata fursa ya kuwa Gavana wa benki kuu.. Sababu ya pili ilikuwa ni rahisi tu, "usikatae wito, kataa maneno"

Kijana huyu akaendesha piki piki kutoka Mikocheni mpaka Upanga mtaa wa Isevya.
Hapo wakaelekea kwenye nyumba Fulani yenye geti jeusi na kugonga.

Baada ya kufunguliwa, wakaingia ndani na yule kijana akabaki sebuleni huku Charles akipelekwa kwenye chumba fulani hivi.

Chumba hiki kwa ndani kilikuwa kama chumba cha daktari mandhari yake.

Dakika chache baadae akaingia mwanamama mmoja akiwa na kibegi cheusi.

Hakuwasalimia wala nini, akaweka kibegi juu ya meza na kutoa sindano na kama kikontena hivi.

"Naomba mkono wako wa kushoto" yule mama akaongea.

"Hey, mnataka kunitoa damu ili iweje??" Charles akang'aka.

Yule mama mwenye sindano hakusema chochote, akamgeukia mwenyeweji wao na kumwangalia.

Mwenyeji wao ambaye alikuwa ni mama wa makamo hivi akaanza kuongea. Akamshika Charlea begani na kuongea kwa utaratibu..
"Charles, kama una amani na hiki kinaxhofanyika uamuzi ni wako, inaweza kugeuza na kurudi nyumbani kwako sasa hivi"

Charles akajifikiria. Akaona kama ameanza kumla ng'ombe ni vyema amalizie kabisa hadi mkia.

Akampa mkono yule mama.

Yule mama akamtoa damu na kisha kuhifadhi sindano kwenye kikontena.
Kisha akamchukua alama za vidole kwa kutumia wino na kugusishwa vidole kwenye karatasi.
Baada ya hapo yule mama akafungasha vitu vyake kwenye kibegi chake cheusi na kuondoka.

Baada ya hapo yule jamaa mwenye piki piki usiku huo huo akamchukua Charles kutoka hapo upanga na kumpeleka maeneo ya Oysterbay, mtaa wa Mzinga.

Wakaelekea kwenye nyumba moja yenye Ukuta mkubwa na geti kubwa jeusi na kugonga.
Walipofunguliwa na mlinzi, wakaingia ndani.
Ndani kulikuwa na nyumba kubwa na eneo la mbele yalipaki magari kadhaa.

Yule kijana akamuongoza Charles ndani ya nyumba mpaka kwenye chumba fulani hivi.

Ndani ya hiki chumba kilikuwa kama ofisi hivi na alimkuta yule mzee, Chifu sekioni Peke yake amekaa.

"Karibu sana kajuna" Chifu sekioni akamkaribisha kwa bashasha kwenye kiti.

Chifu Sekioni alikuwa amevaa kaunda suti nadhifu nyeusi na mkono wa kushoto usawa wa titi alikuwa na pini fulani ya dhambarau ambayo katikati ilikuwa na kama mchoro wa kichwa cha simba kwa rangi ya dhahabu.

"Tufanye haraka haraka wengine wanatusubiri" Chifu akaongea huku anaweka makaratasi mezani.

"Wengine akina nani?" Charles akauliza.

"Si umeona magari yamepaki hapo nje... Wengine wapo chumba kinachofuata wanatusubiri sisi tuanze kikao" Chifu Sekioni akaongea huku anaandika andika kwenye karatasi.

"Na unaweza kunambia "nyiny", ni akina na nani na lengo la kuniita hapa ni nini?" Charles akauliza.

Chifu Sekioni akatabasamu.

"Tunaitwa The Board, na lengo la kukuita hapa utalijua kwenye kikao ndani ya muda mchache.."

Charles akabaki amemkodolea macho tu.

"Nikumbushe majina yako kamili tafadhali" Chifu Sekioni akauliza huku anajiaanda kuandika kwenye yale makaratasi.

"Charles Bernard Kajuna"




***************


January, 2017


Leo ndio ilikuwa siku ambayo nilikuja kulipia ofisi.

Nilikuwa nimeongozana na Kaburi pamoja na Cheupe.

Mwenye nyumba alikuwepo, dalali pamoja na mtoto wake mwenye nyumba ambaye alikuja kama shahidi wa makabidhiano ya hela na kusaini mkataba wa kupanga.

"Nikumbushe majina yako kaka" akaongea dalali Tunda akiwa anaandika andika kwenye ule mkataba wa kupanga.

"Rweyemamu Charles Kajuna" nikamjibu.

Baada ya hapo tukasaini mkataba, nikawakabidhi hela wakaondoka.

Tukabaki, mimi, cheupe na Kaburu.
Tukaanza kukagua kagua mandhari ya ofisi.

"Iko poa?" Nikawaliza.

"Yeah! Iko poa sana ingawa bado sijui unataka kuifanyia nini?" Kaburu akajibu.

"Well now inabidi niende mjini kununua vifaa vya ofisi, meza, viti na kadhalika" nikaongea huku nimeweka mikono mfukoni nikiwaangalia wote na kutabasamu.

"Kabla ya yote unaweza kutudokeza mpango wako?? I really hate being in the dark.!" Kaburu akaongea serious akiwa amenikazia macho.


"Ok! Ngoja niwadokeze kiduchu tu.!" Nikatabasamu.





Itaendelea Ijumaa…
 
EPISODE 23, POST # 4057


Nifah Divine... glory to yhwh BansenBurner Alisen Papushikashi Magazine Fire miss chagga SANCTUS ANACLETUS mngony Excel Mussolin5 Jimena Inferiority Complex gwijimimi wambura marwa Hoshea shareef conscious wambeke The Boss Deejay nasmile gkileo Juma chief Mangi flani hivi Ngongo makaveli10 KENZY kadada wa pili Root aretasludovick jonnie_vincy Clkey KAFA.cOm mbewe makedonia Afande Nyati peterchoka Leonard Robert Nchi Kavu STUNTER Chrizo jully Van persie Khalidoun Tetramelyz punje haradari Mazigazi Alybaba babu na mjukuu platozoom jimmyfoxxgongo Nicodemas Tambo Mwikozi Ls man Heaven Sent sifongo Infantry Soldier haa mym 20acres MTS MarkHilary compos Tembo2 Erick the future nancy1983 Bulah binsaad Fazzaly the wolf everhurt Melvine Mgibeon kijana wa leo samsun Coolant Jagood pacesetter apologize payton George Betram kisengeli Kiranga Jiwe Linaloishi Madame B jay john Guasa Amboni Dinazarde Analyse Diva Beyonce snowhite Mmanu Expected Value onechromosome Missy rose Innocenthezron Immortal_MH Ficus sunola Robot la Matope mamaafacebook II JEKI likikima Compact scorpio me G'taxi YNWA adna yuzo ntamaholo Otorong'ong'o naan ngik-kundie kandukamo1 AFRICA101 mwalidebe Kobe Blaki Womani kalendi savius The Great Emanuel r2ga Ntaluke.N. Transcend Msemachochote Mchumiajuone mwampepec MTOTO WA KUKU Fukara proto cute kawombe zinginary MLALUKO JR Vupu barafu BlackPanther Ntuzu Matola impongo ntamaholo Mkoroshokigoli Deadbody KING easy mahoza Msolo kkenzki deborah1 KIDUDU buffalo44 winlicious riziki Allys MUHUNZI Moses2015 nacktary Liuumi dochivele Renzo @barbers hmjamii mbere TATIANA famicho LUCKDUBE mwanadome Straton memphis ghazar Graph Theory Honey Faith Shunie Slave ddcmanesto zinginary pacesetter Nkanaga KOMUGISHA mikatabafeki johnsonmgaya lee empire wigo MJINI CHAI Asprin mtzmweusi Erasto kalinga Chrizo kichakaa man LULU bike FORTALEZA poleni shibumi ZE DONE umande Edger Sr sir joshua sammoo Roram Password Bavaria hambiliki mwanangu Asili100 Evarist Massawe nice1 Jumong S Rogie 1babake nasreen uberito baest dustless Kilemachocho Tumosa mtembea kwa miguu Debbs Joe scorpnose musacha shibumi seeker of knowledge Simuchi Veni Vidi Vici TUJITEGEMEE abuu garcia Hon Nkundwe Festo Festo marion09 mike2k The dream bro kay vandelintz kirikou1 POINT LOAD lusaka city Dirham Rodcones bato MANCNOO multiphill90 GEORGE Dalali mwanamalundi90 MwaFreeca Roram Ta-kibombo troublemaker mambo KOMUGISHA calabocatz Papaa Azonto Msemachochote Mdomo bakuli tizo1 option dikembe iL Buono fakalava ABDUL KAREEM Gobe Justine Marack Goodluck Mchika MR UNINFORMED darcity nkasoukumu nG'aMBu thatonegAl kabanga MPARE KIBOGOYO Edward Sambai Rassa mnonje srinavas last king of uscoch proto cute Kennedy krava Rais2020 kbosho Mzee wa BsN sam2000 fuma 999 Bableee dawa yenu The Certified DON SINYORI mij adden
bwii ONTARIO Kobe The Vein Mondray jaxonjaxon successor mzee wa liver sawariya Sitaki ukuda Domhome Mpatanishi MKANDAHARI mtugani wa wapi huyo wealthier cluecell Toyota escudo mgumu2 troublemaker Linamo shedede
 
EPISODE 23, POST # 4057


Nifah Divine... glory to yhwh BansenBurner Alisen Papushikashi Magazine Fire miss chagga SANCTUS ANACLETUS mngony Excel Mussolin5 Jimena Inferiority Complex gwijimimi wambura marwa Hoshea shareef conscious wambeke The Boss Deejay nasmile gkileo Juma chief Mangi flani hivi Ngongo makaveli10 KENZY kadada wa pili Root aretasludovick jonnie_vincy Clkey KAFA.cOm mbewe makedonia Afande Nyati peterchoka Leonard Robert Nchi Kavu STUNTER Chrizo jully Van persie Khalidoun Tetramelyz punje haradari Mazigazi Alybaba babu na mjukuu platozoom jimmyfoxxgongo Nicodemas Tambo Mwikozi Ls man Heaven Sent sifongo Infantry Soldier haa mym 20acres MTS MarkHilary compos Tembo2 Erick the future nancy1983 Bulah binsaad Fazzaly the wolf everhurt Melvine Mgibeon kijana wa leo samsun Coolant Jagood pacesetter apologize payton George Betram kisengeli Kiranga Jiwe Linaloishi Madame B jay john Guasa Amboni Dinazarde Analyse Diva Beyonce snowhite Mmanu Expected Value onechromosome Missy rose Innocenthezron Immortal_MH Ficus sunola Robot la Matope mamaafacebook II JEKI likikima Compact scorpio me G'taxi YNWA adna yuzo ntamaholo Otorong'ong'o naan ngik-kundie kandukamo1 AFRICA101 mwalidebe Kobe Blaki Womani kalendi savius The Great Emanuel r2ga Ntaluke.N. Transcend Msemachochote Mchumiajuone mwampepec MTOTO WA KUKU Fukara proto cute kawombe zinginary MLALUKO JR Vupu barafu BlackPanther Ntuzu Matola impongo ntamaholo Mkoroshokigoli Deadbody KING easy mahoza Msolo kkenzki deborah1 KIDUDU buffalo44 winlicious riziki Allys MUHUNZI Moses2015 nacktary Liuumi dochivele Renzo @barbers hmjamii mbere TATIANA famicho LUCKDUBE mwanadome Straton memphis ghazar Graph Theory Honey Faith Shunie Slave ddcmanesto zinginary pacesetter Nkanaga KOMUGISHA mikatabafeki johnsonmgaya lee empire wigo MJINI CHAI Asprin mtzmweusi Erasto kalinga Chrizo kichakaa man LULU bike FORTALEZA poleni shibumi ZE DONE umande Edger Sr sir joshua sammoo Roram Password Bavaria hambiliki mwanangu Asili100 Evarist Massawe nice1 Jumong S Rogie 1babake nasreen uberito baest dustless Kilemachocho Tumosa mtembea kwa miguu Debbs Joe scorpnose musacha shibumi seeker of knowledge Simuchi Veni Vidi Vici TUJITEGEMEE abuu garcia Hon Nkundwe Festo Festo marion09 mike2k The dream bro kay vandelintz kirikou1 POINT LOAD lusaka city Dirham Rodcones bato MANCNOO multiphill90 GEORGE Dalali mwanamalundi90 MwaFreeca Roram Ta-kibombo troublemaker mambo KOMUGISHA calabocatz Papaa Azonto Msemachochote Mdomo bakuli tizo1 option dikembe iL Buono fakalava ABDUL KAREEM Gobe Justine Marack Goodluck Mchika MR UNINFORMED darcity nkasoukumu nG'aMBu thatonegAl kabanga MPARE KIBOGOYO Edward Sambai Rassa mnonje srinavas last king of uscoch proto cute Kennedy krava Rais2020 kbosho Mzee wa BsN sam2000 fuma 999 Bableee dawa yenu @charmie DON SINYORI mij adden
bwii ONTARIO Kobe The Vein Mondray jaxonjaxon successor mzee wa liver sawariya Sitaki ukuda Domhome Mpatanishi MKANDAHARI

Dahh mpaka leo Simo wacha niendelee kuvuta Subra
Mkuu The bold nikumbuke
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom