Viongozi wa Yanga mwacheni Azizi Ki aende tu

ngara23

JF-Expert Member
Aug 31, 2019
2,944
6,595
Nawashauri viongozi wa Yanga, msiwe na pressure kutoka Kwa mashabiki wasiojua mpira mkaingia kwenye mtego wa kumpa Aziz ki pesa ndefu takriban 1.3 billion, mtakuwa mmejichanganya.

Azizi ki Kwa Sasa ana miaka 29 kwenye mpira umri huo jua limezama, unaweza kumbakiza kumbe ndo amefika kwenye peak/ kilele cha career yake.

Nawasihi Yanga muwe na msimamo wa kiwango cha mshahara na utamaduni wenu.

Ukimwongeza Azizi pesa ya usajili na mshahara wa million 80 Kwa mwezi, kila mchezaji akimaliza mkataba atataka alipwe kama Aziz, Ambapo itakuwa gharama kuendesha team.

Africa Kuna vipaji vingi zaidi ya Aziz na vinataka pesa ndefu.

Hakuna mchezaji asiyeizwa au kuachwa akiingia tofauti na uchumi wa club.

Man u walimuuza Ronaldo, Barcelona walimuuza Mesi, arsenal walimuuza Henry na van persie n.k na Bado team zilikomaa na utamaduni wao wakafanya vyema.

Ukimwongeza Azizi ki mkataba wa pacome, yao, mdathir, aucho, max, bacca, job illkiisha watataka mabilion kama ya Aziz.

Wasalam
 
Kipaji anacho tusimbeze.
Kama atapata maslahi mazuri, viongozi waachane nae.
Wamlete Chama ambae hana bei kali anaweza kukaribia Aziz ki kipindi wanajipanga
Chama tena? Mpira wa Gamondi kila mtu ni mkabaji, mpira wa Gamondi kila mtu anatakiwa awe mwana riadha. Kama viongozi watafosi kumsajili Chama basi wajue kuwa wanamsajilia Gamondi mchezaji wa kumuweka benchi. Chama kwasasa kabakiza akili tu mpira ila umri ndio unaomkataa kwasasa hivyo kuna vitu vingi hawezi kufanya kwasasa. Nadhani uongozi wa Yanga warudi tena kiwandani wakachukue mashine nyingine. Kile kiwanda kinazalisha vifaa kila msimu, anatoka mtu anakuja mtu, Asec ni chuo cha kuzalisha mafundi wa mpira Africa.
 
B 1.3
Project yake na yanga Bado haijaisha
Si

Nimeheshimu mawazo yako mkuu.
Umenena jambo la maana mno
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom