Viongozi wa Serikali kuingizwa mpango wa TASAF si sawa

Kamgomoli

JF-Expert Member
May 3, 2018
1,865
3,802
Rais Samia kapendekeza viongozi wa chini kwa maana ya wenyeviti wa vijiji/Mtaa/Sheia wanaoratibu mpango wa Tasaf km wanamaisha magumu waingizwe kwenye mpango.

Nanukuu,"Katika hatua nyingine Rais Samia Suluhu Hassan ameomba viongozi wa ngazi za chini ambao wanaratibu mpango wa TASAF ili hali nao maisha yao ni ya chini waingizwe kwenye mpango huo ili nao wawe wanufaika kwani mpango huo upo kwa ajili ya kuwainua wananchi wote"

Mimi ni mtu ninaeujua vizuri mpango wa Tasaf kwani nimewahi kushiri kuratibu zoezi hilo.Hivyo napinga kabisa hoja ya kuwaingiza viongozi wawe wanufaika. Kwa sababu zifuatazo:-

1. Kwanza Kiongozi yeyote kwenye jamii lazima awe mfano wa kuigwa kwa kufanya kazi kwa bidii na tabia njema. Umaskini si sifa ya kujisifia mbele za watu.Na haitakiwi ufukara iwe ni sifa ya kiongozi labda km anaulemavu wa kimaumbile na si vinginevyo.

2. Wakati serikali inafikiria kuwaingiza viongozi kwenye mpango itambue kuwa bado kuna kundi kubwa la wazee na wasiojiweza ambao walienguliwa na mfumo eti kwa kutotimiza vigezo japo kiuhalisia ukiangalia maisha wanayoishi utaona wanahitaji msaada.

3. Tukiruhusu viongozi kuingia kwenye mpango kutasababisha manung'uniko makubwa kwa watu wa kawaida ambao kiuhalisia wanamaisha magumu lakini hawakuingizwa kwenye mpango. Vile vile itaingiza siasa kwenye mpango kitu ambacho si kizuri.

USHAURI.
1. Nashauri badala ya kuwaingiza viongozi kwenye mpango, posho zao za usimamizi ziboreshwe( Ziongezwe).Kwasasa kiongozi wa mtaa anaesimamia shughuli za Tasaf analipwa 15,000 kwa Mkiti na 10,000/= kwa mjumbe bila kujali masaa ya kazi. Kuna wakati zoezi huanza saa 5asbhi na kuendelea hadi saa 12 jioni, unamlipaje mtu kiasi kidogo km hicho?

2. Wapewe mafunzo yenye malipo ili kuwaongezea uwezo wa kusimamia na kuratibu miradi ya Walengwa wa Tasaf.

3. Pia kupitia hizo semina, viongozi wapatiwe mafunzo ya njia mbalimbali za kujikwamua kiuchumi km kilimo na ufugaji wa mifugo, nyuki na samaki, utunzaji wa mazingira n.k

Kwa kufanya hivyo tutawafanya kuwa viongozi thabiti kwenye jamii kuliko kuendekeza umaskini kwa kuwapa fedha za bure. Matokeo yake watashindwa kuhamasisha shughuli za kimaendeleo kwani watakua wamezoea vya buree.

Mwisho narudia tena,bado kuna watu wengi wa kawaida wenye maisha magumu na wasiojiweza ambao hawakuingizwa kwenye mapango.Hivyo kabla ya kuwafikiria viongozi tuwafikirie kwanza hawa.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom