Viongozi wa CHADEMA chukueni hatua mapema

Viongozi wa CHADEMA chukueni hatua mapema

Ndugu yangu kwa nini tunajitoa fahamu kiasi hiki?
Huyu bwana amejinasibisha kama mwana CDM anayeawaonya viongozi na ndugu zake ndani ya chama chao.Hapa Lowasa kaingiaje?
Kitengo chenu cha propaganda kinalindwa na vyombo vya dola la sivyo viongozi wenu wakuu wangeandikwa vibaya mno humu.
Mnapomshambulia Lowasa paspostahili mnakaribisha mashambulizi kwa watu mnaowapenda mno.
Hakuna jambo baya kama kuaanguka katika kadamnasi na hili lilimtokea Rais wetu mstaafu.Kwa wenye akili tulikuwa tunaomba Mungu hili jambo lifutike katika kumbukumbu zetu na za Mzee wetu ili awe na amani lakini kwenye kampeni mkshambulia afya ya Lowasa kiasi cha kufanya kiongozi wetu nae ashambuliwe.
Tujitahidi kujikita katika hoja na Lowasa kama binadamu leo yupo kesho hayupo,asitupozee muda tukaacha kujadili ambo muhimu.
Ripoti ya CAG iko mezani,uozo uko mezani,waliokuwa madarakani wanajulikana na chama chenye serikali kinajulikana.Tusijitoe fahamu jamani!!!
Pole.
 
Acheni kutetea uFISADI...Chadema ni Harmashauri 3 CCM ninyingi zilizogundulika Wizi mbona hujahoji uhakika wa hizo za CCM namna hii hamsaidii Chama...Kuweni makini kwa ujinga huu Magufuli ataua upinzani na hasa hizi Kauli wanazotoa Viongozi kuhusu wezi anaowasulubu....bila kubadilika Tunasafari ndefu sana!,,,,,Wizi ni wizi haijalishi kaiba mCHADEMA au mCCM acheni kukariri watu wamechoshwa!
Huyo aliye tengeneza hiyo report katumwa na nani? Hivi unakumbuka halimashauri ya chato? Na report imetoa nini kwa hiyo halimashauri?
 
Hivi ripoti hii ya CAG ni ya kuishia mwaka gani? Na hiyo mamlaka ya Tunduma na Halmadhauri ya Hai imekuwa chini ya Chadema toka lini? Nadhani kuna kosa mahali katika kumbukumbu za habari hii.
Hata hivyo Chadema pamoja na vikwazo vingi wavipatavyo wanapopata halmashauri kuziongoza ( mf. Dar) wasichoke kusimamia kwa ukali zaidi
Mbona unalialia.....Dr.Slaa alisema chadema imepoteza credibility ya kukemea ufisadi...mmehamishia kinyesi kitandani...kalagabaho!
 
Huyo aliye tengeneza hiyo report katumwa na nani? Hivi unakumbuka halimashauri ya chato? Na report imetoa nini kwa hiyo halimashauri?
Ati magu ataua upinzani...? Si aliruhusu bunge lionyeswe na pia awaambie mawaziri wake waziache halimashauri zilizo chini ya upinzani zifanye kazi kwa uhuru! Hivi mkurgenzi na watendaji waliopo ktk halimashauri hizo wameteuliwa/ajiriwa na chama gani? Ndio maana tulisema tatizo ni mfumo na si mtu.
 
Huyo aliye tengeneza hiyo report katumwa na nani? Hivi unakumbuka halimashauri ya chato? Na report imetoa nini kwa hiyo halimashauri?
unakunywa viroba na bangi kabla ya kuandika,rudia kusoma ulichoandika.Soma vema ndio ujenge hoja na sio kulialia humu JF.
 
Huyo aliye tengeneza hiyo report katumwa na nani? Hivi unakumbuka halimashauri ya chato? Na report imetoa nini kwa hiyo halimashauri?
Kwahiyo unataka kusema Riport ya CAG nikwaajili yakudhalilisha Harmashauri za CDM
 
TUJISAHIHISHE.!

