Habari ndugu zangu.
Nawasalimu kwa upendo wa dhati toka ndani ya moyo wangu.
Nawapenda sana.
Aidha baada ya salamu hizo, naomba niende kwenye mada tajwa hapo juu.
Ni ukweli mchungu kwamba viongozi wetu hawana huruma na sisi.
Hili linajidhihirisha katika mambo mengi.
Yafuatayo ni baadhi ya mambo yanayoonesha viongozi wetu hawana huruma na sisi hata kidogo;
1. Mfumko wa bei.
Ni jambo la kusikitisha kwamba mfumko wa bei uko katika vilele vyake sasa. Ndani ya miaka miwili, mfumko wa bei umekuwa ukiongezeka kwa kasi ya kimbunga "Fred". Na jambo la kusikitisha sana ni kwamba viongozi wetu mnaonekana kutojihusisha zaidi ya kusingizia vita ya Ukraine na changamoto za Corona. Utafikiri sisi ndo tuko vitani uko Ukraine! Yaani tuko na hali mbaya zaidi kuliko Wa-Ukraine wenyewe wanaopigana! Cha kusikitisha wanaoonekana kuumizwa zaidi na huu mfumko wa bei ni watu wa Tabaka la chini. Wale wanaoishi chini ya dola moja. Yaani kwa hali ya sasa vitu vinapanda bei kila saa. Ukitoka gengeni kununua nyanya za 300, saa 2 asubuhi, saa 3 asubuhi ukirudi tena kuulizia bei utakuta zinauzwa 500! Sasa hivi ni ngumu sana kupata ndizi ya 200. Nyingi zinaanzia 250 hadi 300. Awali tulizoea ukiwa na 200 yako unapata fungu moja la mchicha au sukumawiki, lakini leo hii bila 500 hupati mboga za majani!
2. Tozo.
Mpaka leo bado sijaelewa mantiki ya haya matozo yasiyo na kichwa wala miguu kwenye miamala ya simu. Hivi kweli mnashindwa kusimamia vizuri mapato ya pale bandarini, kodi za wafanyakazi, Kodi za wafanyabiashara, kodi tunalipa kila tukinunua bidhaa kwa jina la VAT, madini n.k.
3. Matumizi yasiyo ya lazima ya serikali.
Eti tunajiita nchi maskini, halafu wskurugenzi tu wa halmashauri wanatembelea magari ya mamilioni, mawaziri wanaishi kwa ufahari kama wako peponi n.k.
4. Kauli za kukatisha tamaa za baadhi ya viongozi.
-eti kuleni kwa urefu wa kamba..
- kodi ya mafuta, iongezwe...
-gharama za simu na bando ziongezwe..
-wale ambao hamtaki, muhamie Burundi n.k
5. Kukopa kulikopitiliza.
Kila siku tunasikia deni la Taifa linaongezeka kwa kasi kuliko miradi ya maendeleo inayodaiwa kwamba fedha hizo zinazokopwa ni kwa ajili ya miradi hiyo.
6. Baadhi ya mawaziri wanaolalamikiwa na raia kwa utendaji mbovu, bado wanatamba na kujidai.
7. Kukatika katika kwa umeme.
Baadhi ya Watanzania wanategemea umeme kama sehemu yao ya kujiingizia kipato. Lakini cha ajabu kwa siku za hivi karibuni kumekuwa na katika katika ya umeme. Kila siku Watanzania wa watu maskini wanalalamika, lakini ni kana kwamba serikali yao imeziba masikio. Haisikii chochote. Macho yote yako kwenye namna ya kuzidi kulamba asali milele!
8. Kutowakanya baadhi ya watu wanaomtukana na kumsema vibaya kipenzi cha Watanzania walio wengi; Hayati JPM.
Hakuna Mtanzania anayejitambua, asiyethamini mchango mkubwa uliotolewa na Hayati JPM kwa nchi hii ya Tanzania.
Hivyo, maskini hawa Watanzania walio wengi kila wakisikia shujaa wao, anasemwa vibaya na baadhi ya viongozi, basi wanajisikia vibaya na kunyong'onyea..
Tafadhali sana, tunatamani kuona hawa watu wakionywa tu hata kwa maneno, kuliko kuendelea kuwaacha tu hivi hivi..
Mwisho kabisa nimalizie kwa kwa kuwaonya viongozi wangu kwamba jueni vyeo mlivyo navyo sasa hivi ni dhamana ambayo ina muda wake. Hivyo kuweni wanyenyekevu kwa mnaowangoza. Wapendeni raia wenu. Wahurumieni. Jitahidini kubuni namna za kuwapunguzia mizigo badala ya kuwaza namna ya kuwatwika watu wenu mizigo.
Jisikieni vibaya kuona watu walio wengi wanawalalamikia kila siku.
Kumbukeni malipo ni hapa hapa duniani.
Tupo tunawaangalia sana kwa umakini.
Tunapima kauli zenu na matendo yenu.
Nimalizizie kwa kuwaomba msikilize wimbo wa Roma Mkatoliki, na muufanyie kazi..
Chaika Chakaya bhamula!