Troll JF
Platinum Member
- Feb 6, 2015
- 9,277
- 13,703
VIDEO:
Siku chache baada ya viongozi waandamizi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA @ChademaTZ2) wakiongozwa na Mwanasheria Mkuu wa chama hicho Wakili Dkt. Rugemeleza Nshala Rugemeleza kuutangazia umma kuwa zuio la Mahakama Kuu lililokuwa limetolewa Juni 10.2025 likipiga marufuku chama hicho kuendelea na shughuli zote za kisiasa na kiutendaji hadi hapo kesi ya msingi inayohusu usawa kwenye 'mgawanyo wa mali' itakapotolewa maamuzi, hatimaye tamko hilo la CHADEMA limepingwa rasmi
Wakili Gido Semfukwe anayeongoza jopo la Mawakili wa waleta maombi (aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar Saidi Issa Mohamed na wenzake wawili) kwenye, amejitokeza mbele ya Waandishi wa Habari na kukanusha vikali tamko la chama hicho, sambamba na kutoa wito kwa umma kupuuza kile alichokiita ni 'upotoshaji wa makusudi' unaofanywa na viongozi wa CHADEMA
"Amri ya Mahakama inapotolewa inakuwa halali na kuzifunga pande zote husika, pamoja na umma kwa ujumla kutegemea na muktadha wa shauri lenyewe mpaka ambapo amri hiyo itatenguliwa na Mahakama yenye mamlaka, pia tunachukua fursa hii kurejea amri husika (amri namba 2, ukurasa wa 20) kutoka maombi madogo Na. 8960/2025 ambayo ilieleza kinagaubaga kuwa mazuio haya ni ya kudumu hadi kesi ya msingi itakaposikilizwa na kutolewa maamuzi" -Wakili Gido
Aidha, Wakili huyo kutoka Hyperion Legal & Corporate Consultant ametoa rai kwa makada wa CHADEMA na Watanzania kwa ujumla wake kujiepusha na upotoshaji unaofanywa na viongozi wao na kuacha kujihusisha na uvunjwaji wa sheria za nchi, kwani matamko hayo yapo kinyume na sheria na yanatazamiwa kuhamasisha, kuvunja na kudharau amri za Mahakama ikiwa ni mkakati wa kupima uwezo wa vyombo vya Dola katika kutimiza utawala wa sheria na utekelezaji wa amri halali za Mahakama.