Viongozi wa serikali acheni dharau kwa wana Mtwara

Kiwi

JF-Expert Member
Sep 30, 2009
1,054
990
Nimesikia kichefuchefu baada ya kusikia kwenye taarifa ya habari ya ITV usiku huu kauli za kejeli na dharau isiyoweza kuvumilika kwa wananchi wa Mtwara.

Mbunge wa Sumve Mh. Ndassa - 'watu wa Mtwara hawana uwezo wa kufikiria na kufanya mambo kama waliyoyafanya leo. Kuna mtu anayewasukuma'.

Suleiman Zedi Mbunge (sikumbuki jimbo lake) - 'watu wa Mtwara waelimishwe ili waelewe'.

jk 'serikali imechoshwa na vitendo vya vurugu na uvunjifu wa amani na itawashughulikia watu wote wa Mtwara waliohusika na vurugu za leo'.

Kauli zote hizi maana yake ni moja: Wananchi wa Mtwara hawana akili za kufikiria, wanapaswa kuelimishwa ili waelewe na kukubaliana na matakwa ya serikali; wasipokubali kutii basi washughulikiwe ipasavyo. Hii ni dhana iliyopitwa na wakati. Ni mawazo ya kikoloni yasiyostahili kuwepo kwenye serikali ya nchi inayojiita 'huru, ya kidemokrasia na sikivu'.

Ninawalilia wananchi wa Mtwara, ninaililia nchi yangu Tanzania. Wapi tulipopotea hadi 'vinyago' hivi vikaingia madarakani?

Mungu Ibariki Tanzania!
 
Na wamasai wa Loliondo wamewaweka kundi gani???!! sasa vita kusini vita kaskazini. Ila najua Mungu yupo na wanyonge. Wao ndio hawana akili waelimishe kuwa gasi ni ya wazawa na sio ya wachina wala JK na bandari yake na Ridhiwani hapo bagamoyo.
 
Kweli huyu mh.ndasa ndio walewale wajiangaliao ktk kioo na kujiona wenyewe tu.wanania mbaya kwa wanamtwara na watanzania wote.
 
kama ni wajinga wanataka kuwadanganya kuwa gas ni moto wakaye nayo mbali? au wawa ambiye inachemka inakaribia kulipuka wahame mtwara!!!
 
Nimemsikia na nimesikitika kwa vile kauli ya Ndassa inaweza kuwachukiza zaidi wanamtwara kwa jinsi alivyowaona kama wasiojua kitu isipokuwa tu wamerubuniwa!Ndassa hekima ni muhimu sana mambo yanapoharibika hivi!Naamini hata spika alishituka kuendelea na Bunge kutokana na kauli kama hizi kudharau watu kama wasiofikiri ambazo zingechochea hasira za Wanamtwara zaidi na kufanya hata muafaka kuwa mgumu!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Hii ni dharau kubwa. Wananchi tunatukanwa. Viongozi wamejisahau. They are so disconnected with the people who elected them and who pay their salaries. Haishangazi wanafanya madudu kila kukicha. Wanafikiri wananchi ni wajinga. Ukitafsiri alichosema Ndasa ni kana kwamba anashangaa ni nani amewapa ujanja watu wa Mtwara. Yaani anasema watu wa Mtwara hawajui haki zao. Yaani hawawezi kudai au kuuliza maswali juu ya masuala yanayowahusu mpaka kuwe na mtu wa kuwasukuma. Ndasa asichotuambia ni kama madai ya WanaMtwara yana mantiki au la.

Fikra hizi za kihuni kwamba watu wa Mtwara wanasukumwa kuuliza maswali wanayoyauliza zimefanya serikali na kina Ndasa kushindwa kuwaelewa watanzania kwa ujumla. Swala linaloulizwa hapa ni kwamba wananchi wananufaikaje na uvunaji wa raslimali hizi? Swali hili ni sawasawa na mfanyakazi kuuliza ni namna gani serikali inatumia kodi anayokatwa kwenye mshahara wake? Sijui ni wangapi wanaridhika na jinsi serikali inavyotumia fedha zilizotokana na jasho lao. Si dhambi kuuliza maswali haya. Yana maana. Hata kama umefundishwa na mtu kuyauliza, hiyo haifanyi yakose maana. Ni kwanini serikali na kina Ndasa wasitekeleze matakwa ya wananchi, badala ya kutafuta ni nani anayewatuma?
 
Wananchi wa Mtwara hawana uwezo wa kufanya mambo yote wanayofanya sasa mtwara. Lazima Kuna watu wako nyuma yao. ...Mbunge - Richard Ndasa
 
Back
Top Bottom