Vipengele vya 'kishetani' ndani ya katiba ya NCCR! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vipengele vya 'kishetani' ndani ya katiba ya NCCR!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Malafyale, Dec 20, 2011.

 1. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #1
  Dec 20, 2011
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,209
  Likes Received: 3,622
  Trophy Points: 280
  Hawezi kukata rufaa

  ""Mwanasheria wa NCCR Mageuzi, Dk Sengondo Mvungi alisema Kafulila hawezi kukata rufaa sehemu yoyote dhidi ya uamuzi wa kumfukuza uanachama kwa mujibu wa kanuni ya 7 (2) ya chama hicho.

  Kanuni hiyo ya 7(2) ya nidhamu na usuluhishi sehemu ya (d) inaeleza kuwa, baada ya uamuzi wa mwisho kufanywa, kikao husika kitatoa maelekezo kwa kikao au vikao vya chini vyenye mamlaka ya kuchukua hatua au kutoa adhabu kwa kiongozi au mwanachama husika. Kipengele (f) kinasema uamuzi utakaofanywa kwa mujibu wa kupengele (d) utakuwa wa mwisho ila tu pale unapomhusu Mwenyekiti Taifa na Makamu Mwenyekiti (Zanzibar) ambao uamuzi wa mwisho kuwahusu wao ni Mkutano Mkuu.


  Kanuni hiyo hiyo sehemu ya 7(1) inaeleza, ''Mlalamikiwa au mhusika atakuwa na haki ya kukata rufaa kwenda kamati ya nidhamu na usuluhishi iliyo katika kikao cha ngazi ya juu zaidi ya kikao husika, na kamati hiyo itakuwa na uwezo sawa na ule wa kamati ya kwanza, ila tu haitapokea ushahidi mara ya pili''.

  MY NOTES:
  Kwa katiba za ajabu kama hizi za NCCR;Je wana mageuzi tuna haki ya kuipa pressure serikali kushirikiana na wadau kuandika katiba mpya?Je Nape akianza kusema kabla ya kuiambia serikali ilete katiba mpya ingelikuwa vyema mngezisafisha zenu zilizooza!tutamjibu nn?

  Kafulila alichaguliwa kwa kura maelfu kule Kigoma-Kusini lkn likely atapoteza Ubunge wake kwa kunyang'wanywa kadi na watu wasio zidi hata 100 waliokutana wakiwa na agenda ya kumtimua wakiongiozwa na Mwenyekiti wao Mbatia ambaye katiba imemfanya awe na nguvu kama ya Mungu-mtu!

  Katiba ya NCCR kuhusu kufukuzana ni madudu matupu;Je kuna yeyote hapa anayo katiba ya vyama vikuu vya upinzani vya CHADEMA na CUF nione tofauti zao kwenye vipengele vya kufukuzana?
   
 2. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #2
  Dec 20, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Vyama vingine katiba anayo mwenyekiti tu, ndo maana mwanachama anayejitokeza kutaka kugombea uenyekiti anakuwa adui wa mwenyekiti. Hayo yamemkuta: TAO, Jidura mabambashi, Zito etc. Vyama vya upinzani bado viko mbali sana.
   
 3. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #3
  Dec 20, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  mtasema sana, kafulila hakuisoma hiyo katiba ya nccr alipoona katiba ya cdm haifai?
  Hiyo katiba imetokea kuzimu sasa hivi? Hamkujua kuwa ipo na Mbatia akisema 'nitakushughulikia' anaweza?

  Kafulila kachemsha, huo ndio ukweli.
  Kama ametuhumiwa na kikao halali kikamkaanga imekula kwake.
   
 4. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #4
  Dec 20, 2011
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Mbona umsahau Marehemu Kolimba? Alikufaje? Kikwete alipingwa na nani Uenyekiti wa CCM?
  Nakumbusha tu vyama vyote vya siasa vimeiga udikteta wa CCM kuhusu nguvu ya Mwenyekiti wa Chama; matokeo yake ni kuwa na Mwenyekiti na Rais mwenye mamlaka kama ya Mungu.
   
 5. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #5
  Dec 20, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  yaliyomkuta shibuda ccm ndiyo laana tuliyonayo tanzania,katiba zote zina matatizo ndiyo maana tunataka katiba ya wananchi.
   
 6. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #6
  Dec 20, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,357
  Trophy Points: 280
  mvungi ni swahiba wa mbatia,kwa hiyo mvungi naye ccm..
   
 7. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #7
  Dec 20, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,969
  Likes Received: 2,963
  Trophy Points: 280
  Kafulila anapishana na "good life".
   
 8. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #8
  Dec 20, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Mkuu sidhani kama unafahamu kuwa Amani Jidulamabambasi Nzugile(RIP) is no more. Ninakubaliana na wewe jamaa alikuwa naye ni kichwa hasa katika kujenga hoja. Mungu Amrehemu
   
 9. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #9
  Dec 20, 2011
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,209
  Likes Received: 3,622
  Trophy Points: 280
  Kwa kweli inaniuma sana;Mtu aliyechaguliwa na wananchi wa vyama tofauti na independents lkn anafukuzwa na kikundi cha watu wachache mno kwa sababu tu kapingana na Mwenyekiti;hi haikubaliki na tunampa Nape points za bure kabisa kutushambulia mwaka 2015!
   
 10. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #10
  Dec 20, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  mimi nashangaa, kwa nini hamtaki kafulila afukuzwe? wakati kakosea?, inamaana tangu anaondoka CDM alionewa? au yeye ni mroho wa madaraka na anatumiwa sana na zito, Mwambieni Zito atamponza.

  Kama kafulila kufukuzwa mnalalamika? je huko china wanaonyonga wahalifu itakuwaje wakati nasi ndio tunatakiwa kueleka huko.
   
 11. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #11
  Dec 20, 2011
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,986
  Likes Received: 3,735
  Trophy Points: 280
  you got a point kikolo, esp hapo kwenye red. very valid point.

  before pointing a finger at one's neighbour or brethrens, one should always take a very good stock of oneself first.

  read Matthew 7:1-5.
   
Loading...