Viongozi wanatakiwa kuwaheshimu wananchi waliowapa madaraka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi wanatakiwa kuwaheshimu wananchi waliowapa madaraka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KILAMHAMA, Dec 7, 2011.

 1. K

  KILAMHAMA Member

  #1
  Dec 7, 2011
  Joined: Dec 7, 2011
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu zanguni, hapa tanzania viongozi hawana heshima kwa wananchi ambao ndio wamewapa madaraka, hapo nyuma kidogo wakati wa mugao mkali wa umeme kuna kiongozi mwandamizi wa tanesco aliyesema eti yeye binafsi na shirika la tanesco halidhani kama watanzania wanaadhirika kwa mgao wa umeme! lakini pia jana spika wa bunge la tanzania amekanusha kile alichokisema katibu wake kwamba posho za wabunge hazijapanda kama vyombo vya habari vilivyotangaza, yeye anna makinda amesema ni kweli posho zimepanda kutoka 70,000 tshs mpaka kufikia 200,000 tshs ikiwa niongezeko la 130,000tshs, aidha spika amefafanua vizuri kwamba ongezeko hilo ni kutokana na ugumu wa maisha na kupanda kwa gharama za masha. Lakini je gharama za maisha zinapanda kwa wabunge peke yao, hivi serikari haioni ugumu wa maisha unaotukabili sisi wananchi wa kawaida? mwalimu anayefundisha dodoma mwenye degree moja analipwa 361,000 kwa mwezi, je yeye gharama za maisha kwake hazijapanda mbona haongezewi mshahara ili aweze kukabili ugumu wa maisha? nawashauri viongozi wawaheshimu wananchi ambao ndio wamewapa madaraka kwasababu siku wananchi watakapo amua hakuna polisi, ffu wala jeshi ambalo litawazuia kufanya yale yanayotokea nchi jirani
   
Loading...