Maajabu ya Dunia: Watanzania kushangilia spidi ya kupelekwa kwenye umaskini

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,559
41,077
Siku zote umaskini wa kipato unaanzia kwenye umaskini wa kichwani. Watanzania walio wengi, kutokana na umaskini wa kichwani wanaamini kuwa huruma ya CCM na Serikali, ndivyo vitawajengea mazingira ya wao kuwa na maisha mazuri.

Wakati huko kwenye nchi za watu wenye utajiri wa kichwani, ni wananchi ndio wanaoilazimisha Serikali kuwajengea wananchi mazingira mazuri ya kuyatengeneza maisha yao. Huku kwa mabwege, ni Serikali na CCM ndiyo huwalazimisha wananchi kujenga mazingira mazuri ya watawala ili wao watawala waweze kuneemeka, kuiba na kufisadi bila kusumbuliwa.

Kule Australia, miaka ya huko nyuma, wananchi waliielekeza Serikali kuwa kwa sababu wao wananchi wanawanunulia viongozi wao magari ya kusafiria, mafuta ya magari yao, kugharamia matengenezo ya magari yao; basi pia wananchi wote wanaotumia usafiri wa umma kwenye miji, kwenye usafiri huo, kila mtumiaji atasafiri bure. Mpaka leo ukisafiri na usafiri wa umma mjini, hulipi chochote. Ni taxi tu, ndiyo utalipia.

Ongezeko la nauli za mjini limedhihirisha maisha ya Watanzania yalivyo duni. Hivi ongezeko la sh 100, kwa watu wenye kipato, nalo kweli ni ongezeko la kupigia kelele? Hata kama lingekuwa ongezeko la sh 500, kwa mwenye kipato cha kawaida, ni ongezeko dogo sana. Kwenye bei ya nyama, ongezeko lilikuwa sh 1,000 kwa kilo. Hawa wanaopigia kelele ongezeko la sh 100, kweli huwa wanakula nyama ambayo ongezeko la bei lilikuwa sh 1,000 kwa kilo?

Sasa ndiyo unaweza kuelewa kwa nini kelele zilikuwa nyingi sana kutokana na ongezeko la bei ya mahindi, mchele na maharage. Kwenye nchi hii inaonekana kuna watu wanaishi kwa mateso makali sana, lakini viongozi wao wanatapanya pesa utadhani ni viongozi wa watu matajiri hasa.

Kwa umaskini huu, viongozi wa Serikali walistahili kutumia vitz badala ya v8. Kwa umaskini huu, Rais wa Tanzania hakustahili kuzunguka huko nje na msululu wa watu ambao hakuna chochote cha maana wanachofanya zaidi ya kutalii kwa gharama ya maskini. Pesa ambayo ingeokolewa ingejenga miradi ya uzalishaji itakayoongeza mauzo ya nje.

Nchi hii bila ya kuwa na uzalishaji utakaovuta pesa nje kuleta nchini, au uzalishaji wa ndani utakaopunguza uagizaji wa bidhaa takataka toka China, tutaendelea kuwa waagizaji wa bidhaa toka nje, wauzaji nje wa ajira zetu, na kutengeneza mamilioni ya maskini kila mwaka.

Nchi hii, miaka ya 1970 ilikuwa inatengeneza bidhaa nyingi za ubora wa hali ya juu, leo uwezo wote umepotea, tumebakia kuwa waagizaji wa bidhaa takataka za kutoka China:

Yapo wapi matairi bora kabisa ya General tyre?

Ziko wapi baiskeli nzuri za Swala?

Ziko wapi kanga za ubora wa hali ya juu za Urafiki?

Yako wapi malori ya scania tuliyokuwa tunaunganisha Kibaha?

Yapo wapi matrekta ya Valmet yenye kiwango cha juu cha ubora, tuliyokuwa tunayaunganisha nchini?

Yako wapi mashuka safi na bora ya Mutex?

Viko wapi viatu bora vya ngozi vya Bora Shoes?

Viko wapi vile vyuo vya FTC, vya Arusha Tech, Dar Tech na Mbeya Tech, vilivyokuwa vikizalisha mafundi wenye uwezo wa hali ya juu kwenye fani zote za ufundi ambavyo wahitimu wake walipendelewa zaidi katika ajira kuliko hata graduate wa engineering?

Vyote tumeua, tumeuza ajira kwa wachina, na sisi kugeuka kuwa wachuuzi wa bidhaa hafifu za wachina. Badala ya kwenda mbele, tunarudi nyuma, huku tukipiga kelele kuwa tupo kwenye kasi kubwa, kumbe ni kasi ya mtu anayedondoka toka kwenye mti, lakini yeye kwa kuwa amefumbwa macho, anayemwongoza anamwaminisha kuwa hiyo spidi siyo ya kudondoka bali ya kupaa kwenda juu.

Kama tunafikiri watawala ndio watutengenezee mazingira ya kupata maendeleo, tusahau habari ya maendeleo.

Wakuu wa Serikali wanakazana kujitengenezea mazingira ya kuwafanya wao na vizazi vyao waneemeke milele. Wakati wa utawala wa Kikwete watawala wakajiwekea sheria kuwa Rais mstaafu, spika mstaafu, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu Mstaafu, alipwe 80% ya mshahara wa yule ambaye yupo madarakani. Hivyo mshahara wa yule ambaye yupo madarakani utakavyopanda, na wa yeye mstaafu utapanda.

Magufuli akapitisha sheria kuwa zaidi ya Rais, sasa hata Spika, Jaji Mkuu, Waziri Mkuu na Makamu wa Rais, hata wafanye uovu gani, hakuna kushtakiwa.

Samia naye, ameongeza, na kuhakikisha kuwa hata wenzi wa marais wastaafu, nao walipwe mishahara.

Unaona kabisa jinsi watawala wanavyohangaika na kujibidisha kutengeneza mazingira ya wao kuishi kwa raha mustarehe maisha yao yote, hata wazao wao.

Wabunge nao, mara kadhaa, wamejipigania kuhakikisha wanapata mishahara mizuri, posho nzuri na kiinua mgongo kizuri kila Bunge linapomaliza muda wake.

Kundi moja tu, ndio limebeba wajinga. Wakati wenzao wanapigania kutengeneza maisha yawe bora; lenyewe linataka lipiganiwe na watu wengine kuyafanya maisha yake yawe bora, hilo ni kundi la umma. Tena hili kundi hata kama likiwa kwenye uduni kabisa, likiambiwa kuwa sasa hivi maisha yenu ni mazuri sana, linashangilia kama vile limefikishwa ahera, wakati linayashuhudia maisha yake yalivyo duni. Ni kundi kipofu, halioni, halitafakari, halichukui hatua; ni kundi la kuambiwa na kuswagwa. Kumdi hili kama haliyajiondoa lenyewe kwenye uduni wa kichwani litaendelea kudidimia milele.

Ni sauti ya kuwaambia wale walalamikaji, ubora wa maisha yao upo mikononi mwao, na ni jukumu lao.
 
Kama Nchi endapo hatutachuklua hatua na kuiambia ccm sasa basi, itatupeleka shimoni na kutufukia!
Uovu unazidi kuwa mkubwa kila uchwao!
Ndani ya CCM, wapo wasindikizaji. Lakini wapo wale ambao kila siku wanahangaika na kuwaza kwa kina namna watakavyohakikisha CCM inaendelea kutumika kuwahakikishia wao wenyewe na wana wao na wana wa wana wao wanaendelea kuwa na maisha ya uhakika, maisha ya starehe, anasa na utajiri.

Pembeni, nje ya mfumo, wapo akina Mwashambwa ambao wanoabweka kwa bidii kushangilia ili angaloa watupiwe hata makombo.
 
Bandiko zuri sana Seema nini Sasa hv humu siku hzi Kuna mabumunda wengi mno mfno kijana mmoja anaitwa Lucas mwashambwa

Ni mpiga pambio mzuri san kial kitu anasifia
Hawa akina Mwashambwa ni wa kuonewa huruma sana. Maana ni wasindikizaji tu. Wakikumbukwa sana, wanarushiwa mifupa ili angalao wapate nguvu za kuendelea kushangilia.
 
Kwa Sasa wajinga wamezidi kuongezeka nchi hii, na uoga umeshikwa Kasi, huku utaratibu mpya wa chawa ukizidi kushamiri. Na kwa kuwa wananchi wanazidi kuwa waoga, serekali inapika data za maendeleo, lakini uhalisia wa maisha unakataa. Cha ajabu viongozi ndio wanazidi kuneemeka katika umasikini huu. Machafuko tu ama mapinduzi ya kijeshi ndio yatarejesha mifumo sahihi, na serekali kuwajibika.
 
Naikumbuka miaka ile ambapo hata vijana wanafunzi tu wa pale UDSM, wakisema wanakutana Nkrumah Hall kujadili maslahi ya Taifa, Serikali yote ilitetemeka na kuanza kujihami. Siku hizi vijana wenyewe ndiyo hawa wanaouonea fahari uchawa.
 
