Mtini
JF-Expert Member
- Apr 28, 2011
- 1,491
- 2,355
Daniel 5:24-31 inasema;
"Ndipo kile kitanga cha ule mkono kikaletwa kutoka mbele zake, na maandiko haya yameandikwa. Na maandiko yaliyoandikwa ni haya; MENE, MENE, TEKELI, NA PERESI. Na tafsiri ya maneno haya ni hii; MENE, Mungu ameuhesabu ufalme wako na kuukomesha. TEKELI, umepimwa katika mizani nawe umeonekana kuwa umepunguka. PERESI, ufalme wako umegawanyika, nao wamepewa Wamedi na Waajemi. Ndipo Belshaza akatoa amri, nao wakamvika Danielii mavazi ya rangi ya zambarau, wakatia mkufu wa dhahabu shingoni mwake, wakapiga mbiu kutangaza habari zake, ya kwamba yeye ni mtu wa tatu katika ufalme. Usiku uo huo Belshaza, mfalme wa Wakaldayo, akauawa. Na Dario, Mmedi, akaupokea ufalme, naye umri wake alikuwa na miaka sitini na miwili.
Napenda kutumia nafasi hii kuwakumbusha wanasiasa/viongozi wote wanaotumia madaraka yao vibaya, wakumbuke utawala wowote wa duniani huwekwa na Mungu ili kuongoza watu walioumbwa kwa sura na mfano wa Mungu. Mungu hatosita kuwaondoa kwa matumizi mabaya ya madaraka ya kukandamiza watu.
Ukiwa wewe ni kiongozi mahali popote "JIULIZE UNATOSHA?'