Viongozi wetu wahakikishe wanaowaongoza wanakuwa na "Peace of mind"!

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,276
Mwisho wa siku sisi wote ni binadamu na tunataka kuona tunapoishi panakuwa sehemu salama na penye furaha kuishi,watu wake wanakuwa na "peace of mind".

Julius Nyerere,Dosa Azizi,Rashid Kawawa,Oscar Kambona,Bibi Titi hawakupambana na waingereza kwa sababu walishindwa kujenga viwanda,la hasha kwa sababu Waingereza walishindwa kutengeneza "peace of mind "kwa watanganyika

Akina Kinjektile Ngwale,Chief Milambo,Isike,Mkwawa,Rumanyika,Mareale hawakupambana na Wajerumani eti kwa sababu Wajerumani walishindwa kujenga viwanda,no,Wajerumani walijenga mabarabara,Reli,Mashule,Mahospitali,Majengo n.k,na watanganyika waliyaona,lakini watanganyika hawa hawakuwa na "Peace of Mind".

Akina Nelson Mandela,Steve Bhiko,Oliver Tambo,Desmund Tutu,waliendesha mapambano na makaburu si kwa sababu hawakuibadilisha Afrika ya kusini,no,hawa makaburu ndiyo walioifanya Afrika ya kusini kuwa kama Ulaya kimiundombinu,lakini hawakuwapa weusi "Peace of mind"

Binadamu anahitaji zaidi "Peace of mind",hata katika familia Baba unaweza kuwa na mali nyingi,kila kitu kipo,ila ukishindwa kutengeneza "Peace of mind"kwa mke na watoto,mali ulizonazo ni sawa na bure!.

Viongozi wetu wahakikishe wanaowaongoza wanakuwa na "Peace of mind"!

Hata ofisini,hata kama unamlipa mtu shilingi milioni 2 kama "take home",akikosa "peace of mind" ipo siku ataacha kazi na kwenda kwenye "take home" ya laki saba ila anapata "peace of mind"

Hujawahi kuona binti anaacha kuolewa na kijana mwenye pesa nyingi,anakwenda olewa na kijana mwenye kipato cha kawaida?mwisho wa siku maisha yanataka "Peace of mind"!

Hujawahi kutana na kijana kaachana na binti msomi,mzuri mwenye kazi nzuri,anakwenda kuona binti mwenye kazi ya kipato cha kawaida?kafuata "Peace of mind".

Kiasili binadamu anataka "peace of mind"watu wako wakiikosa hii ni hatari sana!.
Huu utawala upo madarakani viongozi wengi wamekosa "Peace of mind " ..
 
agreed kwa yote,na mtu akikutukana wewe ni mbwa wakati unajielewa kuwa sio mbwa,maana hauna mkia,hauna miguu minne ,kichwa chako hakijachongoka kama cha mbwa,na akaamua kukaa kimya bila ya kumjibu ,maana unajijua sio mbwa sasa hapa nani ni juha?
 
".....Kiasili binadamu anataka "peace of mind"watu wako wakiikosa hii ni hatari sana!."

Well said mkuu
 
Attachments

  • bitmoji-20170705115205.png
    bitmoji-20170705115205.png
    11.5 KB · Views: 24
Mwisho wa siku sisi wote ni binadamu na tunataka kuona tunapoishi panakuwa sehemu salama na penye furaha kuishi,watu wake wanakuwa na "peace of mind".

Julius Nyerere,Dosa Azizi,Rashid Kawawa,Oscar Kambona,Bibi Titi hawakupambana na waingereza kwa sababu walishindwa kujenga viwanda,la hasha kwa sababu Waingereza walishindwa kutengeneza "peace of mind "kwa watanganyika

Akina Kinjektile Ngwale,Chief Milambo,Isike,Mkwawa,Rumanyika,Mareale hawakupambana na Wajerumani eti kwa sababu Wajerumani walishindwa kujenga viwanda,no,Wajerumani walijenga mabarabara,Reli,Mashule,Mahospitali,Majengo n.k,na watanganyika waliyaona,lakini watanganyika hawa hawakuwa na "Peace of Mind".

