Vipaumbele vya Lowassa vyampendeza JK

Vipaumbele vya Lowassa vyampendeza JK

IamPrince George

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2014
Posts
412
Reaction score
168
*VIPAUMBELE VYA LOWASSA VYAMPENDEZA JAKAYA KIKWETE,

*MAFUGULI AMHOFIA LOWASSA.

Tarehe 15. 08. 2015 majira ya saa 12:40 kulekea saa saba mchana katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam kulikuwa na Sherehe ya kumuaga Rais Jakaya Kikwete sherehe iliyoandaliwa na Wizara ya Ujenzi chini ya Mh. Magufuli kwa mwamvuli wa Makandarasi.

Mh. Magufuli alisikika akisema kuwa Mheshimiwa Rais nakushukuru kwa kusaidia bodaboda kuwepo nchini na kusaidia vijana kujiajiri na ninashangaa hao wanaosema watawapa ajira na kuwasaidia Bodaboda na kusahau kuwa zilitoka na zililetwa na nani Hapa nchini. (Hapa alikuwa akimuongelea Lowassa kwa kuamini kuwa ndiyr tishio kwake).

Mh. Magufuli alisema pia kuwa, Mh Rais Sekta ya Ujenzi ndio sekta kubwa na ya kwanza inayosaidia uchumi wa taifa, lakini Mh. Jk alipozungumza alisema kuwa Sekta ya Elimu ndio sekta kubwa sana na ambayo tunatakiwa kuiangalia na kuipa kipaumbele ikifuatiwa na Sekta ya Ujenzi.

Ni wazi kuwa Lowassa anajua kuwa Elimu ndio msingi wa maendeleo katika taifa lolote duniani na kimsingi ndio kipaumbele chake na Jayaka Kikwete amelisema hilo kwa kuamini kuwa Lowassa yuko sahihi.

Sasa Mh. Magufuli ambaye ndie mgombea Urais nashindwa kuamini kuwa hajui kuwa elimu ndio msingi au ni kweli kuwa Urais kwake haikuwa plan yake, na je, hawakujipanga mapema na Mwenyekiti wake ili wasipishane kauli au ilikuwaje, Maana Magufuli anasema Ujenzi ndio Sekta Muhimu lakini JK anasema Elimu ndio sekta muhimu.

Wananchi hii ndio CCM, Magufuli anasema akiwa Rais Walimu wote watanunuliwa Laptop lakini Nape anakanusha na kusema kuwa Magufuli hakusema hadharani, na maana ya kwamba hakusema hadharani ni kwamba alisema, sasa kama wao kwa wao wanageukana kauli, je, hawatawageuka wananchi?

Lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida JK alitumia nafasi hiyo kufanya kampeni na kuonesha wasiwasi wake juu ya Lowassa kwa kuonekana kumzungumzia Lowassa kwa kusema, (Ndugu Nagufuli usihofu hao wengine ni moto wa mabua, hauwaku ukadumu), hiyo ni ishara ya kwamba LOWASSA amekuwa vichwani mwao (CCM) na kuwaumiza kichwa mpaka kufikia kumzungumzia kwa mabaya, hiyo ni dalili mbaya sana kwa CCM na ni wazi kuwa LOWASSA anawatisha sana hususani sera zake ambazo zimewagusa sana watanzania na kumwamini.

KAZI MNAYO CCM.
 
Mgeja: Mwenyekiti wa CCM alikuja na majina matano mfukoni, tukamwambia mwenyekiti unafanya nn..? Unatuburuza vp..? Haya basi tusomee wasifu wa hao watu wako uliowachaguo watano...? Mwenyekiti kimya...asiyetaka aondoke CCM...majina ndio hayo...hutaki toka CCM...!!!
 
prince, hapo mwisho umesema lowasa ana sera zinazowagusa watanzania!
nambie ni sera gani na alizitaja lini, na wakati wa kampeini bado!!
yaani .!!!!
 
Nimemsikiliza Mh.Lowassa leo,nimependa jinsi anavyoainisha maeneo atakayoyagusa katika sera zake za kampeni,huu si wakati wa kubwabwaja hovyo sera kwa vile wakati kampeni bado,sheria ya uchaguzi itakufunga.kwa kusapoti tu Lowassa alishasema tangu yupo CCM kuwa ataipa kipaumbele zaidi elimu
 
kikubwa xa ivi ni kupambana na rushwa na ubadhilifu wa mali za umma. nchi haiwezi kua maskini wakati tuna rasirimali za kipekee apa duniani.
elimu kitu gani na wakati wapo kibao walioelimika ila mazingira ya ajira ni mabovu. atengeneze mazingira ya ajira kwanza.
 
unaelewa maana ya elimu wewe??
utamuajiri vipi mtu asiye na elimu??
 
unaelewa maana ya elimu wewe??
utamuajiri vipi mtu asiye na elimu??

we uelewi!
wapo kibao uku mjini wana elimu zao lakini mazingira ya kuajiri na kujiajiri ni mabovu!
kila mwaka watu wanahitimu mavyuo wanarundikana mitaani.!
tunataka mgawanyo mzuri wa resources, uwezi kua unasomesha tu na kutoa graduates kila mwaka afu wakae bure bila kuzalisha.
 
acha kukariri vibaya wewe......tunapozungumzia elimu tunamaanisha elimu kwa ujumla wake....... hujui kua CCM haijali vyuo vya kilimo?? veta, tuna madereva ambao hawajasoma vizuri,
in short lielewe neno elimu kwa upana wake
 
Eti mtoto wa KIKWETE ndiye anayeamua Rais atoka upande gani wa TANZANIA hii, watu wana laana hawa!!
 
Elimu kwanza ili sekta ziwe mikononi mwa wazawa..
 
na we uelewe kua katika distribution of resources, scale of preference haipaswi kua elimu. haimaanishi watu hawatatengenezewa mashule au serikari haitagharamia elimu!
NO..!
namaanisha serikari ipunguze au isiongeze mgao sana kwenye kufinance elimu na wakati aijaweka mkakati wa vipi walioelimika watatumia elimu yao kulifaidisha taifa kwa kujiajiri na kuajiri wengne au kuajiriwa.
 
Eti mtoto wa KIKWETE ndiye anayeamua Rais atoka upande gani wa TANZANIA hii, watu wana laana hawa!!

Hiyo yote ni kwasababu CCM imekuwa chama cha familia na kuwapuuza wazee na waasisi wa muhimu,ndio maana kinakufa.
 
Dah Jakaya bonge la msanii asee. Hivi kweli Ccm na Makufuli wanaamini Jakaya ni timu makufuli na si timu Ngoyai?
 
*VIPAUMBELE VYA LOWASSA VYAMPENDEZA JAKAYA KIKWETE,

*MAFUGULI AMHOFIA LOWASSA.

Tarehe 15. 08. 2015 majira ya saa 12:40 kulekea saa saba mchana katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam kulikuwa na Sherehe ya kumuaga Rais Jakaya Kikwete sherehe iliyoandaliwa na Wizara ya Ujenzi chini ya Mh. Magufuli kwa mwamvuli wa Makandarasi.

Mh. Magufuli alisikika akisema kuwa Mheshimiwa Rais nakushukuru kwa kusaidia bodaboda kuwepo nchini na kusaidia vijana kujiajiri na ninashangaa hao wanaosema watawapa ajira na kuwasaidia Bodaboda na kusahau kuwa zilitoka na zililetwa na nani Hapa nchini. (Hapa alikuwa akimuongelea Lowassa kwa kuamini kuwa ndiyr tishio kwake).

Mh. Magufuli alisema pia kuwa, Mh Rais Sekta ya Ujenzi ndio sekta kubwa na ya kwanza inayosaidia uchumi wa taifa, lakini Mh. Jk alipozungumza alisema kuwa Sekta ya Elimu ndio sekta kubwa sana na ambayo tunatakiwa kuiangalia na kuipa kipaumbele ikifuatiwa na Sekta ya Ujenzi.

Ni wazi kuwa Lowassa anajua kuwa Elimu ndio msingi wa maendeleo katika taifa lolote duniani na kimsingi ndio kipaumbele chake na Jayaka Kikwete amelisema hilo kwa kuamini kuwa Lowassa yuko sahihi.

Sasa Mh. Magufuli ambaye ndie mgombea Urais nashindwa kuamini kuwa hajui kuwa elimu ndio msingi au ni kweli kuwa Urais kwake haikuwa plan yake, na je, hawakujipanga mapema na Mwenyekiti wake ili wasipishane kauli au ilikuwaje, Maana Magufuli anasema Ujenzi ndio Sekta Muhimu lakini JK anasema Elimu ndio sekta muhimu.

Wananchi hii ndio CCM, Magufuli anasema akiwa Rais Walimu wote watanunuliwa Laptop lakini Nape anakanusha na kusema kuwa Magufuli hakusema hadharani, na maana ya kwamba hakusema hadharani ni kwamba alisema, sasa kama wao kwa wao wanageukana kauli, je, hawatawageuka wananchi?

Lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida JK alitumia nafasi hiyo kufanya kampeni na kuonesha wasiwasi wake juu ya Lowassa kwa kuonekana kumzungumzia Lowassa kwa kusema, (Ndugu Nagufuli usihofu hao wengine ni moto wa mabua, hauwaku ukadumu), hiyo ni ishara ya kwamba LOWASSA amekuwa vichwani mwao (CCM) na kuwaumiza kichwa mpaka kufikia kumzungumzia kwa mabaya, hiyo ni dalili mbaya sana kwa CCM na ni wazi kuwa LOWASSA anawatisha sana hususani sera zake ambazo zimewagusa sana watanzania na kumwamini.

KAZI MNAYO CCM.

Una mtindio wa ubongo, umeandika utumbo mtupu, shame on you!
 
Mgeja: Mwenyekiti wa CCM alikuja na majina matano mfukoni, tukamwambia mwenyekiti unafanya nn..? Unatuburuza vp..? Haya basi tusomee wasifu wa hao watu wako uliowachaguo watano...? Mwenyekiti kimya...asiyetaka aondoke CCM...majina ndio hayo...hutaki toka CCM...!!!
Duh ni noma na wameondoka kweli wanawaita makapi wakati makapi ni wao
 
Back
Top Bottom