Viongozi wa dini wamtuliza Dk Slaa
"Rais amechaguliwa na robo tu ya wapigakura. Nec imeongeza majina kwa sababu kabla ya uchaguzi ilisema wapigakura wote ni 19.9 milioni, lakini akitangaza mshindi Jaji Lewis Makame anasema ni 20.1, hatujui wametoka wapi, alisema Profesa Baregu.
Dr angewafukuza wanafiki wakubwa hawa, kama kweli wanaipenda amani wangeanzia kuiambia CCM iache kuwadhulumu watanzania haki yao kwa kuchakachua matokeo ya urais. Lakini wanakaa kimya halafu tuwaeleweje!
Ina maana shughuli yote ile kumbe Prof wangu alikuwa akishindania wapiga kura laki mbili tu katika nchi yenye watu milioni 45!!!!
Kuna ukweli katika message yakoHawa watu ni hatari. Wanalinda sana madhambi ya watawala kwa kutudanganya waumini kwa kisingizio cha amani na utulivu. Mbona Yesu alikabiriana na udhalimu hivyo hivyo. Mungu ameshaadhibu mataifa kwa sababu ya uongozi batili. Adhabu tuliyonayo Tanzania ya maisha magumu, ufisadi ni dhahiri ni ghadhabu ya Mungu. Kwa sisi wote wenye imani na Dr. Slaa tumtie moyo apiganie haki zetu kwa sababu Mungu anasikia vilio vya sisi wanyonge wenye kuporwa haki kupitia utaratibu halali za sanduku la kura. Napenda kuwaomba wote kuwa hili siyo suala la Dr. Slaa bali letu sote tulioporwa haki hata kama ni kura moja.
Naomba swali hili aulizwe Dr Mokiwa. Labda kama zile milioni 10 alizichukua.Kwa Matokeo ya Ubunge CHADEMA wanaweza kwenda mahakamani . . .
Lakini je kwa matokeo ya Urais, watafuata utaratibu gani wa sheria?
that is why i believe in myself.Roho inauma sana, hasa pale inapotegemewa dini ziondoe na kuvunja dhuluma, ndiyo zinazidi kuwaondolea wananchi hata ile haki kidogo wanayotaka kuijenga na kuitetea!
hawa mafisadi ni mkono wa ibilisi, na yeyote anayesimama upande wao, naye ni baba wa uovu.
tanzania inahitaji ukombozi.
dini ni mambo ya kiroho, ila wanasahau kama mwili una mateso, hata dini haikubaliki popote. wao wana-assume kuwa raia watateseka kimwili na papo hapo waweze kutii dini? kamwe haitatokea. wakumbuke darfur, congo, rwanda, irak, afghan nk. hawataki hata kuisikia neno dini, kwani haijawaondoa ktk machungu ya dhuluma zilizowapata.
haki kwanza, ndipo imanina dini itapata nguvu.