Viongozi wa CHADEMA chukueni hatua mapema

blackwise

Member
Aug 4, 2013
39
62
TUJISAHIHISHE.!

By Malisa GJ,

Ripoti ya CAG inaonesha kuwa Halmashauri 3 zilizopata Hati chafu ni;

1. Karatu DC (CHADEMA)
2. Hai DC (CHADEMA)
3. Kigoma/Ujiji MC (CCM)

Halmashauri 1 iliyopata Hati Mbaya ni Halmashauri ya mji wa Tunduma (Town Council) inayoongozwa na CHADEMA. Hawa walificha vitabu 79 vya mapato, Walificha hati za malipo (voucher) zenye thamani ya SHS.178,511,580, Na walitumia SHS.17,158,500 kufanya malipo yasiyo na viambatanisho. Pia wakati wanakaguliwa hawakuandaa vitabu vya hesabu.

#MyTake:
Nimesikitika sana kuona Halmashauri zilizo chini ya CHADEMA zimeongoza katika kufanya vibaya. Hivi kama tumepewa Halmashauri chache na tukafanya vibaya tukipewa nchi itakuaje?

Tulipaswa kuwa mfano kwa wengine. Wananchi wanakata tamaa kuona tunafanya yaleyale yanayofanywa na CCM. Halmashauri ya Wilaya ya Hai ni nyumbani kwa Mwenyekiti wetu wa chama. Tunaongoza halmashauri hii kwa mara ya pili sasa, hii ilipaswa kuwa mfano. Lakini imetia aibu kwa kupata hati chafu?

Halmashauri ya Karatu alikua anatoka Katibu Mkuu wetu wa Chama Dr.Wilbroad Slaa. Wakati ukaguzi unafanyika alikua bado hajajiuzulu. Maana yake ni kwamba ikiwa Dr.Slaa asingejiuzulu tungekuwa na Halmashauri mbili zenye hati chafu. Moja nyumbani kwa Mwenyekiti wetu na nyingine nyumbani kwa Katibu Mkuu. This typical shame.!

Tutapata wapi moral authority ya kukemea CCM ikiwa tunaruhusu ujinga wa aina hii uendelee kujitokeza kwenye halmashauri tunazoongoza?

Watendaji waliofanya ubadhirifu Hai, Tunduma na Karatu na kutusababishia doa kwenye chama chetu wamechukuliwa hatua gani? Au madiwani wanaendelea kuwalea? Nilitegemea baraza la madiwani Hai, Karatu na Tunduma wawe wameshawang'oa wakurugenzi wa Halmashauri hizo pamoja na watendaji wote waliohusika.

Lakini mnakaa kimya bila kuchukua hatua yoyote then mnategemea wananchi waendelee kutuamini? Kama madiwani wa halmashauri husika mmeshindwa kuchukua hatua mnategemea wananchi ndio wajimobilize na kufanya mobb justice au? Kama ndivyo, nini maana ya nyie kuwepo sasa?

Watanzania wametuamini, wametupa mamlaka ya kuongoza jiji la Dar na Manispaa zake mbili pamoja na majiji ya Arusha na Mbeya. Je ripoti ya CAG inatoa taswira gani kwny haya majiji tuliyopewa kuongoza kama tumeanza kuteleza kwenye halmashauri za wilaya?

Ni aibu kwamba katika Halmashauri 4 zilizofanya vibaya, 3 zinaongozwa na CHADEMA na moja CCM. Hii ni sawa na kusema robo tatu (75%) ya mafisadi waliopo kwenye Halmashauri, wamejaa zaidi kwenye Halmashauri zinazoongozwa na CHADEMA. Hii si sawa hata kidogo na inakatisha tamaa sana.

Nategemea chama kitoe tamko kuhusiana na jambo hili na kwa kuwa halmashauri zote 3 bado zipo chini ya CHADEMA hadi sasa, basi mabaraza ya madiwani yaagizwe kufanya kuchukua hatua kali kwa watendaji wote waliohusika ikiwa ni pamoja na kuwang'oa wakurugenzi.

Haiwezekani kila siku tunakemea wizi serikalini lakini sisi tunalea wezi kwenye halmashauri tunazoongoza. Kama Mayor/Mwenyekiti ameshindwa kuzuia ufisadi kwenye halmashauri yake ni bora ajiuzulu na atoe nafasi kwa wengine wenye uwezo wa kupambana na ufisadi.

Huu sio muda wa kubembelezana, ni muda wa kazi. Wananchi wametuamini na kutupa kazi tusiwaangushe. Ikiwa tunashindwa kuwa waaminifu katika haya madogo hivi, itakuaje kwa makubwa? Tujisahihishe.!

Nimeyasema haya kwa nia njema kbs ya kusaidia chama changu. Marehemu Mohamed Mtoi aliwahi kusema "Tusiwe wepesi wa kutetea uozo kwenye chama chetu, maana tutakuwa hatukisaidii chama wala wabunge wake"

Na ktk hili nimeamua kusimamia maneno ya Mtoi. Siwezi kutetea uozo huu kwa sababu tu umefanywa na chama changu. Never.!

NB: Najua kuna watu wangependa nitoe maoni haya kwenye vikao vya ndani, lakini nimelazimika kuyasema hadharani kwa sababu ufisadi wa halmashauri hizi ulifanyika hadharani na CAG ametoa taarifa yake hadharani na Tanzania nzima inajua kuw ktk halmashauri 4 zilizofanya vibaya, 3 zinaongozwa na CHADEMA na 1 ilikua chini ya CCM lakini kwa sasa ipo ACT.

Narudia maneno ya Marehemu Mtoi kuwa "Tusiwe wepesi wa kutetea uozo ndani ya chama chetu, tutakua hatukisadii chama wala wabunge wake". Penye mazuri tusifie lakini penye makosa tukosoe na kukemea. Chama kwangu ni muhimu lakini Tanzania ni muhimu zaidi.

Malisa GJ.!
 
Ni kweli hii sio taswira nzuri kabisa kwa Chadema.
Lakini kwenye halmashauri zetu kumekuwa na ubinafsi na uwazi kukosekana kabisa hii pia inatokana mifumo ya siasa katika nchi hii.
Mifano ipo katika mitaa yetu utakuta viongozi wa chama tawala na chama cha upinzani kila upande unafanya vikao vya siri vya maendeleo ya wananchi wale wale katika wilaya au mkoa husika kukosekana kwa uwazi na usiri kunachangia ufisadi kuongezeka.
 
Huyu mwandishi anayejiita Malisa GJ ni mnafiki tu.

Kwa akili na fikra zake anashangaa halmashauri zinazoongozwa na CHADEMA kupata hati zisizoridhisha lakini hashangai kwa CHADEMA kumpa Lowassa nafasi ya kugombea Urais wa Tanzania kwa njia ya kura za wazi wakati kwa miaka zaidi ya nane walikiimarisha chama kwa kutumia njia ya kutuambia kuwa Lowassa ni fisadi na ushahidi upo.

Kama chama kiliweza kumkubali kuwa mgombea Urais mtu ambaye kilidai kina ushahidi kuhusu ufisadi wake, kwa nini iwe ni ajabu kwa halmashauri ambazo inaziongoza kupata hati mbaya kutoka kwa CAG.

Hii inatuambia kwamba, kelele za baadhi ya viongozi wa CHADEMA kuhusu ufisadi ni kukosa fursa. Fursa za kufisadi zikipatikana wanajiunga kwenye ufisadi kwa kasi kubwa.
 
Hivi ripoti hii ya CAG ni ya kuishia mwaka gani? Na hiyo mamlaka ya Tunduma na Halmadhauri ya Hai imekuwa chini ya Chadema toka lini? Nadhani kuna kosa mahali katika kumbukumbu za habari hii.
Hata hivyo Chadema pamoja na vikwazo vingi wavipatavyo wanapopata halmashauri kuziongoza ( mf. Dar) wasichoke kusimamia kwa ukali zaidi
 
Chadema ni genge la wezi linalotaka madaraka kwa hali na mali,na huyu Malisa kaanza kuifukunyua chadema Mbowe hatamvumilia,tukumbuke yaliyompata Zitto.Hapa kina molemo,makene lazima wampe Mbowe habari na atanyooshwa tu.
 
Nakumbuka zitto alipokuwa anakikosoa chama chake hasa wakati ule alipokuwa MKT wa PAC, aliambiwa kuwa ni msaliti ( hakuwatonya)

Mleta mada umeongea ukweli dhahiri, na utaitwa msaliti.

Lakini mkae mkijua uwepo wa Lowassa CDM ni kikwazo kikubwa katika mapambano dhidi ya ufisadi.........huo ndio ukweli.
 
Nilishawahi kusema, "CHADEMA ni kama NGO"

chama hakijaandaa viongozi wa fani mbalimbali, wanakurupuka sana.....
tuwaombee lakini
 
ahsante ndugu.Malisa wasalimie wana ccm wenzako, naamini buku 7 ushapata sasa.
 
Huyu mwandishi anayejiita Malisa GJ ni mnafiki tu.

Kwa akili na fikra zake anashangaa halmashauri zinazoongozwa na CHADEMA kupata hati zisizoridhisha lakini hashangai kwa CHADEMA kumpa Lowassa nafasi ya kugombea Urais wa Tanzania kwa njia ya kura za wazi wakati kwa miaka zaidi ya nane walikiimarisha chama kwa kutumia njia ya kutuambia kuwa Lowassa ni fisadi na ushahidi upo.

Kama chama kiliweza kumkubali kuwa mgombea Urais mtu ambaye kilidai kina ushahidi kuhusu ufisadi wake, kwa nini iwe ni ajabu kwa halmashauri ambazo inaziongoza kupata hati mbaya kutoka kwa CAG.

Hii inatuambia kwamba, kelele za baadhi ya viongozi wa CHADEMA kuhusu ufisadi ni kukosa fursa. Fursa za kufisadi zikipatikana wanajiunga kwenye ufisadi kwa kasi kubwa.
Ndugu yangu kwa nini tunajitoa fahamu kiasi hiki?
Huyu bwana amejinasibisha kama mwana CDM anayeawaonya viongozi na ndugu zake ndani ya chama chao.Hapa Lowasa kaingiaje?
Kitengo chenu cha propaganda kinalindwa na vyombo vya dola la sivyo viongozi wenu wakuu wangeandikwa vibaya mno humu.
Mnapomshambulia Lowasa paspostahili mnakaribisha mashambulizi kwa watu mnaowapenda mno.
Hakuna jambo baya kama kuaanguka katika kadamnasi na hili lilimtokea Rais wetu mstaafu.Kwa wenye akili tulikuwa tunaomba Mungu hili jambo lifutike katika kumbukumbu zetu na za Mzee wetu ili awe na amani lakini kwenye kampeni mkshambulia afya ya Lowasa kiasi cha kufanya kiongozi wetu nae ashambuliwe.
Tujitahidi kujikita katika hoja na Lowasa kama binadamu leo yupo kesho hayupo,asitupozee muda tukaacha kujadili ambo muhimu.
Ripoti ya CAG iko mezani,uozo uko mezani,waliokuwa madarakani wanajulikana na chama chenye serikali kinajulikana.Tusijitoe fahamu jamani!!!
 
TUJISAHIHISHE.!

By Malisa GJ,

Ripoti ya CAG inaonesha kuwa Halmashauri 3 zilizopata Hati chafu ni;

1. Karatu DC (CHADEMA)
2. Hai DC (CHADEMA)
3. Kigoma/Ujiji MC (CCM)

Halmashauri 1 iliyopata Hati Mbaya ni Halmashauri ya mji wa Tunduma (Town Council) inayoongozwa na CHADEMA. Hawa walificha vitabu 79 vya mapato, Walificha hati za malipo (voucher) zenye thamani ya SHS.178,511,580, Na walitumia SHS.17,158,500 kufanya malipo yasiyo na viambatanisho. Pia wakati wanakaguliwa hawakuandaa vitabu vya hesabu.

#MyTake:
Nimesikitika sana kuona Halmashauri zilizo chini ya CHADEMA zimeongoza katika kufanya vibaya. Hivi kama tumepewa Halmashauri chache na tukafanya vibaya tukipewa nchi itakuaje?

Tulipaswa kuwa mfano kwa wengine. Wananchi wanakata tamaa kuona tunafanya yaleyale yanayofanywa na CCM. Halmashauri ya Wilaya ya Hai ni nyumbani kwa Mwenyekiti wetu wa chama. Tunaongoza halmashauri hii kwa mara ya pili sasa, hii ilipaswa kuwa mfano. Lakini imetia aibu kwa kupata hati chafu?

Halmashauri ya Karatu alikua anatoka Katibu Mkuu wetu wa Chama Dr.Wilbroad Slaa. Wakati ukaguzi unafanyika alikua bado hajajiuzulu. Maana yake ni kwamba ikiwa Dr.Slaa asingejiuzulu tungekuwa na Halmashauri mbili zenye hati chafu. Moja nyumbani kwa Mwenyekiti wetu na nyingine nyumbani kwa Katibu Mkuu. This typical shame.!

Tutapata wapi moral authority ya kukemea CCM ikiwa tunaruhusu ujinga wa aina hii uendelee kujitokeza kwenye halmashauri tunazoongoza?

Watendaji waliofanya ubadhirifu Hai, Tunduma na Karatu na kutusababishia doa kwenye chama chetu wamechukuliwa hatua gani? Au madiwani wanaendelea kuwalea? Nilitegemea baraza la madiwani Hai, Karatu na Tunduma wawe wameshawang'oa wakurugenzi wa Halmashauri hizo pamoja na watendaji wote waliohusika.

Lakini mnakaa kimya bila kuchukua hatua yoyote then mnategemea wananchi waendelee kutuamini? Kama madiwani wa halmashauri husika mmeshindwa kuchukua hatua mnategemea wananchi ndio wajimobilize na kufanya mobb justice au? Kama ndivyo, nini maana ya nyie kuwepo sasa?

Watanzania wametuamini, wametupa mamlaka ya kuongoza jiji la Dar na Manispaa zake mbili pamoja na majiji ya Arusha na Mbeya. Je ripoti ya CAG inatoa taswira gani kwny haya majiji tuliyopewa kuongoza kama tumeanza kuteleza kwenye halmashauri za wilaya?

Ni aibu kwamba katika Halmashauri 4 zilizofanya vibaya, 3 zinaongozwa na CHADEMA na moja CCM. Hii ni sawa na kusema robo tatu (75%) ya mafisadi waliopo kwenye Halmashauri, wamejaa zaidi kwenye Halmashauri zinazoongozwa na CHADEMA. Hii si sawa hata kidogo na inakatisha tamaa sana.

Nategemea chama kitoe tamko kuhusiana na jambo hili na kwa kuwa halmashauri zote 3 bado zipo chini ya CHADEMA hadi sasa, basi mabaraza ya madiwani yaagizwe kufanya kuchukua hatua kali kwa watendaji wote waliohusika ikiwa ni pamoja na kuwang'oa wakurugenzi.

Haiwezekani kila siku tunakemea wizi serikalini lakini sisi tunalea wezi kwenye halmashauri tunazoongoza. Kama Mayor/Mwenyekiti ameshindwa kuzuia ufisadi kwenye halmashauri yake ni bora ajiuzulu na atoe nafasi kwa wengine wenye uwezo wa kupambana na ufisadi.

Huu sio muda wa kubembelezana, ni muda wa kazi. Wananchi wametuamini na kutupa kazi tusiwaangushe. Ikiwa tunashindwa kuwa waaminifu katika haya madogo hivi, itakuaje kwa makubwa? Tujisahihishe.!

Nimeyasema haya kwa nia njema kbs ya kusaidia chama changu. Marehemu Mohamed Mtoi aliwahi kusema "Tusiwe wepesi wa kutetea uozo kwenye chama chetu, maana tutakuwa hatukisaidii chama wala wabunge wake"

Na ktk hili nimeamua kusimamia maneno ya Mtoi. Siwezi kutetea uozo huu kwa sababu tu umefanywa na chama changu. Never.!

NB: Najua kuna watu wangependa nitoe maoni haya kwenye vikao vya ndani, lakini nimelazimika kuyasema hadharani kwa sababu ufisadi wa halmashauri hizi ulifanyika hadharani na CAG ametoa taarifa yake hadharani na Tanzania nzima inajua kuw ktk halmashauri 4 zilizofanya vibaya, 3 zinaongozwa na CHADEMA na 1 ilikua chini ya CCM lakini kwa sasa ipo ACT.

Narudia maneno ya Marehemu Mtoi kuwa "Tusiwe wepesi wa kutetea uozo ndani ya chama chetu, tutakua hatukisadii chama wala wabunge wake". Penye mazuri tusifie lakini penye makosa tukosoe na kukemea. Chama kwangu ni muhimu lakini Tanzania ni muhimu zaidi.

Malisa GJ.!
Jiulize huyo mkaguzi katumwa na nani? Na je baada ya kukagua kuna uhakiki unafanywa na halimashauri husika kuona km kilichoandikwa ni sahihi km kilivyo kaguliwa? Baada ya hapo andika comments zako.
 
Mimi nazani hizo halimashauri za chadema ziligoma kutoa rushwa ili ziandikiwe hati nzuri, maana wengine wapo mahakamani eti kisa kuomba rushwa ili wawape hati nzuri
 
ahsante ndugu.Malisa wasalimie wana ccm wenzako, naamini buku 7 ushapata sasa.
Acheni huu upumbavu....au wewe ni miongoni mwa hao mlioko kwenye Harmashauri...mnaofisadi NCH...tunawasupport msidhani tunapenda Rangi za Bendera za chama na kombati tunataka uTofauti na CCM nyie leteni ujinga tu....2020 kama tutapata hata Udiwani
 
well said malisa tunahitaji hatua zichukuliwe mara moja wapo watu chadema wamekufa kwa kupigwa risas na polis wakipnga dhuruma dhid ya mafisad ccm leo hii et hata chadema no no no!
 
Ngoja waje, utajuuta kuwashauri kwa mitusi utakayopewa, maana hayo ndio wanayoyaweza siku hizi.
 
Ndugu yangu kwa nini tunajitoa fahamu kiasi hiki?
Huyu bwana amejinasibisha kama mwana CDM anayeawaonya viongozi na ndugu zake ndani ya chama chao.Hapa Lowasa kaingiaje?
Kitengo chenu cha propaganda kinalindwa na vyombo vya dola la sivyo viongozi wenu wakuu wangeandikwa vibaya mno humu.
Mnapomshambulia Lowasa paspostahili mnakaribisha mashambulizi kwa watu mnaowapenda mno.
Hakuna jambo baya kama kuaanguka katika kadamnasi na hili lilimtokea Rais wetu mstaafu.Kwa wenye akili tulikuwa tunaomba Mungu hili jambo lifutike katika kumbukumbu zetu na za Mzee wetu ili awe na amani lakini kwenye kampeni mkshambulia afya ya Lowasa kiasi cha kufanya kiongozi wetu nae ashambuliwe.
Tujitahidi kujikita katika hoja na Lowasa kama binadamu leo yupo kesho hayupo,asitupozee muda tukaacha kujadili ambo muhimu.
Ripoti ya CAG iko mezani,uozo uko mezani,waliokuwa madarakani wanajulikana na chama chenye serikali kinajulikana.Tusijitoe fahamu jamani!!!
Kuna mijitu inaishi kwa kukariri...so..niwakuonea huruma tu....Itabidi wabebe Mimba ya Lowasa ili akifa wawe nakumbukumbu
 
Hivi ripoti hii ya CAG ni ya kuishia mwaka gani? Na hiyo mamlaka ya Tunduma na Halmadhauri ya Hai imekuwa chini ya Chadema toka lini? Nadhani kuna kosa mahali katika kumbukumbu za habari hii.
Hata hivyo Chadema pamoja na vikwazo vingi wavipatavyo wanapopata halmashauri kuziongoza ( mf. Dar) wasichoke kusimamia kwa ukali zaidi
Jimbo la Hai sasa ni awamu ya Pili mfululizo liko chadema, kumbuka hiyo.
 
Siku zote anayeingia ndiye hutazamwa na watu hata kama hana tatizo sasa hawa ccm ndio waliotuongoza muda mrefu,wameharibu kila kona na hayo majipu yanayotimbuliwa yaliandaliwa na haohao.
 
Jiulize huyo mkaguzi katumwa na nani? Na je baada ya kukagua kuna uhakiki unafanywa na halimashauri husika kuona km kilichoandikwa ni sahihi km kilivyo kaguliwa? Baada ya hapo andika comments zako.
Acheni kutetea uFISADI...Chadema ni Harmashauri 3 CCM ninyingi zilizogundulika Wizi mbona hujahoji uhakika wa hizo za CCM namna hii hamsaidii Chama...Kuweni makini kwa ujinga huu Magufuli ataua upinzani na hasa hizi Kauli wanazotoa Viongozi kuhusu wezi anaowasulubu....bila kubadilika Tunasafari ndefu sana!,,,,,Wizi ni wizi haijalishi kaiba mCHADEMA au mCCM acheni kukariri watu wamechoshwa!
 
Back
Top Bottom