Ombi langu kwa CCM ni waonee huruma Wananchi kwa kuchagua viongozi waadilifu

RNA

JF-Expert Member
Mar 27, 2013
1,584
2,683
Habari wana JF,

Binafsi sijawahi kuwa Mwanachama wa CCM na ni ukweli usipingika kwa Hiki Chama kutoka madarakani itakuwa Ngumu sana sana kuliko tunavyofikiri

Sasa hivi kwa hali ilivyo sio rafiki sana kama ilivyo kwa tawala zilizopita za CCM pesa zetu zinapotea sana na raslimali zetu zinapotea. Yaani kikubwa tunachofurahia sasa ni Uhuru wa kijamii huku mambo mengine yakiwa magumu sana

Kibaya zaidi ni kwamba wananchi wa chini ndio tunakamuliwa sana kupitia Kodi, Tozo pamoja na kupanda kwa Ugumu wa Maisha .

Kwa kifupi inaumiza sana kuhimizwa kutoa kodi na Tozo kisha mtu au kikundi cha Watu kujinufaisha pesa zetu .

OMBI LANGU:- Muonee huruma wananchi na Nchi kwa ujumla kwa kukubali kuachia Madaraka au Kwa maslahi mapana ya Taifa mbadilike na kuwa wazalendo mtuletee viongozi waadilifu na wachapakazi sio hawa wasio na mchango kwa Taifa zaidi kutafuta umaarufu wa kisiasa na kujinufaisha Wao .

Ntashukuru kama Ombi langu litachukuliwa kwa Mtazamo Chanya Maana mmetawala kwa Muda mrefu Sana hatuoni matunda yanayoendana na raslimali tulizo nazo .
 
Wakija viongozi wanafuata sheria na waadilifu mnasema wanawabana wakija viongozi waadilifu na wanawapa uhuru mnasema wanawatoza sasa sijui mnahitaji nini watanzania.
Viongozi waliopo madarakani na waliostaafu wajitathmini kama kweli wamekuwa waadilifu na wanafanya yale yanayompendeza Mungu !! Ukiona watu wanaomba waonewe huruma ujue soon Mungu ataingilia kati !! KARMA !!!
 
Mungu alishaingilia kati kutuondolea yule kichaa Mrundi aliyewatala Watanzania kwa mkono wa chuma.
 
Mimi naamin watanzania tumelaaniwa tena na Aka kanyerere, kuna mengi sana unfairly tunafanyiwa lakini tuko kimya tu. Aya ni matokeo ya kurogwa na kulaaniwa.

Uyu mwigulu mshamba kabisa wa uko iramba ati akadai tozo tutalipa kama hatutaki tuamie Burundi, uyu mama akawaruhusu viongozi wake wale kwa urefu wa kamba zao, uyu tena mama katiri akawapa dili wamiliki wa vituo vya mafuta na matajiri kujenga vituo lukuki vya mafuta ili watupige lkn sie tuko kimya tu kama mapoyoyo.
Tu
Nakuomba Mungu maisha yetu yawe magumu sana labda tutaamka, unga ufike elf4, mafuta elf5 uko we shall wake up na kufight for our rights
 
Hahahaa maombi mabaya sans
 
Back
Top Bottom