Kuna kila sababu ya kuwa wazi kwa kuacha unafiki juu ya Imani ya kiislam ili ijulikane uislam ni upi na unaishia wapi ambapo ugaidi unaanza. Katiba ya nchi imetoa uhuru wa kuabudu lakini sheria zisivunjwe. Kama kuna imani inahubiriwa na watu kutoka Tz na hata uarabuni ya kuua wasio waislam, ninaitaka serikali itamke ni wakati gani inastahili kuchukua hatua dhidi ya watu kama hawa ambao bila kujali kweli mungu wao anataka hivyo au ni tafsiri zao, kwamba wachukuliwe hatua za kuvunja sheria?
Ni hatua gani zimechukuliwa kwa wanaoua na kuchoma makanisa kule bukoba? Au kwa kuwa wanahujumiwa ni wakristo Serikali inaona sawa tu? Kama serikali haitawalinda wasiokuwa waislam, itangaze ili watafute ulinzi wako binafsi.
Ninaamini kwenye waislam kuna wenye busara na uelewa ingawa ni dhahiri shida ipo. Ninapendekezwa badala ya Pinda kufanya unafiki kwa ajili ya kura zao kinyume cha sheria, kufanyike utaratibu maalumu wa kutoa elimu kwa viongozi wa hili kundi la wenzetu ambalo halitaki hata shule. Elimu hiyo wafundishwe umuhimu wa kuheshimu katiba ya nchi ambayo iko juu ya dini zote.
Lakin pia iundwe sheria kali inayolazimisha (kwa nguvu) watu wote waende shule hata kama hawataki ili taifa liwe linaongea lugha moja. Itakuwa ni shida kuwa na kundi la watu hawataki kusoma elimu ya kawaida, halafu wanachokisoma wanakijua wao na kinahamasisha chuki na machafuko katika jamii, halfu viongozi wanabaki kuwachekea wakijikomba ili wapewe kura, na mwisho wa siku tuwe na taifa lenye vurugu kwa sababu ya kundi moja lisilo na ustaarabu wa kuheshimu kanuni na sheria, lisilotawalika linalonuia kuua watu wengine wasiofanana nalo.
Sambamba na hilo, kunahitajika juhudi kubwa za kuwapa elimu viongozi wa kiislam ili pia waache kukubali kudanganywa na watawala dharimu. Watambue lipi linawezekana na lilpo halilwezekani na wahoji ahadi wanazopewa kwa minajiri ya rushwa. Hii itawasaidia kuishi kwenye uhalisia badala ya kuweka matumaini yao kwenye masuala yasioyowezekana, wanaend up kuwa heart broken pale yanaposhindikana.
Mfano, hakuna chama chochote kitakachoamua kuandka katiba yenye mahakama ya kadhi kwa sababu katiba ya nchi ni ya watanzania wote na wala si ya chama cha siasa kimoja wala kundi la waislam wachache wanaoona watapata manufaa kwa kuandika katiba yenye misingi ya kiislam. Waikatae ccm kwa sababu ya ulaghai, kukosa nia ya kuleta maendeleo kwa taifa na kuishia kuwagawa watanzania na pia kuwafanya Waislam wajinga. Waikatae katiba pendekezwa kwa sababu imeshamirisha ufisadi, imehalalisha rushwa na imesimika udictator na hivo kuhatarisha ustawi wa Watanzania na nchi yao. LAKINI WASIWAZE KWAMBA KUNA MTAWALA ATAASILIMISHA NCHI KWA SABABU YEYE KATAKA.
Tukijenga misingi ya kuambizana ukweli, kushirkishana kwa lazima kwenye suala la maendeleo ikiweom elimu na uzalishaji, tukaweka utaifa wetu mbele, na kuacha majungu hila na ubinafsi, ninaimani tutafika kwenye Tanzania tuikayo.