By Malisa GJ,

Ripoti ya CAG inaonesha kuwa Halmashauri 3 zilizopata Hati chafu ni;

1. Karatu DC (CHADEMA)
2. Hai DC (CHADEMA)
3. Kigoma/Ujiji MC (CCM)

Halmashauri 1 iliyopata Hati Mbaya ni Halmashauri ya mji wa Tunduma (Town Council) inayoongozwa na CHADEMA. Hawa walificha vitabu 79 vya mapato, Walificha hati za malipo (voucher) zenye thamani ya SHS.178,511,580, Na walitumia SHS.17,158,500 kufanya malipo yasiyo na viambatanisho. Pia wakati wanakaguliwa hawakuandaa vitabu vya hesabu.

#MyTake:
Nimesikitika sana kuona Halmashauri zilizo chini ya CHADEMA zimeongoza katika kufanya vibaya. Hivi kama tumepewa Halmashauri chache na tukafanya vibaya tukipewa nchi itakuaje?

Tulipaswa kuwa mfano kwa wengine. Wananchi wanakata tamaa kuona tunafanya yaleyale yanayofanywa na CCM. Halmashauri ya Wilaya ya Hai ni nyumbani kwa Mwenyekiti wetu wa chama. Tunaongoza halmashauri hii kwa mara ya pili sasa, hii ilipaswa kuwa mfano. Lakini imetia aibu kwa kupata hati chafu?

Halmashauri ya Karatu alikua anatoka Katibu Mkuu wetu wa Chama Dr.Wilbroad Slaa. Wakati ukaguzi unafanyika alikua bado hajajiuzulu. Maana yake ni kwamba ikiwa Dr.Slaa asingejiuzulu tungekuwa na Halmashauri mbili zenye hati chafu. Moja nyumbani kwa Mwenyekiti wetu na nyingine nyumbani kwa Katibu Mkuu. This typical shame.!

Tutapata wapi moral authority ya kukemea CCM ikiwa tunaruhusu ujinga wa aina hii uendelee kujitokeza kwenye halmashauri tunazoongoza?

Watendaji waliofanya ubadhirifu Hai, Tunduma na Karatu na kutusababishia doa kwenye chama chetu wamechukuliwa hatua gani? Au madiwani wanaendelea kuwalea? Nilitegemea baraza la madiwani Hai, Karatu na Tunduma wawe wameshawang'oa wakurugenzi wa Halmashauri hizo pamoja na watendaji wote waliohusika.

Lakini mnakaa kimya bila kuchukua hatua yoyote then mnategemea wananchi waendelee kutuamini? Kama madiwani wa halmashauri husika mmeshindwa kuchukua hatua mnategemea wananchi ndio wajimobilize na kufanya mobb justice au? Kama ndivyo, nini maana ya nyie kuwepo sasa?

Watanzania wametuamini, wametupa mamlaka ya kuongoza jiji la Dar na Manispaa zake mbili pamoja na majiji ya Arusha na Mbeya. Je ripoti ya CAG inatoa taswira gani kwny haya majiji tuliyopewa kuongoza kama tumeanza kuteleza kwenye halmashauri za wilaya?

Ni aibu kwamba katika Halmashauri 4 zilizofanya vibaya, 3 zinaongozwa na CHADEMA na moja CCM. Hii ni sawa na kusema robo tatu (75%) ya mafisadi waliopo kwenye Halmashauri, wamejaa zaidi kwenye Halmashauri zinazoongozwa na CHADEMA. Hii si sawa hata kidogo na inakatisha tamaa sana.

Nategemea chama kitoe tamko kuhusiana na jambo hili na kwa kuwa halmashauri zote 3 bado zipo chini ya CHADEMA hadi sasa, basi mabaraza ya madiwani yaagizwe kufanya kuchukua hatua kali kwa watendaji wote waliohusika ikiwa ni pamoja na kuwang'oa wakurugenzi.