018100094042.JPG
 
Umeongea kwa uchungu ambao wengi tunao pia, adui ya mwafrika ni viongozi wenye madaraka ya juu
Hata wao wanaogopana sana ndio maana wanapitisha sheria za kuwalinda watangulizi wao na wake zao na watoto wao na hata mali zao, kwa sababu wanapigwa mikwara na kuelekezwa wafanye nini

Wenzetu wanaendelea kwa sababu wananchi wana nguvu na systems zao na sheria ziko imara na hazivunjwi kipumbavu kisa mimi nina cheo fulani

Bora nahangaika nje na maisha yangu but I'm well off
 
Siku zote umaskini wa kipato unaanzia kwenye umaskini wa kichwani. Watanzania walio wengi, kutokana na umaskini wa kichwani wanaamini kuwa huruma ya CCM na Serikali, ndivyo vitawajengea mazingira ya wao kuwa na maisha mazuri.

Wakati huko kwenye nchi za watu wenye utajiri wa kichwani, ni wananchi ndio wanaoilazimisha Serikali kuwajengea wananchi mazingira mazuri ya kuyatengeneza maisha yao. Huku kwa mabwege, ni Serikali na CCM ndiyo huwalazimisha wananchi kujenga mazingira mazuri ya watawala ili wao watawala waweze kuneemeka, kuiba na kufisadi bila kusumbuliwa.

Kule Australia, miaka ya huko nyuma, wananchi waliielekeza Serikali kuwa kwa sababu wao wananchi wanawanunulia viongozi wao magari ya kusafiria, mafuta ya magari yao, kugharamia matengenezo ya magari yao; basi pia wananchi wote wanaotumia usafiri wa umma kwenye miji, kwenye usafiri huo, kila mtumiaji atasafiri bure. Mpaka leo ukisafiri na usafiri wa umma mjini, hulipi chochote. Ni taxi tu, ndiyo utalipia.

Ongezeko la nauli za mjini limedhihirisha maisha ya Watanzania yalivyo duni. Hivi ongezeko la sh 100, kwa watu wenye kipato, nalo kweli ni ongezeko la kupigia kelele? Hata kama lingekuwa ongezeko la sh 500, kwa mwenye kipato cha kawaida, ni ongezeko dogo sana. Kwenye bei ya nyama, ongezeko lilikuwa sh 1,000 kwa kilo. Hawa wanaopigia kelele ongezeko la sh 100, kweli huwa wanakula nyama ambayo ongezeko la bei lilikuwa sh 1,000 kwa kilo?

Sasa ndiyo unaweza kuelewa kwa nini kelele zilikuwa nyingi sana kutokana na ongezeko la bei ya mahindi, mchele na maharage. Kwenye nchi hii inaonekana kuna watu wanaishi kwa mateso makali sana, lakini viongozi wao wanatapanya pesa utadhani ni viongozi wa watu matajiri hasa.

Kwa umaskini huu, viongozi wa Serikali walistahili kutumia vitz badala ya v8. Kwa umaskini huu, Rais wa Tanzania hakustahili kuzunguka huko nje na msululu wa watu ambao hakuna chochote cha maana wanachofanya zaidi ya kutalii kwa gharama ya maskini. Pesa ambayo ingeokolewa ingejenga miradi ya uzalishaji itakayoongeza mauzo ya nje.

Nchi hii bila ya kuwa na uzalishaji utakaovuta pesa nje kuleta nchini, au uzalishaji wa ndani utakaopunguza uagizaji wa bidhaa takataka toka China, tutaendelea kuwa waagizaji wa bidhaa toka nje, wauzaji nje wa ajira zetu, na kutengeneza mamilioni ya maskini kila mwaka.

Nchi hii, miaka ya 1970 ilikuwa inatengeneza bidhaa nyingi za ubora wa hali ya juu, leo uwezo wote umepotea, tumebakia kuwa waagizaji wa bidhaa takataka za kutoka China:

Yapo wapi matairi bora kabisa ya General tyre?

Ziko wapi baiskeli nzuri za Swala?

Ziko wapi kanga za ubora wa hali ya juu za Urafiki?

Yako wapi malori ya scania tuliyokuwa tunaunganisha Kibaha?

Yapo wapi matrekta ya Valmet yenye kiwango cha juu cha ubora, tuliyokuwa tunayaunganisha nchini?

Yako wapi mashuka safi na bora ya Mutex?

Viko wapi viatu bora vya ngozi vya Bora Shoes?

Viko wapi vile vyuo vya FTC, vya Arusha Tech, Dar Tech na Mbeya Tech, vilivyokuwa vikizalisha mafundi wenye uwezo wa hali ya juu kwenye fani zote za ufundi ambavyo wahitimu wake walipendelewa zaidi katika ajira kuliko hata graduate wa engineering?

Vyote tumeua, tumeuza ajira kwa wachina, na sisi kugeuka kuwa wachuuzi wa bidhaa hafifu za wachina. Badala ya kwenda mbele, tunarudi nyuma, huku tukipiga kelele kuwa tupo kwenye kasi kubwa, kumbe ni kasi ya mtu anayedondoka toka kwenye mti, lakini yeye kwa kuwa amefumbwa macho, anayemwongoza anamwaminisha kuwa hiyo spidi siyo ya kudondoka bali ya kupaa kwenda juu.

Kama tunafikiri watawala ndio watutengenezee mazingira ya kupata maendeleo, tusahau habari ya maendeleo.

Wakuu wa Serikali wanakazana kujitengenezea mazingira ya kuwafanya wao na vizazi vyao waneemeke milele. Wakati wa utawala wa Kikwete watawala wakajiwekea sheria kuwa Rais mstaafu, spika mstaafu, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu Mstaafu, alipwe 80% ya mshahara wa yule ambaye yupo madarakani. Hivyo mshahara wa yule ambaye yupo madarakani utakavyopanda, na wa yeye mstaafu utapanda.

Magufuli akapitisha sheria kuwa zaidi ya Rais, sasa hata Spika, Jaji Mkuu, Waziri Mkuu na Makamu wa Rais, hata wafanye uovu gani, hakuna kushtakiwa.

Samia naye, ameongeza, na kuhakikisha kuwa hata wenzi wa marais wastaafu, nao walipwe mishahara.

Unaona kabisa jinsi watawala wanavyohangaika na kujibidisha kutengeneza mazingira ya wao kuishi kwa raha mustarehe maisha yao yote, hata wazao wao.

Wabunge nao, mara kadhaa, wamejipigania kuhakikisha wanapata mishahara mizuri, posho nzuri na kiinua mgongo kizuri kila Bunge linapomaliza muda wake.

Kundi moja tu, ndio limebeba wajinga. Wakati wenzao wanapigania kutengeneza maisha yawe bora; lenyewe linataka lipiganiwe na watu wengine kuyafanya maisha yake yawe bora, hilo ni kundi la umma. Tena hili kundi hata kama likiwa kwenye uduni kabisa, likiambiwa kuwa sasa hivi maisha yenu ni mazuri sana, linashangilia kama vile limefikishwa ahera, wakati linayashuhudia maisha yake yalivyo duni. Ni kundi kipofu, halioni, halitafakari, halichukui hatua; ni kundi la kuambiwa na kuswagwa. Kumdi hili kama haliyajiondoa lenyewe kwenye uduni wa kichwani litaendelea kudidimia milele.

Ni sauti ya kuwaambia wale walalamikaji, ubora wa maisha yao upo mikononi mwao, na ni jukumu lao.

Hongera sana mkuu umeandika Jambo la msingi Sana. Narudia Hongera Sana na uedelee kutuelimisha zaidi kwa Hekima zako.
 
The mighty Sahara is well endowed with sand, naturally found all over. If it were to have necome 'communist' in those brighter years, the joke has it that shortages of sand were to follow suit. But then with passage of time and due shift in geo-political forces, liberalization of the sand based economy befitting market economics in modelling would have seen whatever remaning sand being exported to China. With no more sand, Sahara no more! Void?
 
Mtu akisoma ulichoandika anaweza Dhani unatumia akili ya kuku.

Hoja Yako ni dhaifu sana.

Wewe maandiko yako humu yanafahamika. Na wenye uwezo wa kitafakari wanajua wewe ni mtu wa namna gani.

Bahati mbaya kwako ni kwamba andiko hili ni kwaajili ya watu ambao ni mentally fit na ambao wana upeo mpana wa kuelewa misingi ya maendeleo. Siyo wale ambao wakivaa shati zuri la kupewa, au akavaa kubasi baada ya kufanya kibarua, anaona kuwa ameendelea. Wewe huhitajiki kwenye mada hizi zinazohitaji upeo na uelewa mpana.
 
Huna hoja,huwezi kuja na ujinga hapa wa kudai kwamba huko mlikotoka mlikuwa na welfare nzuri wakati mlikuwa mnavaa viraka,usafiri tabu,,chakula tabu Kila kitu tabu.

Haya ndio madhala ya Utapiamlo uliokithiri 😁😁
 
Back
Top Bottom