Viongozi wa Serikali za mitaa wa viti maalum jitathimini kama mnastahili

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,682
1,110
Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya 1977 ambayo ndiyo inayo tumika mpaka sasa imesema, serikali itapata madaraka na mamlaka yake toka kwa wananchi, na msingi mkuu wa serikali ni ustawi kwa wananchi.

Tarehe 24/11 kulikuwa na uchaguzi wa serikali wa viongozi wa serikali za mitaa, uchaguzi uliojaa dosari nyingi na ubabe wa kidola na kusababisha vyama pinzani kujitoa kwenye mchakato mzima wa uchaguzi.

Pamoja na kujitoa na mazingira tatanishi yaliyo sababishwa na serikali yenyewe kwa idara zake kuwa sehemu ya kuhodhi uchaguzi, bado katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano ilikanyagwa makusudi kukibeba chama dola kushinda ushindi wa mezani. Hali inayoleta athari nchini kwa kuwa washindi wa kura za maoni ndani ya CCM ndiyo wateuliwa kwa nafasi za uongozi ambazo mamlaka ya kuwachagua ipo ndani ya wananchi bila kujali vyama vyao.

Kwa maana hiyo, uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa (TAMISEMI) umekiukwa kwa zaidi ya asilimia 95%,kwa kuwa kanuni za uchaguzi huo zimekuwa na nguvu kuliko matakwa ya katiba.

Katiba imetoa haki ya wananchi kuchagua au kuchaguliwa kuwa viongozi na wananchi, lakini pia mamlaka yanayoipa madaraka serikali yapo kwa wananchi pia, kwa kanuni hizo za wagombea kupita bila kupingwa tutegemee migongano na wananchi kama ilivyotokea huko Kyela.

Serikali imepora mamlaka ya wananchi ya kuchagua viongozi wao, wametengeneza kanuni zenye nguvu ya kuimeza sheria mama na kuifanya katiba ni kitabu cha hadithi za kusadikika,athari yake ni kubwa kwa jamii kwa kuwa waliopitishwa kwenye vikao vya chama cha CCM ,hawakupata idhini ya wapiga kura.

Mgogoro mkubwa wa kikatiba ambao utaifanya nguvu ya dola kuwatishia wananchi kuheshimu mamlaka ya wanaccm, inaweza sababisha sintofahamu na uvunjifu wa uvumilivu kwa wananchi.

Nimekuwa nikiwakumbusha kuwa Mwalimu aliasa bila CCM madhubuti nchi itayumba, kauli hii imewafanya mbweteke na kutoka kwenye chama chenye ushawishi na kuwa chama dola, kinacho tegemea nguvu kuliko ushawishi kwa wananchi.

Matokeo yake mnalazimisha maji kupanda mlima badala kuyafungulia yafuate mkondo wake.

Hatuna budi kulitazama hili jambo kwa jicho la kinabii, vinginevyo hayo maendeleo mnayo yasema itabaki historia.

Ni wakati sasa kwa wanasheria na watetezi wa haki za wananchi kulitazama hili kwa macho ya kizalendo ili mgogoro huu wa kikatiba ulioletwa na serikali upatiwe uvumbuzi kwenye jicho la sheria.

Wananchi ambao ndiyo waathirika wakubwa (deceases) walioporwa haki yao ya kutoa mamlaka na madaraka kwa serikali za mitaa, wasaini petition ya kutoutambua uchaguzi huu wa kihuni katika historia ya Tanzania.

Itasemwa ni uchochezi kama ilivyo kawaida yao lakini uchochezi ni upi, kuibuka migogoro baina ya wateuliwa wa CCM na wananchi au wananchi kudai haki yao ya kuwachagua viongozi wawatakao!!!

Tusiwalazimishe wananchi upofu wa akili tukidhani tunakisaidia Taifa, athari ya kulazimisha mambo ni kubwa kuliko kuliondoa tatizo.
 
Back
Top Bottom