Viongozi wa Chadema tuambieni tukusanyike wapi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi wa Chadema tuambieni tukusanyike wapi

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Quinine, Nov 3, 2010.

 1. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #1
  Nov 3, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,840
  Likes Received: 11,962
  Trophy Points: 280
  Hii haikubaliki nasema kama noma na iwe noma

  Matokeo Tunduru Kaskazini

  Kikwete amepata kura 22,261

  Slaa amepata kura 1,965

  Lipumba amepata kura 12,935
   
 2. DICTATOR

  DICTATOR JF-Expert Member

  #2
  Nov 3, 2010
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hayo matokeo yameandaliwa kabla hata ya uchaguzi na kutumwa NEC yale yenyewe yamechakachuliwa, ni imani yangu mwisho wa CCM ndo huu, kama watachomoka saizi ndani ya miaka mitano itakuwa migumukwa watanzania. Its too sad.
   
 3. s

  shiezo Member

  #3
  Nov 3, 2010
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Tuache ushabiki, katika uchaguzi wa mwaka huu ni vigumu sana kuchakachua matokeo, labda kwa kuwahonga mawakala. Kila kituo kina wakala, baada ya kuhesabu matokeo hujazwa na kila wakala husaini na kupewa nakala ya fomu ya matokeo. Matokeo yakiwa tofauti na nakala aliyopewa wakala, kisheria matokeo hayo ni batili. sasa utachakachuaje hapo. Tuache ushabiki wa kisiasa, unaweza kuiangamiza nchi yetu. Tudai haki kwa demokrasia. Kama chama fulani kimeshinda, wacheni kiongoze. Ndio Demokrasia. Jambo la msingi la kufanya ni kujipanga ili na hiki kilichoshindwa kishinde katika uchaguzi ujao. kama kina sera nzuri kiwaelimishe wananchi hadi wakikubali na wakipe ushindi. Otherwise tunaweza kuipeleka nchi yetu kubaya
   
 4. m

  mtx2006 JF-Expert Member

  #4
  Nov 3, 2010
  Joined: Feb 1, 2008
  Messages: 273
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45

  Usidanganye watu ndugu yangu. Kama ingekuwa hivyo kwa nini TUME iwakataze watu kutumia matokeo kama yanavyopatikana kwenye vituo. Wasimamizi wa vituo wana haki ya kutangaza matokeo ya vituo vyao. NEC taifa inatakiwa itangaze mshindi atakaye pata kura nyingi.

  Matatizo ninayo yaona:-
  1. NEC ya akina Makame na Kiravu haitambui kuwa wasimamizi wa vituo nao ni NEC. Ndio maana wakawazuia kutoa matokeo ya uraisi
  2. Kama wasimamizi wa vituo wameaminiwa kutanga washindi wa udiwani na ubunge, kwa nini wasiaminiwe kutanga matokea ya uraisi

  Hapa kuna namna na watanzania tunatakiwa kuwa macho na ili. La sivyo tutegemee akina R1, January, Mwinyi n.k wataendelea kupeta
   
 5. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #5
  Nov 3, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,840
  Likes Received: 11,962
  Trophy Points: 280
  Chadema muwe jasiri say something we cant wait longer say NO to NEC then leave the lest to us, haiwezekani waibe leo tusubiri miaka mitano wapi na wapi. Najua mnaangalia sheria zinasemaje lakini wao hawaangalii sheria zinasemaje,

  ...........nani hukooooo ndani..............hebu....niletee chuma changu leo naenda kusikiliza matokeo ya NECK ya mtu. KAMA NOMA NA IWE NOMA.
   
 6. Juaangavu

  Juaangavu JF-Expert Member

  #6
  Nov 3, 2010
  Joined: Nov 3, 2009
  Messages: 915
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Vipi! Mbona vyama vilivyoshiriki havichukui jukumu la kujumlisha matokeo ya kwenye vivuli walopewa na kisha kumwaga hadharani ili tulinganishe! Au watakamatwa!
   
 7. Hero

  Hero JF-Expert Member

  #7
  Nov 3, 2010
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 749
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 45
  Kumbe unajua ni rahisi sana kuchakachua eeh alafu unajichanganya. Hii delaying tactic ndio haswaa inayopelekea kuchakachuliwa kwa matokeo. tume yenyewe ya ccm, ili itangaze lazima ikulu itoe consent, who is ikulu JK. sasa wewe unaongea nini, toka usingizini kama unaijali nchi yako!!!!
  hivi kubaya wapi zaidi ya mafisadi walikoipeleka?
   
 8. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #8
  Nov 3, 2010
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,293
  Trophy Points: 280
  Kaanzieni Jangwani au pale stesheni:smile-big:
   
 9. Hero

  Hero JF-Expert Member

  #9
  Nov 3, 2010
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 749
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 45
  You can fool people so some time only!
   
 10. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #10
  Nov 3, 2010
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Na mkamwage damu zenu wenyewe!
   