Akina Nelson Mandela,Steve Bhiko,Oliver Tambo,Desmund Tutu,waliendesha mapambano na makaburu si kwa sababu hawakuibadilisha Afrika ya kusini,no,hawa makaburu ndiyo walioifanya Afrika ya kusini kuwa kama Ulaya kimiundombinu,lakini hawakuwapa weusi "Peace of mind"

Binadamu anahitaji zaidi "Peace of mind",hata katika familia Baba unaweza kuwa na mali nyingi,kila kitu kipo,ila ukishindwa kutengeneza "Peace of mind"kwa mke na watoto,mali ulizonazo ni sawa na bure!.

Viongozi wetu wahakikishe wanaowaongoza wanakuwa na "Peace of mind"!

Hata ofisini,hata kama unamlipa mtu shilingi milioni 2 kama "take home",akikosa "peace of mind" ipo siku ataacha kazi na kwenda kwenye "take home" ya laki saba ila anapata "peace of mind"

Hujawahi kuona binti anaacha kuolewa na kijana mwenye pesa nyingi,anakwenda olewa na kijana mwenye kipato cha kawaida?mwisho wa siku maisha yanataka "Peace of mind"!

Hujawahi kutana na kijana kaachana na binti msomi,mzuri mwenye kazi nzuri,anakwenda kuona binti mwenye kazi ya kipato cha kawaida?kafuata "Peace of mind".

Kiasili binadamu anataka "peace of mind"watu wako wakiikosa hii ni hatari sana!.
Huu utawala upo madarakani viongozi wengi wamekosa "Peace of mind " ..
Upo sahihi mkuu
 
The problem is ....serikali ya Magufuli....Imejikita kwenye mental blackmail and Gaging people....

So peace of mind is will never be achieved....
 
Hii mpya hii.

Tangu lini serikali ikakupa hicho unachokiita "peace of mind? "

Happiness and inner awesomeness are from within.

Serikali ni mfumo mbovu tu wa binadamu kujitawala.

So get used to it.

Kutegemea serikali ikupe peace of mind ni sawa na kutegemea maji yajae kwenye tenga.
 
Piece of mind? Inaanza na hiyo mind yako,maana imo ndani yako.Ukijiepusha na kila aina ya conflict utaipata tu mkuu.Tii mamlaka,lipa kodi,usiibe,usiue nk.But is it easy?
Kila ufanyalo linamatokeo,usipofanya kazi hutakuwa na kitu,usipokuwa na kitu utalalamika?yes utamlalamikie Mr government,naye hatataka. Kama hiyo piece of mind tungeipata magereza yangekuwa ni makanisa na dunia ingekuwa nzuri sana.
 
Well said! Mi nimefurahishwa zaidi na orodha ndeefu ya uliowataja, ukiondoa Desmond Tutu waliobaki walishatangulia mbele za haki!! Kumbe kiburi cha binadam ni cha bure, hapa duniani ni pa kupita tu, tukiyajua haya basi tutajitahidi kutenda haki kwa wenzetu kwa maana njia yetu wote ni moja, kwa muktadha huu BINADAMU WOTE NI SAWA! Uwe na mali, mamlaka, nguvu na chochote kile. Mwenyezi Mungu apewe sifa kwa mizania hii
 
Piece of mind? Inaanza na hiyo mind yako,maana imo ndani yako.Ukijiepusha na kila aina ya conflict utaipata tu mkuu.Tii mamlaka,lipa kodi,usiibe,usiue nk.But is it easy?
Kila ufanyalo linamatokeo,usipofanya kazi hutakuwa na kitu,usipokuwa na kitu utalalamika?yes utamlalamikie Mr government,naye hatataka. Kama hiyo piece of mind tungeipata magereza yangekuwa ni makanisa na dunia ingekuwa nzuri sana.
Kila upande ukitimiza wajibu wake nasi kwa upande mmoja.
 
Viongoz wengi wanasahau walikotoka kabla ya kuwa kiongoz anamkosoa aliyekuwepo akipewa yeye anafanya kama aliyetoka huo msiba uliokuwepo
 
Unaongozwa na mtu mwenye inferiority complex halafu unategemea ajali 'peace of mind' yako wakati yeye hana!
 
Back
Top Bottom