ndenjii handsome
JF-Expert Member
- Apr 27, 2021
- 647
- 704
- Thread starter
- #21
Siasa tamunyumba-serikali.
chakula-serikali.
umeme-serikali.
maji-serikali.
usafiri wa kifahari na gharama zake-serikali
matibabu-serikali
starehe-serikali
walioweka haya walikuwa na nia nzuri sana ili kiongozi atulize akili katikakutatua changmotl tu,ila hawa panya wanaona ni kama watu waliobarikiwa kula mpaka wanajiongezea nyingine bila uoga.
Kati ya vitu ninavyoshindwa kuelewa ni kama hili suala.
Naombeni kwanza mniambie mimi mwananchi wetu sehem gani au ni mkoa gani ambao mmejitenga wenyewe
Maana haiwezekani wananchi wenu gharama ya maisha inapanda kiasi hiki alafu mnakuja mnajitokeza mnatoa majibu mepesi kwa vitu ambavyo vinawagharimu wananchi wenu,
Ina maana kama msoto huu unaoendelea hapa nchini tungekuwa tunakula wote, na kuishi wote mngejua namna ya kumsaidia mwananchi wenu,
Vitu vinapanda ovyo ovyo alafu anajitokeza kamtu kamoja kanaanza kusema, uchumi umeyumba kwenye nchi za wenzetu ndio maana haya yanatokea, hivi akili zenu zipo sawa.
Mara paah miujiza ya Mungu hiyoo Tanzania imehamia Jupiter au Mars na mpo wenyewe huko yaani watz tu sayari nzima hakuna nchi jirani wala misaada ya wahisani, Mngechukua hatua gani kuongoza nchi yenu?
Kiufupi hamtendi haki kazi kupeana vyeo ambavyo hata sioni vinamsaidia nini mwananchi ambaye saizi analia na mbolea, analia na mafuta,
Mnashindwa hata kuiga mifano nchi za wenzetu, kazi tu miradi ya kimkakati, mwananchi hoi nyie mpo tu
Mkuu viongozi hawaishi maisha yetu. Hawajui na wala hawawezi kujua struggle zetu.
Nyumba bure, usafiri bure, umeme, maji, simu, internet, houseboy, housegirl, hata wakipumua wanalipwa posho ya usumbufu....