Viongozi wa CHADEMA chukueni hatua mapema

Ifike mahali watendaji wakuu wa halmashauri kama Mkurugenzi, mwekahazina na Afisa mipango wawe ajira zao zinasimamiwa na halmashauri husika ili yatokeapo mambo kama haya lawama iende directly kwa baraza la madiwani.
Ona ilivyokuwa Halmashauri ya jiji la Mwanza wakati ipo chini ya Chadema na mkurugenzi ni Kabwe hali ilivyokuwa, madiwani wanalalamika na Mbunge analalamika lakini Pinda anamlinda mtu wake.
Hapo bado CAG akitoa hati chafu ya kunuka kabisa bado kuna watu wangesema ona halmashauri ya chadema imepata hati chafu. Huo ni ujinga wa kimfumo
 
Good tumia profession yako vizur bhac na fact
Zuberi, siasa ni jinsi ya kucheza na akili na kujua nini kitawafurahisha ama wadharirisha watu fulani na kwa maslahi gani lkn siasa hazipo kwa kukupa wewe faida kabla ya wao kunufaika. Hivi kuzuia sukari na kufanya mwanainchi ateseke eti napambana kupata kodi ilihali migodi wanakwepa na vitaru vya gesi hutaki watu wajue hapo unamsaidia nn mtanzania wa shinyanga vijijini?
 
M
TUJISAHIHISHE.!

By Malisa GJ,

Ripoti ya CAG inaonesha kuwa Halmashauri 3 zilizopata Hati chafu ni;

1. Karatu DC (CHADEMA)
2. Hai DC (CHADEMA)
3. Kigoma/Ujiji MC (CCM)

Halmashauri 1 iliyopata Hati Mbaya ni Halmashauri ya mji wa Tunduma (Town Council) inayoongozwa na CHADEMA. Hawa walificha vitabu 79 vya mapato, Walificha hati za malipo (voucher) zenye thamani ya SHS.178,511,580, Na walitumia SHS.17,158,500 kufanya malipo yasiyo na viambatanisho. Pia wakati wanakaguliwa hawakuandaa vitabu vya hesabu.

#MyTake:
Nimesikitika sana kuona Halmashauri zilizo chini ya CHADEMA zimeongoza katika kufanya vibaya. Hivi kama tumepewa Halmashauri chache na tukafanya vibaya tukipewa nchi itakuaje?

Tulipaswa kuwa mfano kwa wengine. Wananchi wanakata tamaa kuona tunafanya yaleyale yanayofanywa na CCM. Halmashauri ya Wilaya ya Hai ni nyumbani kwa Mwenyekiti wetu wa chama. Tunaongoza halmashauri hii kwa mara ya pili sasa, hii ilipaswa kuwa mfano. Lakini imetia aibu kwa kupata hati chafu?

Halmashauri ya Karatu alikua anatoka Katibu Mkuu wetu wa Chama Dr.Wilbroad Slaa. Wakati ukaguzi unafanyika alikua bado hajajiuzulu. Maana yake ni kwamba ikiwa Dr.Slaa asingejiuzulu tungekuwa na Halmashauri mbili zenye hati chafu. Moja nyumbani kwa Mwenyekiti wetu na nyingine nyumbani kwa Katibu Mkuu. This typical shame.!

Tutapata wapi moral authority ya kukemea CCM ikiwa tunaruhusu ujinga wa aina hii uendelee kujitokeza kwenye halmashauri tunazoongoza?

Watendaji waliofanya ubadhirifu Hai, Tunduma na Karatu na kutusababishia doa kwenye chama chetu wamechukuliwa hatua gani? Au madiwani wanaendelea kuwalea? Nilitegemea baraza la madiwani Hai, Karatu na Tunduma wawe wameshawang'oa wakurugenzi wa Halmashauri hizo pamoja na watendaji wote waliohusika.

Lakini mnakaa kimya bila kuchukua hatua yoyote then mnategemea wananchi waendelee kutuamini? Kama madiwani wa halmashauri husika mmeshindwa kuchukua hatua mnategemea wananchi ndio wajimobilize na kufanya mobb justice au? Kama ndivyo, nini maana ya nyie kuwepo sasa?

Watanzania wametuamini, wametupa mamlaka ya kuongoza jiji la Dar na Manispaa zake mbili pamoja na majiji ya Arusha na Mbeya. Je ripoti ya CAG inatoa taswira gani kwny haya majiji tuliyopewa kuongoza kama tumeanza kuteleza kwenye halmashauri za wilaya?

Ni aibu kwamba katika Halmashauri 4 zilizofanya vibaya, 3 zinaongozwa na CHADEMA na moja CCM. Hii ni sawa na kusema robo tatu (75%) ya mafisadi waliopo kwenye Halmashauri, wamejaa zaidi kwenye Halmashauri zinazoongozwa na CHADEMA. Hii si sawa hata kidogo na inakatisha tamaa sana.

Nategemea chama kitoe tamko kuhusiana na jambo hili na kwa kuwa halmashauri zote 3 bado zipo chini ya CHADEMA hadi sasa, basi mabaraza ya madiwani yaagizwe kufanya kuchukua hatua kali kwa watendaji wote waliohusika ikiwa ni pamoja na kuwang'oa wakurugenzi.

Haiwezekani kila siku tunakemea wizi serikalini lakini sisi tunalea wezi kwenye halmashauri tunazoongoza. Kama Mayor/Mwenyekiti ameshindwa kuzuia ufisadi kwenye halmashauri yake ni bora ajiuzulu na atoe nafasi kwa wengine wenye uwezo wa kupambana na ufisadi.

Huu sio muda wa kubembelezana, ni muda wa kazi. Wananchi wametuamini na kutupa kazi tusiwaangushe. Ikiwa tunashindwa kuwa waaminifu katika haya madogo hivi, itakuaje kwa makubwa? Tujisahihishe.!

Nimeyasema haya kwa nia njema kbs ya kusaidia chama changu. Marehemu Mohamed Mtoi aliwahi kusema "Tusiwe wepesi wa kutetea uozo kwenye chama chetu, maana tutakuwa hatukisaidii chama wala wabunge wake"

Na ktk hili nimeamua kusimamia maneno ya Mtoi. Siwezi kutetea uozo huu kwa sababu tu umefanywa na chama changu. Never.!

NB: Najua kuna watu wangependa nitoe maoni haya kwenye vikao vya ndani, lakini nimelazimika kuyasema hadharani kwa sababu ufisadi wa halmashauri hizi ulifanyika hadharani na CAG ametoa taarifa yake hadharani na Tanzania nzima inajua kuw ktk halmashauri 4 zilizofanya vibaya, 3 zinaongozwa na CHADEMA na 1 ilikua chini ya CCM lakini kwa sasa ipo ACT.

Narudia maneno ya Marehemu Mtoi kuwa "Tusiwe wepesi wa kutetea uozo ndani ya chama chetu, tutakua hatukisadii chama wala wabunge wake". Penye mazuri tusifie lakini penye makosa tukosoe na kukemea. Chama kwangu ni muhimu lakini Tanzania ni muhimu zaidi.

Malisa GJ.!

Ndugu Malisa unapotosha umma. Lakini inawezekana unafanya siasa-laghai. CAG hakagui utendaji wa mabaraza ya madiwani ambao Chadema inaweza kuwa inaongoza. CAG anakagua mamlaka ya utendaji, Mkurugenzi wa Halmashauri na team yake. Hawa wote ni wateule au waajiriea wa Serikali ya Chama tawala. Sheria, taratibu na kanuni zetu za utawala wa Halmashauri haziruhusu madiwani kuwafukuza kazi wateule wa mamlaka za juu katika Halmashauri. Kwa hiyo, defacto corrupt katika hizo Halmashauri zilizotajwa na CAG ni watendaji wake, wateule/waajirowa wa Serikali ya Chama tawala.
Ili kuwa na uhakika wa uwajibikaji katika siku za usoni, tupendekeze kufanyika kwa mabadiliko katika sheria za Serikali za Mitaa kuweka kipengele cha wafanyakazi na maofisa wa halmashauri kuajiriwa na kuwajibika moja kwa moja kwa Mabaraza ya Madiwani.

JPM anafanya vizuri, CAG amempa suppprt kubwa. Sisi wananchi tunawajibika kuwa wakweli.
 
Unaulizwa hivi halimashauli zilizopata hati chafu ni kwa sababu ya Lowasa. Unaacha hoja ya msingi unaleta chuki zako na Lowasa. Lowassa ninani ktk CDM. Mashinji unamjua?
Zimepata hati chafu kwa sababu Chadema kuna unafiki, narudia tena, shutuma zinahusu unafiki wa Chadema, Lowasa ni mfano tu wa huo unafiki.
 
Chadema ni genge la wezi linalotaka madaraka kwa hali na mali,na huyu Malisa kaanza kuifukunyua chadema Mbowe hatamvumilia,tukumbuke yaliyompata Zitto.Hapa kina molemo,makene lazima wampe Mbowe habari na atanyooshwa tu.
Soma ripoti ya CAG serkali ni ya CCM kitu ambacho hamsemi ni kwamba wakurugenzi ni wateule wa Rais hivyo wanakingwa kifua wizara.Kulikuwa na mtandao wa wizi ndani tamisemi ndo maana Rais ameona ahamishie wizara ofisi ya Rais.Ili kukomesha wakurugenzi waajiriwe na halmashauri zenyewe ili wawajibike moja kwa moja..
 
Zuberi, siasa ni jinsi ya kucheza na akili na kujua nini kitawafurahisha ama wadharirisha watu fulani na kwa maslahi gani lkn siasa hazipo kwa kukupa wewe faida kabla ya wao kunufaika. Hivi kuzuia sukari na kufanya mwanainchi ateseke eti napambana kupata kodi ilihali migodi wanakwepa na vitaru vya gesi hutaki watu wajue hapo unamsaidia nn mtanzania wa shinyanga vijijini?
Unachokisema ni kweli kabisa kua hadi sasa mtanzania wa hali ya chini hajaanza nufaika na tanzania yetu kiujumla. Na mabadiliko ya kiutawala ya kipindi hichi kwa kiasi flani nimeona yameanza vizuri ingawa kuna weakness za hapa na pale nyingi. Sakata la sukari nahisi ni kukosha ushauri mzuri wa kudhibiti pili sakata hili hili lina tatizo kubwa kua viwanda vyetu bado vina stock kubwa tangu january na soko limeshikiliwa na sukari ya india ambayo utaambiwa inaingia inapelekwa burundi. tatu gesi na migodi ni mikataba ambayo tumeingia siku nyingi na kuifumua tutaingiza hasara kubwa coz tumewekewa condition ambazo hatuwez kuzi fulfil. eg nigeria yule rais alisema kwenye campain kua ata futa mikataba ya mafuta hadi sasa kaweza? Turudi tanzania tunahitaji kufanya reformation ya nchi sana tena sana.
 
Jiulize huyo mkaguzi katumwa na nani? Na je baada ya kukagua kuna uhakiki unafanywa na halimashauri husika kuona km kilichoandikwa ni sahihi km kilivyo kaguliwa? Baada ya hapo andika comments zako.

Kwa hiyo unataka kusema CAG kakagua kikada, amezipa hati chafu halmashauri zinazoongozwa Na Chadema makusudi....

Mawazo ya kipuuzi sana haya.
 
Chadema pale hakuna kitu, tena sasa hivi wala hawana sera, hakuna watakalo ongea tuwaamini, hovyooo.....
 
Zimepata hati chafu kwa sababu Chadema kuna unafiki, narudia tena, shutuma zinahusu unafiki wa Chadema, Lowasa ni mfano tu wa huo unafiki.
Nina mashaka na uelewe wako.
 
You are missing the point, kilichojadiliwa ni unafiki wa Chadema kumsimamisha urais mtu waliyemtuhumu muda mrefu kwa ufisadi, jina la Lowasa inabidi litokee kwa sababu ndo aliyesimamishwa, ila shutuma ni za Chadema.
I am not missing the point my dear!!!It is an obvious spinning that I am trying to deal with.We are very much aware that there is a propaganda machinery using this platform to misinform the public at large!!!
 
Mkurugenzi wa halmashauri anateuliwa na nani? Katibu tawala wa mkoa anapatikanaje? hao ndio watendaji wakuu
 
Watanzania wametuamini, wametupa mamlaka ya kuongoza jiji la Dar na Manispaa zake mbili pamoja na majiji ya Arusha na Mbeya. Je ripoti ya CAG inatoa taswira gani kwny haya majiji tuliyopewa kuongoza kama tumeanza kuteleza kwenye halmashauri za wilaya?

Wakati unatokapovu ujiulize Wakurugenzi wanateuliwa na nani na wanaripoti kwa Nani?
Unakumbuka kilichomkuta Kabwe wa Dar?. Kwani yeye mteule wa nani?
 
Hiyo ni report ya 2014/15 tunduma haikuwa chini ya Chadema.
 
Halmashauri zote zilizopewa hati Chafu za Chadema watendaji wake lazima wang'oke tu hakuna njia.Haiwezekani kuona tunapiga kelele kuhusu utumiaji mzuri wa utaratibu wa fedha na wa kisheria leo tuambiwe eti Halmashauri zetu zina hati chafu.

Hapo inabidi Mayor na Wenyeviti kuwatumbua wote waliofanya ubadhirifu wa mali za Umma.Awe CCM au Chadema.Ninajua Rushwa kwenye ukaguzi ni kitu cha kawaida sana ila ilibidi kabla hmajakabidhiwa Halmashauri lazima mfanye Audit kama hamkufanya Audit basi mjue imekula kwenu.
 
Mimi nazani hizo halimashauri za chadema ziligoma kutoa rushwa ili ziandikiwe hati nzuri, maana wengine wapo mahakamani eti kisa kuomba rushwa ili wawape hati nzuri

Unachosema ni kweli kabisa.Hebu Imagine madudu yote ya Dar lakini ati Halmashauri zina hati safi.
 
TUJISAHIHISHE.!

By Malisa GJ,

Ripoti ya CAG inaonesha kuwa Halmashauri 3 zilizopata Hati chafu ni;

1. Karatu DC (CHADEMA)
2. Hai DC (CHADEMA)
3. Kigoma/Ujiji MC (CCM)

Halmashauri 1 iliyopata Hati Mbaya ni Halmashauri ya mji wa Tunduma (Town Council) inayoongozwa na CHADEMA. Hawa walificha vitabu 79 vya mapato, Walificha hati za malipo (voucher) zenye thamani ya SHS.178,511,580, Na walitumia SHS.17,158,500 kufanya malipo yasiyo na viambatanisho. Pia wakati wanakaguliwa hawakuandaa vitabu vya hesabu.

#MyTake:
Nimesikitika sana kuona Halmashauri zilizo chini ya CHADEMA zimeongoza katika kufanya vibaya. Hivi kama tumepewa Halmashauri chache na tukafanya vibaya tukipewa nchi itakuaje?

Tulipaswa kuwa mfano kwa wengine. Wananchi wanakata tamaa kuona tunafanya yaleyale yanayofanywa na CCM. Halmashauri ya Wilaya ya Hai ni nyumbani kwa Mwenyekiti wetu wa chama. Tunaongoza halmashauri hii kwa mara ya pili sasa, hii ilipaswa kuwa mfano. Lakini imetia aibu kwa kupata hati chafu?

Halmashauri ya Karatu alikua anatoka Katibu Mkuu wetu wa Chama Dr.Wilbroad Slaa. Wakati ukaguzi unafanyika alikua bado hajajiuzulu. Maana yake ni kwamba ikiwa Dr.Slaa asingejiuzulu tungekuwa na Halmashauri mbili zenye hati chafu. Moja nyumbani kwa Mwenyekiti wetu na nyingine nyumbani kwa Katibu Mkuu. This typical shame.!

Tutapata wapi moral authority ya kukemea CCM ikiwa tunaruhusu ujinga wa aina hii uendelee kujitokeza kwenye halmashauri tunazoongoza?

Watendaji waliofanya ubadhirifu Hai, Tunduma na Karatu na kutusababishia doa kwenye chama chetu wamechukuliwa hatua gani? Au madiwani wanaendelea kuwalea? Nilitegemea baraza la madiwani Hai, Karatu na Tunduma wawe wameshawang'oa wakurugenzi wa Halmashauri hizo pamoja na watendaji wote waliohusika.

Lakini mnakaa kimya bila kuchukua hatua yoyote then mnategemea wananchi waendelee kutuamini? Kama madiwani wa halmashauri husika mmeshindwa kuchukua hatua mnategemea wananchi ndio wajimobilize na kufanya mobb justice au? Kama ndivyo, nini maana ya nyie kuwepo sasa?

Watanzania wametuamini, wametupa mamlaka ya kuongoza jiji la Dar na Manispaa zake mbili pamoja na majiji ya Arusha na Mbeya. Je ripoti ya CAG inatoa taswira gani kwny haya majiji tuliyopewa kuongoza kama tumeanza kuteleza kwenye halmashauri za wilaya?

Ni aibu kwamba katika Halmashauri 4 zilizofanya vibaya, 3 zinaongozwa na CHADEMA na moja CCM. Hii ni sawa na kusema robo tatu (75%) ya mafisadi waliopo kwenye Halmashauri, wamejaa zaidi kwenye Halmashauri zinazoongozwa na CHADEMA. Hii si sawa hata kidogo na inakatisha tamaa sana.

Nategemea chama kitoe tamko kuhusiana na jambo hili na kwa kuwa halmashauri zote 3 bado zipo chini ya CHADEMA hadi sasa, basi mabaraza ya madiwani yaagizwe kufanya kuchukua hatua kali kwa watendaji wote waliohusika ikiwa ni pamoja na kuwang'oa wakurugenzi.

