Namini kuwa waasisi wa TANU na ASP nimewataja na pia viongozi wa kiserikali wa mwanzo pia ikiwa Baraza la mawaziri kwa upande wa Tanganyika na Baraza la Mapinduzi kwa upande wa Zanzibar. Lazima tukubali kuwa Tanzania imejengwa ama imekuwa shaped na mawazo ya waliokuwepo katika TANU na ASP na uhuru wa Tanganyika na Mapinduzi ya Zanzibar ni matukio makubwa ya kihistoria ambayo yana nafasi ya kipekee katika kujenga kitu kinachoitwa taifa la Tanzania.