Viongozi wa dini wanaruhusiwa kutumia nyumba za ibada kama anavyofanya Gwajima au huu uhuru unapatikana kwa wanachama wa CCM tu?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Mhe. Gwajima anatumia nyumba ya ibada na amekuwa akitumia nyumba ya ibada kutekeleza mahitaji yake ya kisiasa ikiwemo kudhalilisha watu. Lakini pia mara zote amekuwa akienda mbali zaidi na kupambana kwa nguvu zote na Rais wa nchi.

Alianza awamu ya JK, alipoingia JPM akawa anamuunga mkono na hataki asemwe kwa lolote, Sasa hivi awamu ya sita amefika point anakiandama kiti Cha Rais moja kwa moja japo anatumia wasaidizi wake.

Natambua kwamba anatumika kupunguza nguvu na Kasi ya agenda ya Katiba mpya na Kodi lakini je wanaomtuma kuzima mjadala huo wamejiuliza madhara ya mbinu anayotumia?

Viongozi wa dini wakisimama adharani kupingana na serikali kwa kile wanachoona hakipo sawa tutakaa kimya kama tunavyokaa kimya kwa Gwajima?

Kuwa mwanachama wa CCM kunakuwaje Kinga, natamani waibuke viongoz wengine wa dini watumie madhabau zao kuhubiri misimamo na mitizamo yao tuone Kama watavumiliw kama Gwajima.
 
Uhuru huo unapatikana kijani pekee,kama ilivyo ruksa kwa kijani kuendesha mikutano na makongamano ila sii wengine.
 
Gwajima yuko juu sana kwa sasa! Ukiona hata mzee mzima Ai Jii Pii alimgwaya, basi utambue siyo mtu wa mchezo mchezo! Huenda anamiliki siri nyingi za chama.
 
Back
Top Bottom