 11. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #11
  Nov 3, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Wakuu tuache kuhamasishana kufanya mambo ambayo yataipeleka nchi katika machufuko. It doesnt matter whether wamechakachua or not, so far, hayawezi kubadilika. Sanasana hapo watu kadhaa watapoteza maisha, na Kikwete ataendelea kuwa Rais, waliokufa itakuwa imekula kwao. Sasa it doesnt help. Lets be generous tunapofanya maamuzi magumu kama haya. Hivi kuna fahari gani tuingie kwenye machafuko kama ya Kenya halafu at the end of the day, Slaa awe waziri mkuu wakati watanzania elfu kadhaa wapo kaburini? Tuweni waungwana wakuu. Mshaurini Slaa atulize mzuka kuokoa maisha ya watanzania wanaoweza kufa pasipo hatia.
   
 12. Hero

  Hero JF-Expert Member

  #12
  Nov 3, 2010
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 749
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 45
  Nafikiri wa kushauriwa ni JK na wala sio Dr. Slaa! lawama ya yoyote yatakayotokea ni kwa JK na si vinginevyo + ccm propaganda machinery (kinana)!
   
 13. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #13
  Nov 3, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,840
  Likes Received: 11,962
  Trophy Points: 280
  Watu wanakufa kwa ajili ya wengine ndiyo maana kuna siku ya mashujaa, natamani haya maneno ungemwambia Mkwawa wakati anakutetea wewe toka kwa wajerumani kuwa alipokufa ilikuwa imekula kwake shame on you x2.
   
 14. Hero

  Hero JF-Expert Member

  #14
  Nov 3, 2010
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 749
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 45
  He really deserve that, shame upon him always!!!!
   
 15. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #15
  Nov 3, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,221
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Mkuu nadhani hauifahamu Tunduru Kaskazini; Ni sawasawa na kulalamika Dr. slaa kupata kura 40 kwenye jimbo la Pemba,kama ungeifahamu hali ya kisiasa ya huko usingeshangazwa kwa Chadema kupata kura hizo.

  Tatizo wengi wetu tunaifikiria hali ya kisiasa ya Tanzania kwa mtizamo wa ki-JF, muhimu ni kuyachukuliwa matokeo haya kama fursa nzuri ya kujenga mtandao mzuri wa kichama kuelekea 2015, makosa ya NCCR baada ya uchaguzi wa 1995 yasirudiwe kamwe.
   
 16. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #16
  Nov 3, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Usilinganishe kesi ya Mkwawa na hii ya sasa. Mkwawa ajiua, je na Slaa naye ajiue kuepusha aibu ya kushindwa na CCM?

  Na kwa bahatimbaya inaonekana hujafanya utafiti wa kutosha kuweza kujua kama ni kweli Slaa amepata hizo kura au la. Kwa taarifa yako, CCM ilikuwa inamnunua mpiga kura kwa bei ya 5000 hadi 10000. Hizi ni habari zenye ushahidi kabisa. Mabalozi wa nyumba kumi katika baadhi ya maeneo huko Iringa walikuwa wanapita nyumba hadi nyumba wanaulizia kama una kadi ya kupigia kura, wakiprove kwamba unayo wanakuandika jina, wanakukatia buku kumi, plus khanga, tshirt na kofia na kukuambia uhakikishe unaipigia kura CCM. Usipoipigia viongozi wa serikali watagundua kwamba hukuipigia na hatua zitachukuliwa dhidi yako. Kwa hiyo watu wengi huko vijijini walidanganyika na kujikuta wakiipigia kura CCM.

  Sasa ninyi mtakomaa tu kwamba kura zimeibiwa pasipo kutrace back hali halisi. Njaa ya watanzania ndiyo inayoipa ushindi CCM. Badala ya kujiingiza kwenye vurugu zisizo za lazima, tuangalie namna ya kutoa elimu ya kutosha kwa watanzania kwa ajili ya mabadiliko ya baadaye.
   
 17. k

  kasimba123 JF-Expert Member

  #17
  Nov 3, 2010
  Joined: Apr 18, 2010
  Messages: 1,318
  Likes Received: 188
  Trophy Points: 160

  wanaiba kwa kuwahonga mawakala mbona hilo liko wazi
   
 18. u

  umenena Member

  #18
  Nov 3, 2010
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dhuruma zimezidi, wazalendo tusimame imara, nguvu ya umma itumike, kusubiri miaka mingine mitano ni kutojua wajibu wetu kwa kizazi kijacho, tutaendelea hivi hadi lini??? Dr. Slaa tunasubiri tamko lako, umetufumbua macho, maovu mengi ya viongozi wetu tumeyaona na tunaendelea kushuhudia, nchi na raslimali zake si zao peke yao, ni mali ya umma, wazalendo tujifunge mikando tufuatilie haki zetu. :A S angry:
   
 19. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #19
  Nov 3, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  hilo la wizi wa kura usiseme kabisa. Katika jimbo la ubungo katika maeneo ambayo walijua ni ngome ya chadema kulikuwa na vituo 7 vya kupiga kura; kura zilihesabiwa na kukamilika ndani ya masaa mawili, yaani saa mbili usiku matokeo yalikuwa tayari yamejulikana fomu za matokeo kujazwa na mawakal kutakiwa kuondoka na nakala zao. Katika ngome za ccm zenye vituo 2 au 3 vya kupiga kura zilihesabiwa kwa masaa zaidi ya matano mpaka nne usiku na matokeo kubandikwa ukutani na masanduku kuchukuliwa mara moja kupelekwa makao makuu ya kata.

  Katika vituo vilivyokuwa katika ngome ya chadema licha ya kazi ya kuhesabu kukamilika saa mbili usiku, fomu za matokeo kujazwa na mawakala kutakiwa kuondoka, masanduku ya kura hayakuondoshwa hadi alfajiri ya jumatatu ndipo na matokeo yakabandikwa ukutani. Ucheleweshaji wa kuondoa masanduku ya kura licha ya kazi ya kuhesabu kukamilika mapema katika ngome za chadema ilikuwa na nia ya kuwazuia wapiga kura kufahamu matokeo mapema kwa sababu wananchi hawaruhusiwi kusogea kwenye eneo la kuhesabu kura kama masanduku ya kura hayajaondolewa.

  Utagundua kuwa kuchelewesha kuhesabu kura za vituo vichache katika maeneo yaliyo ngome za ccm kulifanywa kusudi ili kufahamu ccm ilipata kura ngapi na uchakachuaji kufanyika.
   
 20. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #20
  Nov 3, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  dr slaa na wote tunaotaka mabadiliko tusipokuwa waangalifu na makini, hii mashua ya mabadiliko chadema tutaizamisha, tukumbuke kuwa watanzania walio wengi wanatamani kuvipatia kura vyama vya upinzani lakini wanatishwa na ccm kuwa vyama vya upinzani vitasababisha vuruguna umwagaji damu. Lakini katika uchaguzi huu baadhi ya watanzania wameamua kupuuza kauli hizo potofu za ccm na kumpigia kura dr slaa na chadema.

  Sasa tutakapoanzisha vurugu kwa visingizio vya kuibiwa kura, athari zake hazitawatapata wanaccm peke yao, kwani vurugu hazina macho. Wanachama, mashabiki na wote walioipigia kura chadema watakuwa hatarini kuathirika kwa namna mbali mbali kama vile kupoteza maisha, kuumia, kupoteza au kuharibiwa kwa mali zao n.k mara baada ya vurugu na umwagaji damu huo kuisha watakaa chini na kutafakari kwa makini na pengine huo ndio utakuwa mwisho wa watanzania kuunga mkono vyama vya upinzani. Hilo likitokea tutakuwa tumejenga upinzani au tumeinufaisha ccm na mafisadi kwani watatumia hali hiyo kuwatisha zaidi watanzania.

  Hebu fikiria kwa woga tuu siku mbili kabla ya upigaji kura mafuta yalianza kupotea vituoni, je zitakapoibuka vurugu ni ajira kiasi za watanzania zitapotea?

  Je kuna uhakika gani hao watakaopotelewa na ndugu, jamaa, kuumia kupoteza ajira au biashara zao, mali n.k kama wataendelea kuiunga mkono chadema na upinzani?

  Lakini kama tutadai haki zetu kwa busara, hekima na kufuata taratibu ni wazi kuwa tutatunza idadi ya wanachama, mashabiki na waliotuunga mkono mwaka 2010 na kila kukicha tutaongeza idadi yao baada ya watanzania kugundua ukweli kuwa upinzania sio vurugu, fujo, vita na kuuana.

  Tukumbuke kuwa ccm tayari imetayarisha vijana wake wajulikanao kama green guard, na tayari wameshanunua bendera, kofia na mavazi ya chadema kwa ajili ya kuvvaa vitu hivyo na kuanzisha fujo, vurugu na hata mauaji mara tu tutakapoanza kupinga matokeo ya uchaguzi huu. Ili chadema ionekane ni chama cha umwagaji damu.

  Ushauri wangu ni kuwa dr slaa atuongoze na sisi sote tuelekeze ngucvu zetu katika kudai katiba mpya kwa maandamano makubwa ya mara kwa mara, kwani hata katika kujibu maswali kuhusu mabadiliko ya katiba mara kwa mara viongozi wa ccm wamwkuwa wakisema kuwa katiba itabadilishwa kutakapokuwepo mahitaji ya kufanya hivyo. Hivyo iwapo tutaanisha maandamano ya kudai katiba na tukahamasishana kushiriki kwa wingi ni wazi kuwa haja ya kubadili katiba itajionyesha wazi wazi na hilo litashughulikiwa.

  Ni katika kubadili katiba ndipo tume huru ya uchaguzi itakapoundwa na kuondoa mifumo yaote ya kuipendelea ccm katika chaguzi mabali mbali.

  Kikubwa tukumbuke kuwa tumeamua kuviunga mkono vyama vya upinzania kwa nia ya kuongeza kasi ya maendeleo ya tanzania, hivyo vurugu, fujo na mengine kama hayo ni kinyume cha lengo letu la kuongeza kasi ya maendeleo ya tanzania. Najua sote tuna uchungu wa kuibiwa kura, lakini tuspokuwa makini tukazamisha mashua tuliyomo chadema, hata hizo siasa za ushindani zitapoteza mweleko.

   
Loading...