Vipaumbele vya Lowassa vyampendeza JK

Vipaumbele vya Lowassa vyampendeza JK

prince, hapo mwisho umesema lowasa ana sera zinazowagusa watanzania!
nambie ni sera gani na alizitaja lini, na wakati wa kampeini bado!!
yaani .!!!!

Soma title utaelewa kamaanisha nini. Ni vipaumbele na mtu kitaja vipaumbele vyake sio lazima asubiri kampeni. Ili utoe tatizo mama la umasikini ni lazima uhusishe ELIMU na sio vinginevyo
 
kiukwel kila kitu kipangwe upya sera ya afya majanga sera ya elimu mashaka ajira ndo ucseme njaa imekisiri. rais ajae afikirie haya.
 
Kipaumbele cha Lowassa ni haya mambo matatu:

1. Elimu
2. Elimu
3. Elimu

Haitaji kusema kwani kashasema mara nyingi hata akiwa kule kwa magamba

Elimu ni ufunguo wa maisha
Mtu aliyeelimika hadanganywi kama sasa ccm wanavyofanya
Mtu akiwa na elimu anajua haki zake
Mtu akiwa na elimu haogopi
Taifa lenye wasomilina maendeleo
Taifa lenye wasomi haliogopi kuunfana na mataifa mengine, Tz tunawaogopa sana majirani zetu kwa sababu ya elimu yetu duni

Kiwango cha wanaojua kusoma na kuandika Tz imeshuka sana baada ya Mwalimu kung'atuka 1985

Yeyote anayesema Tanzania kuna wasomi na yeye hajitambui

Kiongozi yeyote anayekuja na kipaumbele mbali na elimu ni muongo na atafanya kama CCM walifanya kwa zaidi ya miaka 50 iliyopita
 
kikubwa xa ivi ni kupambana na rushwa na ubadhilifu wa mali za umma. nchi haiwezi kua maskini wakati tuna rasirimali za kipekee apa duniani.
elimu kitu gani na wakati wapo kibao walioelimika ila mazingira ya ajira ni mabovu. atengeneze mazingira ya ajira kwanza.

Fuatilia hata kwenye hotuba yake siku anatangaza nia, alisema kiwa hatuwezi kuwa nchi ya omba omba wakati tuna rasilimali, tutaweka misingi imara ya kushughulikia rushwa
 
Back
Top Bottom