Viongozi wa dini zingatieni kujali mda katika ibada mnatukwaza waumini wenu.

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,551
22,097
Naomba niseme tu!
Ibada ni jambo jema sana na sina nia ya kupinga, lakini kinachokera watu wengi ni ile kutozingatia mda uliopangwa; Viongozi msitumie udhaifu Wa unyenyekevu Wa waumini kufanya mnavyotaka!
Mataifa yaliyoendelea ambayo ndiyo haswa walitutangulia kujuwa kusali hawako kama sisi tunavyo sali;
Mfano; nimewahi shiriki ibada huko marekani wapo makini sana kwenye mda!
Sasa hapa kwetu Tanzania muumini anayehoji suala la kuzingatia mda anaonekana hana imani! This is not fair!
Kuna Mzungu mmoja ambaye ni padre aliwahi kuja hapa Tanzania mwaka juzi ilitokea siku alipangwa kwenda kusoma ibada ya mazishi katika msiba Wa muumini mmoja mkoani dar es salaam, katika ratiba walimwambia ibada itaanza SAA tano kamili!...yeye alizingatia mda akafika saa nne na nusu kabla ya ibada! Alisubiri hadi saa 7 ibada ikiwa bado haijaanza, alichokifanya aliondoka, na saa Tisa walipompigia arudi aliwajibu tafteni padri mwingine! By the way alirudi kwao Italy!
Kwahiyo suala la mda viongozi Wa dini nyingi hawazingatii kabisa!
"They talk too much"
Na ukihoji wanakwambia Leo siku ya ibada unaharaka kwenda wapi?
Hawatambui kwamba kila muumini huwa anaratiba zake, wengine huwa wanawahi watoto nyumbani, wengine huwa wanawahi stand au airport Kwa safari n.k
Kwanini msizingatie mda? Kwanini baadhi matangazo yasiyo ya lazima yakabandikwa kwenye mbao za matangazo? Halafu pia ebu nihoji- inashindikana vipi ratiba za usafi makanisani wakaajiliwa rasmi baadhi ya waumini kufanya usafi na kanisa likawalipa mishahara Kwa sadaka/michango ya sisi waumini? Inakera sana kusikia baadhi ya viongozi analaumu waumini wasiohudhuria usafi yaani waache kwenda makazini wakafanye usafi! Kwanini msiajili watu na waumini wakawalipa?
 
tutajie kanisa twende kuwaonya
 
Dah.. Mungu ndio amekupa uhai, kazi, watoto, biashara.. shule.. unavihangaikia hivyo kwa siku sita tena kwa uaminifu..

Yani siku moja.. tena masaa machache.. ujihudhurishe kwake kumshukuru, kumsifu na kusikia neno lake unaona kazi sana.. wakati yeye alikuwa na wewe wiki nzima ulipokuwa umelala na ulipokuwa unafanya kazi.. amekulinda, amekufanikisha.. n.k

Kweli wafu wakifufuliwa na watasema..

Ila makanisa ya mwendo kasi si yapo.. mnashindwa nini kuhamia?
 
Back
Top Bottom