Kelele za Viongozi wa Serikali Dhidi ya Viongozi wa Dini, ni Uduni wa Uelewa wa Viongozi wa Serikali

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,559
41,071
Nchi yetu ipo kwenye mkorogano wa ajabu kwa sababu ya kuwa na viongozi wasioelewa chochote kuhusiana na sheria na katiba. Uduni huu wa viongozi kukosa kuelewa sheria, na wakati fulani hulka ya unafiki, vimewafanya baadhi ya viongozi kuropoka vitu vya ajabu na hata kuingia kusaini na kuridhia mikataba ya hovyo, kama huu wa bandari.

Rais anapowateua wasaidizi ni muhimu kuwateua watu wenye weledi wa kutosha, watu walio wakweli na siyo wanafiki ambao uwezo wao unaishia kwenye kuimba nyimbo za kumsifia tu Rais, hata pale anapokosea. Masiha Kristo aliwahi kunena kuwa, kipofu hawezi kumwongoza kipofu mwenzie la sivyo wote watatumbukia shimoni. Rais siyo mtaalam wa sheria, anamteua Waziri ambaye hana uelewa wala hajishughulishi kuzijua sheria, kuwa waziri wa Mambo ya Ndani ili akasimamie sheria, atafanya nini la maana zaidi ya kuropoka na kuwaagiza polisi wakafanye mambo yaliyo kinyume cha sheria? Kuwa waziri siyo lazima kuwa mwanasheria lakini mtu akishateuliwa kuwa Waziri au katibu mkuu, ni muhimu kwake kuzitambua sheria na vifungu vya katiba vinavyoongoza Wizara anayoiongoza. Maana huwezi ukawa unaapa kulinda kitu ambacho hata hukijui. Utaapaje kuwa utalinda katiba wakati hata katiba yenyewe huijui?

Waziri anathubutu kusema kuwa eti viongozi wa dini sheria haiwaruhusu kushiriki siasa, halafu haitaji hata hiyo sheria, ni sheria gani! Huu ni uropokaji wa kiongozi wa Serikali asiyejua chochote.

Hakuna sheria yoyote, inayomzuia kiongozi yeyote wa dini kushiriki au kufanya shughuli za siasa. Haipo sheria hiyo. Katiba yetu inatamka wazi kuwa mtanzania yeyote anao uhuru wa kushiriki shughuli za siasa, ikiwa ni pamoja na kuomba kuchaguliwa kuwa kiongozi na kuchagua kiongozi. Ndiyo maana, tangu zamani, kuna viongozi wa dini, kama Askofu Mwamasika alikuwa mbunge wa Iringa miaka ya 1970, marehemu Askofu Rwakatare alikuwa mbunge wa kuteuliwa, na sasa Askofu Gwajima ni mbunge wa Kawe, na wengine wengi. Hao wote ni viongozi wa dini na ni viongozi wa kisiasa. Ni Kanisa Katoliki pekee ndiyo linalowazuia viongozi wake wa dini kugombea uongozi wa kisiasa wakiwa bado ni viongozi wa kanisa, lakini siyo zuio la kikatiba au sheria yoyote.

Kinachokatazwa ni kiongozi wa dini kutumia jukwaa la dini kufanya siasa, siyo kiongozi wa dini kufanya shughuli za kisiasa.

Jambo la pili, kupinga uovu kama vile wizi, uporaji, uonevu na upendeleo, rushwa, ufisadi, hila na hadaa, siyo siasa bali ni suala la kimaadili na kiimani; sawa na ilivyo kutetea haki za watu. Haya yanaweza kufanywa kwenye nyumba za ibada, majukwaa ya kijamii na hata kwenye majukwaa ya siasa.

Tunaomba Rais Samia, mkanye kwa nguvu Waziri Masauni, asitoe maneno ya uwongo kuwatisha viongozi wa dini. Yeye Masauni, kwa kuwazuia viongozi wa dini wasishiriki shughuli za kisiasa mahali popote na kwa mazingira yoyote, anakiuka katiba ya JMT. Kutokana na kosa hilo, Masauni anastahili kufukuzwa kutoka kwenye nafasi ya uwaziri kwa sababu anafanya kinyume na kiapo chake cha kulinda katiba.
 
DP imekutoa Kwenye kutumia Lugha za Staha hadi sasa umekuwa mtu wa Matusi Matusi na Lugha za ajabu ajabu 😀😀

Siasa ni pamoja na uvumilivu ndio Sababu huwezi kumsikia Kikwete au Mbowe wakitumia Lugha mbofu mbofu!
Kamsikilize wasira,watu wanadhani watakuwa Marais Kwa kutumia dini na DP World imeshawakata wasubirie 2030 huko.
 
Kamsikilize wasira,watu wanadhani watakuwa Marais Kwa kutumia dini na DP World imeshawakata wasubirie 2030 huko.
Wassira amepitwa na wakati hata uwezo wake wa kufikiri kwa umri wake ni chini ya 50% ni Heri ya artificial intelligence

Iwe Mwigullu au January DP hawezi kuwazuia!
 
Wasira na wewe dekio nani amepitwa na wakati? 😁😁
Wasafwa mnaotawaliwa na Wanyakyusa hadi leo 😂😂

Wasafwa nyie ni Watumwa akishuka Masanja Kutoka Ludewa mnajipanga Foleni kuchukua namba za kulima Kwenye Mashamba yake ya mpunga huko Rujewa na Hii ameishuhudia pale KKKT Kijitonyama 🤣

Nyie Wasafwa ndio kabila la mwisho kabisa Kwenye Ulimwengu wa Siasa 😀😀🔥🔥
 
Ni ujinga tu, wanalazimisha kuaminisha watu Chadema wanakosea kuwaalika viongozi wa dini kwenye mkutano wao, wakati wao wakiwa na mambo wanayotaka kuifikia jamii, kama kukemea rushwa, huomba msaada toka kwa viongozi wa dini waongee na waumini wao.

Lakini kibao kinapogeuka, wao wanasiasa wanapotakiwa kusikiliza ushauri toka kwa viongozi wa dini, wanabadilika, wanadai isichanganywe dini na siasa, hawakumbuki hata hao wanasiasa wenyewe, nao pia wana dini zao.

Hivi utaitenganisha vipi dini na siasa? kwani siasa ipo kwa ajili ya n'gombe? siasa ni watu, na dini pia, inahusisha watu hao hao, sasa utatenganisha vipi hivi vitu viwili?

Hawa matapeli wanataka dini itenganishwe na siasa ili wakiiba wasikemewe, wanataka kupunguza uwanja wa kuwakemea kwa kuwaondoa viongozi wa dini wanaowaogopa, na kuwaonea aibu, wabaki wanasiasa wenzao, ili wakiulizwa maswali magumu, waje na majibu mepesi.

Tusichezeane, tusidanganyane, tusitaniane, mkataba wa bandari ni wa hovyo, mwarabu hawezi kuja kujitawala milele kwenye ardhi ya Tanganyika, Never.
 
Wassira amepitwa na wakati hata uwezo wake wa kufikiri kwa umri wake ni chini ya 50% ni Heri ya artificial intelligence

Iwe Mwigullu au January DP hawezi kuwazuia!
Nukuu ya JF leo hii: ...Eti jogoo akizeeka anataga kayai kadogo...Du! 🤣
 
Back
Top Bottom