Viongozi wetu na Dhana ya Kujilimbikizia Mali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi wetu na Dhana ya Kujilimbikizia Mali

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Regia Mtema, Jan 6, 2010.

 1. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #1
  Jan 6, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Wakuu .Habari!
  Kuna jambo moja linanishangaza sana naomba msaada wenu katika hili. Siku za Mazishi ya Mzee Kawawa na baada ya Mazishi yake,Mzee huyu amemwagiwa sifa mbalimbali.Moja ya sifa alizomwagiwa ni kuwa Mzee huyu hakujilimbikizia Mali. Hili mimi linanishangaza sana na inawezekana kabisa kwamba labda mimi sifahamu maana ya kujilimbikizia Mali. Wakati nafuatilia mazishi yake kwa njia ya Luninga niligundua kuwa huyu Mzee alikuwa na eneo kubwa sana pale nyumbani kwake Madale to the extent that maelfu ya watanzania waliweza kushiriki kwenye mazishi yake live bila ya chenga. Pia kuna eneo kubwa tu ambalo liko reserved kwaajili ya Makaburi ya wanafamilia. Hata kule kijijini kwake alikozaliwa alikuwa na eneo kubwa tu. Vile vile nimeambiwa kwamba Sophia House zote zilikuwa za Mkewew Sophia Kawawa.,Na hizi Sophia Houses zimezagaa kila kona ya jiji la Dar es Salaam. Hizi ni baadhi tu ya Mali nilizobahatika kuzifahamu lakini katika hizi bado mi naona jamaa wala hakuishi maisha ya kawaida kama watu wanavyodai.je kujilimbikizia mali ni kupi?au mapka uwe na mahoteli Makubwa ya Kitalii? Nisaidieni jamani.
   
 2. Mgeninani

  Mgeninani Senior Member

  #2
  Jan 6, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 190
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  labda alipewa maana yeye kama kuzijenga angejenga miaka ya 80 na alistaafu miaka hiyohiyo,ardhi ilikua rahisi mno enzi hizo na madale hakuna mtu alikua anataka kwenda kuishi huko, hizo sophia apartment sidhani kama zina muda zaidi ya miaka 20,tatizo si kuwa na mali shida umezipatajepataje? au labda umeshinda bahati nasibu
   
 3. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #3
  Jan 9, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Kujilimbikizia mali siyo haramu kabisa. Tatizo upatikanaji wa hizo mali ni kwa njia gani [halali au haramu]
  Kuhusu mzee wetu alihamia eneo hilo wakati lilikuwa pori tu na nadhani alifanya juhudi ya kuhamasisha watu kuhamia eneo hilo. Ingawa mimi siyo msemaji wa familia lakini ninavyofahamu hizo nyumba zilizoandikwa SOFIA HOUSE siyo za kina Kawawa bali ni za wahindi. Hilo jina la sofia lisionekane kuwa ni la maremu mkewe mzee wetu.
   
Loading...