Haiwezekani kila siku tunakemea wizi serikalini lakini sisi tunalea wezi kwenye halmashauri tunazoongoza. Kama Mayor/Mwenyekiti ameshindwa kuzuia ufisadi kwenye halmashauri yake ni bora ajiuzulu na atoe nafasi kwa wengine wenye uwezo wa kupambana na ufisadi.

Huu sio muda wa kubembelezana, ni muda wa kazi. Wananchi wametuamini na kutupa kazi tusiwaangushe. Ikiwa tunashindwa kuwa waaminifu katika haya madogo hivi, itakuaje kwa makubwa? Tujisahihishe.!

Nimeyasema haya kwa nia njema kbs ya kusaidia chama changu. Marehemu Mohamed Mtoi aliwahi kusema "Tusiwe wepesi wa kutetea uozo kwenye chama chetu, maana tutakuwa hatukisaidii chama wala wabunge wake"

Na ktk hili nimeamua kusimamia maneno ya Mtoi. Siwezi kutetea uozo huu kwa sababu tu umefanywa na chama changu. Never.!

NB: Najua kuna watu wangependa nitoe maoni haya kwenye vikao vya ndani, lakini nimelazimika kuyasema hadharani kwa sababu ufisadi wa halmashauri hizi ulifanyika hadharani na CAG ametoa taarifa yake hadharani na Tanzania nzima inajua kuw ktk halmashauri 4 zilizofanya vibaya, 3 zinaongozwa na CHADEMA na 1 ilikua chini ya CCM lakini kwa sasa ipo ACT.

Narudia maneno ya Marehemu Mtoi kuwa "Tusiwe wepesi wa kutetea uozo ndani ya chama chetu, tutakua hatukisadii chama wala wabunge wake". Penye mazuri tusifie lakini penye makosa tukosoe na kukemea. Chama kwangu ni muhimu lakini Tanzania ni muhimu zaidi.

Malisa GJ.!
Tunashukuru kwa kuiona cdm tu
 
Ati magu ataua upinzani...? Si aliruhusu bunge lionyeswe na pia awaambie mawaziri wake waziache halimashauri zilizo chini ya upinzani zifanye kazi kwa uhuru! Hivi mkurgenzi na watendaji waliopo ktk halimashauri hizo wameteuliwa/ajiriwa na chama gani? Ndio maana tulisema tatizo ni mfumo na si mtu.
Mkuu tukibaki tunakariri haya Maneno tutakwama lazima twende na hali halisi Kumbuka Ccm ndio waliotangazwa na wako tayari kufa nyachochote kubaki madarakani sasa tukitegemea kwamba wataweka Ground sawa ili washindwe nikujilisha upepo Katika ugumuu huu lazima tuonyeshe Uongozi lkn kulialia hakutusaidii
 
Kwahiyo unataka kusema Riport ya CAG nikwaajili yakudhalilisha Harmashauri za CDM
Nimekuuliza unakumbuka sakata la chato na ni nini report imetoa juu yake? Hivi dar kwa akili yako na uozo wote wa kina masaburi na juzi mkurugenzi kufukuzawa hadharani lkn ina hati safi...! Km upo mbali wewe tulia tu.
 
Jiulize huyo mkaguzi katumwa na nani? Na je baada ya kukagua kuna uhakiki unafanywa na halimashauri husika kuona km kilichoandikwa ni sahihi km kilivyo kaguliwa? Baada ya hapo andika comments zako.
Ukiona hujui maana ya audit tafuta watu wakuelekeze. hata cku moja auditor hawezi kutoa opinion bila kuwapa management muda wa kusahihisha makosa yao ila ikishindikana kusahihishwa anatoa riport yake na hio ni baada ya kutoa internal report katafute wajua audit wakupe elimu
 
Nakumbuka zitto alipokuwa anakikosoa chama chake hasa wakati ule alipokuwa MKT wa PAC, aliambiwa kuwa ni msaliti ( hakuwatonya)

Mleta mada umeongea ukweli dhahiri, na utaitwa msaliti.

Lakini mkae mkijua uwepo wa Lowassa CDM ni kikwazo kikubwa katika mapambano dhidi ya ufisadi.........huo ndio ukweli.
Unataka kunambia Lowasa ndie amesababisha hizo halimashauli zipate hati chafu. Jitambue.
 
Ukiona hujui maana ya audit tafuta watu wakuelekeze. hata cku moja auditor hawezi kutoa opinion bila kuwapa management muda wa kusahihisha makosa yao ila ikishindikana kusahihishwa anatoa riport yake na hio ni baada ya kutoa internal report katafute wajua audit wakupe elimu
TIA, graduated 2009 , CPA 2011.
 
Nilishawahi kusema, "CHADEMA ni kama NGO"

chama hakijaandaa viongozi wa fani mbalimbali, wanakurupuka sana.....
tuwaombee lakini
Wingi wa mafisadi ndani ya CCM ni kwa sababu ni NGO? Usikurupuke.
 
Napenda sana kusoma post zako ila umeamua kuota mapembe kwa Ku. question uwezo wa mwenyekiti wako. kwenye hili Zitto pekee alithubutu mpaka Leo kaondolewa sasa my young brother jiandae
 
Ndugu yangu kwa nini tunajitoa fahamu kiasi hiki?
Huyu bwana amejinasibisha kama mwana CDM anayeawaonya viongozi na ndugu zake ndani ya chama chao.Hapa Lowasa kaingiaje?
Kitengo chenu cha propaganda kinalindwa na vyombo vya dola la sivyo viongozi wenu wakuu wangeandikwa vibaya mno humu.
Mnapomshambulia Lowasa paspostahili mnakaribisha mashambulizi kwa watu mnaowapenda mno.
Hakuna jambo baya kama kuaanguka katika kadamnasi na hili lilimtokea Rais wetu mstaafu.Kwa wenye akili tulikuwa tunaomba Mungu hili jambo lifutike katika kumbukumbu zetu na za Mzee wetu ili awe na amani lakini kwenye kampeni mkshambulia afya ya Lowasa kiasi cha kufanya kiongozi wetu nae ashambuliwe.
Tujitahidi kujikita katika hoja na Lowasa kama binadamu leo yupo kesho hayupo,asitupozee muda tukaacha kujadili ambo muhimu.
Ripoti ya CAG iko mezani,uozo uko mezani,waliokuwa madarakani wanajulikana na chama chenye serikali kinajulikana.Tusijitoe fahamu jamani!!!
You are missing the point, kilichojadiliwa ni unafiki wa Chadema kumsimamisha urais mtu waliyemtuhumu muda mrefu kwa ufisadi, jina la Lowasa inabidi litokee kwa sababu ndo aliyesimamishwa, ila shutuma ni za Chadema.
 
Hizo ni siasa tu, ndg yangu leo siasa zinaweza mfanya mtu aliye hai lkn ukaaminishwa amefariki ili mambo yaende tu.
Unakumbuka bunge la 2015 lilisema nini juu ya wizara ya ujenzi! Lkn kuna mtu umesikia kafukuzwa pale?
 
You are missing the point, kilichojadiliwa ni unafiki wa Chadema kumsimamisha urais mtu waliyemtuhumu muda mrefu kwa ufisadi, jina la Lowasa inabidi litokee kwa sababu ndo aliyesimamishwa, ila shutuma ni za Chadema.
Unaulizwa hivi halimashauli zilizopata hati chafu ni kwa sababu ya Lowasa. Unaacha hoja ya msingi unaleta chuki zako na Lowasa. Lowassa ninani ktk CDM. Mashinji unamjua?
 
Back
Top Bottom