Haiwezekani kila siku tunakemea wizi serikalini lakini sisi tunalea wezi kwenye halmashauri tunazoongoza. Kama Mayor/Mwenyekiti ameshindwa kuzuia ufisadi kwenye halmashauri yake ni bora ajiuzulu na atoe nafasi kwa wengine wenye uwezo wa kupambana na ufisadi.

Huu sio muda wa kubembelezana, ni muda wa kazi. Wananchi wametuamini na kutupa kazi tusiwaangushe. Ikiwa tunashindwa kuwa waaminifu katika haya madogo hivi, itakuaje kwa makubwa? Tujisahihishe.!

Nimeyasema haya kwa nia njema kbs ya kusaidia chama changu. Marehemu Mohamed Mtoi aliwahi kusema "Tusiwe wepesi wa kutetea uozo kwenye chama chetu, maana tutakuwa hatukisaidii chama wala wabunge wake"

Na ktk hili nimeamua kusimamia maneno ya Mtoi. Siwezi kutetea uozo huu kwa sababu tu umefanywa na chama changu. Never.!

NB: Najua kuna watu wangependa nitoe maoni haya kwenye vikao vya ndani, lakini nimelazimika kuyasema hadharani kwa sababu ufisadi wa halmashauri hizi ulifanyika hadharani na CAG ametoa taarifa yake hadharani na Tanzania nzima inajua kuw ktk halmashauri 4 zilizofanya vibaya, 3 zinaongozwa na CHADEMA na 1 ilikua chini ya CCM lakini kwa sasa ipo ACT.

Narudia maneno ya Marehemu Mtoi kuwa "Tusiwe wepesi wa kutetea uozo ndani ya chama chetu, tutakua hatukisadii chama wala wabunge wake". Penye mazuri tusifie lakini penye makosa tukosoe na kukemea. Chama kwangu ni muhimu lakini Tanzania ni muhimu zaidi.

Malisa GJ.!
Umeongea ukweli lkn nikupe ukweli uujue chadema haina dhamira ya dhati kupambana na ufisadi kama anavyojinasibu ukweli nikuwa wanatumia kama gia kupata kibari kwa wananchi waonekane wanaweza kuwa na jipya.
Hawa jamaa ni wabaya sana siku tukilogwa tukawapa nchi hutakuwa tumekwisha vbya..

Wapo kimasrahi zaidi, niangalie mnyika, baba yenu mbowe, akina Lema na wengine wengi wamefanya nini cha tofauti majimbona kwao?
Ukweli nikwamba ccm ukipata mwenyekiti kama Magufurika utarudi kwenye ubora wake
 
Acheni kutetea uFISADI...Chadema ni Harmashauri 3 CCM ninyingi zilizogundulika Wizi mbona hujahoji uhakika wa hizo za CCM namna hii hamsaidii Chama...Kuweni makini kwa ujinga huu Magufuli ataua upinzani na hasa hizi Kauli wanazotoa Viongozi kuhusu wezi anaowasulubu....bila kubadilika Tunasafari ndefu sana!,,,,,Wizi ni wizi haijalishi kaiba mCHADEMA au mCCM acheni kukariri watu wamechoshwa!

Tunatakiwa tujifunze na Makosa yetu.Tusije fikiria kwa sababu CCM hiki basi na Chadema ni sawa kibaya kikifanyika cha msingi kama mtendaji ni mbovu ni wa kumtumbua tu hakuna njia.
 
Umeongea ukweli lkn nikupe ukweli uujue chadema haina dhamira ya dhati kupambana na ufisadi kama anavyojinasibu ukweli nikuwa wanatumia kama gia kupata kibari kwa wananchi waonekane wanaweza kuwa na jipya.
Hawa jamaa ni wabaya sana siku tukilogwa tukawapa nchi hutakuwa tumekwisha vbya..

Wapo kimasrahi zaidi, niangalie mnyika, baba yenu mbowe, akina Lema na wengine wengi wamefanya nini cha tofauti majimbona kwao?
Ukweli nikwamba ccm ukipata mwenyekiti kama Magufurika utarudi kwenye ubora wake
Dar na ufisadi wote ina hati safi usanii.
 
Mbowe anang'ara ng'aring'ari. Huyu baba kama Chenge tu. Akiona dili la pesa halali mpaka lipigwe.
 
Back
Top Bottom