Viongozi wa Simba ndio tatizo la kwanza kwenye klabu, wajitathimini wao kwanza kabla ya kuwatoa kafara wengine!

Majok majok

JF-Expert Member
Aug 3, 2023
618
1,570
Viongozi wa Simba na mwekezaji wake ni watu wa propaganda nyingi sana na wamekuwa wakiishi hivyo kwa mda mrefu walicheza na akili za wanachama wao!

Jambo hili limekuwepo kwa mda mrefu na ilikuwa ni suala la muda tu ufike waumbuke, awa wakina Try again, mangungu, Mo mwenyewe, wamekuwa ni watu wa kupiga uongo uongo mwingi kiutendaji lakini uhalisia wa kile wanachokuwa wanakiongea imekuwa ni zero kabisa!

Bahati mbaya sana ata wanachama wao wamekuwa wakiwaamini hasa hasa wale wanatoka kwenye matawi yanayokuwa na maslai na awa viongozi uwa awataki ata shabiki yoyote aiongelee vibaya Simba, wao uwa wanataka waisifie na kuiabudu tu ata Kama inatumbukia shimoni!

Simba ilishaonyeaha dalili mbaya mda mrefu lakini watu walishupaza shingo, kuanzia kwenye usajili walioufanya awakuwa serious Kuna watu walipiga pesa pale, Simba walisajili majina ya wachezaji na sio wachezaji, unasajili wachezaji kufurahisha genge na sio kiufundi unadhani unaweza kutoboa?

Angalia wachezaji Kama kina Saido, chama, Ngoma, umri wao umekwenda Awana jipya Tena la kupigania kwenye soka ni ngumu kukimbizana na vijana wenye energy kubwa uwanjani na hao ndio tegemezi kwenye kiungo.

Angalia usajili wa Miksoni ulikuwa ni usajili wa ovyo sana ule, umeshasajili kramo, unae Kibu, unae ulikuwa nae Banda, Sako, wote hao walikuwa wanacheza eneo moja, lakini unaenda kuongeza bonge miksoni ambae alishabaki jina tu eti aje aongeze kitu kwenye timu?

Timu inajinasibu kwenda kukaa airport kusubiria wachezaji wanaoshuka kwenye ndege ili iwaibe Ina maana ya kwamba ni timu inayoendeshwa kihuni sana hawana scout na wala viongozi wake hawajitambui matokeo yake ndio yale ya kufanya usajili wa mihemko mnakuja kupigwa tano!

Kama ni kufukuzwa waanze kina Mo, try again, Mangungu kabla hawajawagusa wengine, Mwekezaji amekuwa na porojo nyingi sana kwenye uwekezaji wake, alishapewa masharti ya kufata ili mchakato uendelee wa mabadiliko baada ya kugundulika alifanya ujanja ujanja mwingi kwenye hatua za kupewa timu lakini amebaki kulaumu na kupiga propaganda uchwara!

Wachezaji wanaangushiwa jumba bovu kwamba wameuza mechi wakati Kila kitu kilikuwa kinaonekana hadharani, siku nyingi tulikuwa tukisema Simba haiko sawa ni unga sana ikikutana na timu yenye quality na umakini Italia kilio Cha mbwa tulikuwa tunabezwa. Sasa imeadhibiwa lawama wanapewa wachezaji!
Tatizo la Simba linaanzia kwa viongozi hata wakimleta Guadiola hawezi toboa kwa viongozi awa wajanja wajanja!
 
Tatizo la simba ni kuanzia.
1. Muwekezaji.
2. Mwenyekiti mangungu.
3.Try again.
4. Body ya wakurugenzi
5. Management.
6.Benchi la ufundi lote.
7. Scout analyst,nk
8. wadau.
9. Washauri wa Bodi.
10 mashabiki mbumbumbu
Akitolewa chama wanalia na kuzomea pmf sana, wanamlilia miquisson kurejeshwa, Adebagor na manzoki
 
Tatizo la simba ni kuanzia.
1. Muwekezaji.
2. Mwenyekiti mangungu.
3.Try again.
4. Body ya wakurugenzi
5. Management.
6.Benchi la ufundi lote.
7. Scout analyst,nk
8. wadau.
9. Washauri wa Bodi.
10 mashabiki mbumbumbu
Akitolewa chama wanalia na kuzomea pmf sana, wanamlilia miquisson kurejeshwa, Adebagor na manzoki
Naliunga mkono💯..Hata tumlete mourinho bado hakutakuwa na nukta ya mabadiliko.
Tukianzia hapo namba 1 ndiyo tatizo kuu..Wameifanya timu kama ya familia toka enzi za kina azim dewji,huyu wa sasa naye Sanaa nyingi,toka alipotuletea yule Betina wake Barbra mtu asiyejua mpira awe bosi nilishangaa Sana njaa hizi,kumbe anamtengenezea ulaji FIFA..
Timu ya wasichana kampatia Dada yake.Anatumia njaa za hao kenge wengine kufanya mambo yake..
Nini maana ya "Nguvu moja!?"
Yanga nawapongeza Sana Sana,ukweli usemwe mko vizuri kuanzia wadhamini hadi uongozi...
Mimi siyo mbaguzi wa rangi Ila hakuna wala haijawahi tokea mhindi akafadhili timu bila kujali maslahi ...
 
Shida yote hii ni baada ya kufungwa na Yanga! Mbona sisi wenzenu tumefungwa na Ihefu lakini tumetulia? Mashabiki wa simba acheni umbumbumbu.

Simba ni timu kama zilivyo timu nyingine za mpira wa miguu. Hivuo kufungwa, kutoa sare na kushinda ni sehemu ya mchezo.
 
Afadhali Sasa mmeanza kutambua utapeli wa mwekezaji na viongozi anaowaweka, unaye Banda, Sakho hauwapi nafasi halafu unasema viwango vimeshuka, inasajili Onana hivi Peter Banda angekuwa anapewa nafasi Kama Onana leo ingekuwaje.
Wamemwacha Kakolanya ili wasajili kipa wa nje lakini Kipa anakuja anakaa benchi.
Unakaa na wachezaji Kama Boko, Saidoo halafu unajigamba unataka kuchukua ubingwa was Afrika.
 
Back
Top Bottom