Viongozi waasisi wa Tanzania - Tanganyika na Zanzibar

omarilyas

JF-Expert Member
Jan 24, 2007
2,130
145
Ndugu wanajamii,

Kwa muda mrefu nimekuwa nikisikia hili neno la waasisi wetu. Kwa kweli naamini kwa wengi wetu maana halisi ya waasisi wetu bado ni suala tata. Kwa muono wangu ni kuwa kuna waasisi na viongozi waasisi. Kutambua waasisi ni zoezi kubwa mno lakini naamini kwa manufa ya kimfumo ni bora tukawatambua waasisi wa vyama vyetu vikuu vya ukombozi na viongozi wa serikali za mwanzo wakati tukiwa tumepata uhuru kwa upande wa Tanganyika na Mapinduzi kwa upande wa Zanzibar kama waasisi wa Taifa letu la Tanzania. hapa naambatanisha majina yao kama ambavyo nimeweza kuyakusanya.

nakaribisha mjadala...

VIONGOZI WAASISI WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR
Waasisi wa TANU:
Julius Nyerere, Geremano Pacha, Joseph Kimalando, Japhet Kirilo, C. O Milinga, Abubakar Ilanga, L.B Makaranga, Saadani Kandoro, Suleiman Kitwara, Kisung’uta Gabara, Tewa Said Tewa, Dossa Aziz, Abdul Sykes, Patrick Kunambi, Joseph Kasela Bantu, Ally Sykes, John Rupia

Waasisi wa ASP
African Association:
Abeid Karume, Mtoro Rehani, Ibrahim Saadala, Mtumwa Borafia, Bakari Jabu, Rajab Swedi, Saleh Juma, Abdula Kassim Hanga Shirazi Association: Thabit Kombo, Muhidin Ali Omar, Ali Ameir, Ameir Tajo, Ali Khamis, Mdungi Usi, Haji Khatibu, Othman Sharif, Ali Juma Seif, Mzee Salehe Mapete

Baraza la Kwanza la Mawaziri Tanganyika
Amir Jamal, Rashid Kawawa, Oscar Kambona, Paul Bomani, Abdallah Fundikira, George Kahama, Bhoke Mnanka, Job Lusinde, E Brayson

Baraza la Mapinduzi Zanzibar
Seif Bakari, Khamisi Daruweshi, Abdulla Said Natepe, Edington Kisasi, Hassan Nassor Moyo, Hasnu Makame, Ahmed Ameir, Abdulaziz Twala, Idris Abdulwakil, Khamis Hemed, Yussuf Himid, Pili Khamisi, Ali Mahfoudh, Abood Jumbe, Abdulrahman Babu, Said Issa Bavuai, Ramadhani Haji Faki, Abdulla Khamis Ameir, Ibrahim Makungu, Saleh Sadalla Akida, Ali Sultan Issa, Hafidh Suleiman, Mohamed Mfaume, Ibrahim Amani, Mohamed Abdula Kaujore, Rashid Abdula, Muhsin Bin Ali, Daud Mahmoud.

NB: Majina niliyoweka "bold" naamini ndio walio hai hadi leo hii. Kama kuna mapungufu ama makosa naomba samahani
 
Namini kuwa waasisi wa TANU na ASP nimewataja na pia viongozi wa kiserikali wa mwanzo pia ikiwa Baraza la mawaziri kwa upande wa Tanganyika na Baraza la Mapinduzi kwa upande wa Zanzibar. Lazima tukubali kuwa Tanzania imejengwa ama imekuwa shaped na mawazo ya waliokuwepo katika TANU na ASP na uhuru wa Tanganyika na Mapinduzi ya Zanzibar ni matukio makubwa ya kihistoria ambayo yana nafasi ya kipekee katika kujenga kitu kinachoitwa taifa la Tanzania.
 
Zanzibar ilipata uhuru sawa na Tanganyika hakuna tofauti yoyote kwenye suala la uhuru.

Nadharia ya kutuonesha kama Mapinduzi na ASP ndio uasisi, utakuwa unalo unalokusudia kutonesha hapo.Na ndio maana nikasema hiyo heading hailengi ukweli wa mambo.Hao ni waasisi wa vyama vya siasa, ASP kilikuwa ni chama kimoja sawa na vyama vyengine huko Zanzibar.Hakikuwa na tofauti yoyote kisiasa ya kusema viongozi wa ASP, ndio waasisi wa Zanzibar.

Kufanya hivyo ni kupotosha malengo ya wasomaji, si kweli kama Mapinduzi yamejenga Zanzibar!Ukiniuliza mie nitakwambia yamebomoa zaidi, na hadi leo jinamizi la Mapinduzi linaendelea kuvitafuna visiwa hivyo na wala haliwezi kuviacha ...hadi viongozi wakiri na kuomba radhi wale waliondokewa na wapenzi wao kwenye tukio hilo la Mapinduzi.

Nawakilisha...
 
Namini kuwa waasisi wa TANU na ASP nimewataja na pia viongozi wa kiserikali wa mwanzo pia ikiwa Baraza la mawaziri kwa upande wa Tanganyika na Baraza la Mapinduzi kwa upande wa Zanzibar. Lazima tukubali kuwa Tanzania imejengwa ama imekuwa shaped na mawazo ya waliokuwepo katika TANU na ASP na uhuru wa Tanganyika na Mapinduzi ya Zanzibar ni matukio makubwa ya kihistoria ambayo yana nafasi ya kipekee katika kujenga kitu kinachoitwa taifa la Tanzania.

Kwa upande wa Zanzibar Historia ina watu wengi waliopigania uhuru (kama huko ndiko kuasisi) ambao wewe hukuwaorodhesha.
Nikosa kufikiri eti ASP tu ndio walikuwa wanaikombowa Zanzibar na wale wa upinzani eti sio.
 
Ndio maana nikatumia neno VIONGOZI WAASISI nikiwa na maana wale ambao walikuwa na majukumu ya kushape Tanzania ya sasa , Tanganyika na Zanzibar.

Kuhus Uhuru wa Zanzbar mwaka 1963 mimi sina tatizo nao lakini siamini kuwa uliweza KUASISI Zanzibar ya sasa. Lakini pia sio kweli kuwa ambao hawakuwa ASP hawakuwa na nafasi ya kuasisi Zanzibar kwani ukiangalia Mapinduzi yalifanywa na watu kutoka ASP, UMMA Party na wengineo ambao hawakuwepo katika vyama. Wapo hata waliokuwa ZNP lakini walishiriki kwa njia moja ama nyingine kama sio wakati wa mapinduzi basi baada ya mapinduzi. Ndio maana baraza la mapinduzi halikuwa na watu wa ASP tu. NA kama ni ASP lakini pia walikuwepo watu ambao mwanzoni walikuwa upande tofauti wa ASP lakini wakaja kujumuika pamoja kujenga Zanzibar ya KIMAPINDUZI ambayo yawezekana kabisa ilikuwa tofauti na ile Zanzibar njema kwa wote ambayo mapinduzi yalidhamiria kuijenga.
 
Kuhus Uhuru wa Zanzbar mwaka 1963 mimi sina tatizo nao lakini siamini kuwa uliweza KUASISI Zanzibar ya sasa.
Sasa kama uhuru huo unaosema haukuasisi, Ni vipi hayo Mapinduzi (ambayo yanaasisi Zanzibar ya leo) yangepatikana?

Huu ndio upotoshaji ambao nilianza kuugundua mwanzoni :rolleyes:
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom