Viongozi wa BAVICHA kujulikana Aprili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi wa BAVICHA kujulikana Aprili

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Luteni, Feb 19, 2011.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Feb 19, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  MKUTANO mkuu wa kuwachagua viongozi wa ngazi za juu wa Baraza la Vijana wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) unatarajia kufanyika mwishoni mwa Aprili, mwaka huu.

  BAVICHA haina uongozi rasmi wa ngazi za juu baada ya uchaguzi wa baraza hilo kuharibika mwaka jana, kutokana na kasoro mbalimbali, hivyo nafasi hizo kuongozwa na Kamati ya Uendeshaji.

  Akizungumza na Tanzania Daima, Katibu Mkuu wa Kamati ya Uendeshaji, Ally Chitanda alisema tayari Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) iliyoketi Januari 29 na 30 mwaka huu, imebariki kufanyika kwa uchaguzi huo.

  Chitanda alisema kutokana na baraka hizo, kinachosubiriwa sasa ni maelekezo kutoka ngazi za juu za chama ili waweze kuanza maandalizi ya kufanikisha uchaguzi huo ikiwamo na kuwatangazia wajumbe na vijana wa chama hizo.

  "Kwa kuwa BAVICHA tutakuwa tunafanya uchaguzi wa kwanza ndani ya katiba mpya ya chama chetu …matumaini yangu uchaguzi utafanyika vizuri na tutapata viongozi wachapakazi kama ilivyo katika chama," alisema Chitanda.

  Mkutano mkuu wa uchaguzi huo utaowajumlisha wajumbe kutoka katika majimbo na wilaya, utamchagua mwenyekiti, makamu mwenyekiti, wajumbe watano watakaoingia katika baraza kuu la chama na wajumbe 20 wa mkutano mkuu wa chama.


  My take: Siyo siri chama chochote cha siasa (modern political party) vijana huwa ndiyo moyo(engine) wa chama wanategemewa kwa mambo mengi hasa kwenye uhamasishaji. Natoa wito kwa Chadema wasiichezee tena hii nafasi, wakipoteza watakuwa wanachelewesha maendeleo ya chama, wanachama na wananchi wanaowategemea ajue kwamba mwaka 2015 si mbali kama wanavyofikiri.
   
 2. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #2
  Feb 19, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  wagombea washafahamika ua bado? Na ngazi ya mkoa je?
   
 3. J

  Jenifa JF-Expert Member

  #3
  Feb 19, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 603
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 60
  wasipochaguliwa vijana wa mbowe uchaguzi utafutwa tena. teua tu si kudanganya wadanganyika
   
 4. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #4
  Feb 19, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,173
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  fafanua bibie.
   
 5. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #5
  Feb 19, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Form zinatolewa lini nikachukue
   
 6. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #6
  Feb 20, 2011
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 231
  Trophy Points: 160
  Ngazi za mikoa walishafanya uchaguzi mwaka 2009 mkuu
   
 7. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #7
  Apr 1, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Nina hamu ya kujua vijana wanaogombea uongozi BAVICHA maana nategemea wao ndio watakaokuwa dira ya Taifa letu kwa miaka 10 hadi 20 ijayo tuliwakategemea UVCCM lakini dira yao imepoteza mwelekeo.
   
 8. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #8
  Apr 1, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Moderators naomba kwanza Muache kunishambulia au Kunifungia kwa Uonevu,Nilikuwa member wa huku bila jina bila kuweza kuandika baada ya ninyi kunifungia pasipo sababu za msingi mwaka jana,kisa nilikuwa na mabishano na kutokuelewana na mtu mmoja humu ndani jina nitamtaja baadae.Nikabaki kuwa msomaji tu.Hata hivyo nashukuru sana kwa kuwa members wengi najua mtaniunga mkono,sitamuonea mtu haya wala sitafuata mkumbo

  Anyway,hoja yangu ni kuwa tunatambua kuwa Baraza la Vijana la CHADEMA linafanya Uchaguzi mwezi huu kama sikosei.Ningependa kuwatahadharisha BAVICHA kuwa makini na watu wafuatao kwa kadiri nitakavyowachambua

  1. John Heche


  Huyu ni kijana mwenye uwezo katika kukuru kakara za siasa Tanzania,alishawahi kuwa Diwani huko Tarime
  Pia alishashiriki kwa kugombea Uenyekiti kwenye uchaguzi wa Mwanzo.Ni mhitimu ambaye ni mwalimu proffesionally

  Lakini:-


  Huyu ni mpenda vurugu na utoto mwingi.Sidhani kama ana uwezo wowote wa kuongoza CHADEMA ktk level hii ya sasa labda kama ingekuwa enzi zile CHADEMA ikiwa changa bado

  Huyu naye pamoja na kuwa ameoa bado harakati zake na sketi hazijakoma,hana maadili ya kitanzania.Uchaguzi uliyopita huyu ndiye aliyekuwa Chanzo cha kuvunjika uchaguzi ule.Pia hata uchaguzi wa Tarime,huyu ndiye chanzo cha CHADEMA kukosa lile jimbo kwa sababu ya Ubinafsi wake

  2.David Silinde

  Huyu ni Mbunge wa mbozi.Ni kijana mwenye bidii na ana ushawishi chuo kikuu cha Dar Es Salaam.Ni mhitimu mwenye degree ya biashara

  Uhusiano wake nje ya siasa za UDSM haufahamiki kwa sababu hata Bungeni sijaona jambo lolote kutoka kwake.Huyu ni bora angeachia wenzake wenye nguvu na spidi ktk kujenga jumuiya inayoendana na kasi ya mabadiliko.Kwanza huyu hana uelewano mzuri na wabunge wenzake,ni kijana asiye na dira na hawezi kujenga ushawishi kwa vijana 9kwa maana ya makundi yote ya vijana0.huyu atarudisha kasi ya mabadiliko nyuma.Ninayo ya ziada nitaeleza hapo baadae

  Maadili yake ni machafu,kuokota okota vichangu mitaa ya kati tu,hana simile na mademu.Utoto umemjaa mno.Hii ni hatari


  3.Ben Saanane

  Huyu ni Mpole kwa kumwangalia usoni ila ......
  Ni mhitimu mwenye Masters kwenye maswala ya Uhusiana wa kimataifa na Diplomasia.Ana uwezo mkubwa wa kuchambua mambo na kupanga mikakati ya kisiasa.Ni bingwa wa Propaganda

  Ila ni Hatari kwa sababu

  Kwanza huyuni Mzaliwa wa Kilimanjaro kanda ya kaskizini.Wandugu mnaelewa jinamizi linaloitafuna CHADEMA,Udini na ukabila.Huyu moja kwa moja hafai

  Pia ,
  akiwa chuo kikuuu ana kashfa ya kutembe na profesa wake anaitwa Beer Sheba ambaye alikuwa visiting Professor from Hebrew University ya Israel,alisababisha hadi ugomvi kati ya Profesa Beer Sheba na dada mmoja ambaye alikuwa Ofisa ubalozi kwenye Ubalozi wa South Africa-Indiaambaye naye alikuwa anatoka na huyu jamaa,tena baada ya huyu jama kumzidi kete jamaa mmoja wa Nigeria na Mzambia waliokuwa wanamfukuzia

  Pia,nakumbuka huyu jamaa wakati anagombea Urais wa serikali ya wanafunzi wa kimataifa hapo Chuoni,alitumia propaganda chafu kuwagawa wakenya.Alitumia ukabila akaweza kuungwa mkono na wakikuyu na waluya.Pia alitugawa waafrika kikanda ali ajihakikishie kura za nchi za SADC na Africa magharibi.

  Pia ana Kashfa ya kumdhulumu Nape Nnauye ambaye anaheshimika hapa Tanzania na hasa vijana kwa kumuundia zengwe hadi wakampindua alipokuwa mwenyekiti wa jumuiya ya wanafunzi wa Acharya university kule Bangalore India,ingawa yeye hakuwa mtu jimbo lile alihakikisha amewatumia Marafiki zake akina Emmanuel oberlin ambaye alikuwa mwenyekiti mahala pa Nape Nnauye

  Huyu hafai kwa sababu amekuwa na kashfa ya kushawishi kundi lake la wanafunzi wa kihindi wafanye siasa za kimabavu na ubabe hadi vurugu zikatokea na wanafunzi 12 kuuwaa na polisi 7 kuchinjwa katika zile vurugu wakati akiwa mwanafunzi chuo kikuu Allahabad,chuo kilifungwa na yeye kuhojiwa na polisi.Kwa sababu ya ushenzi wake wakaiba faili la upelelezi,huyu hafai BAVICHA

  Sababu nyingine,alisababisha uhusiano mbaya na ubalozi kwa kumuandikia barua ya vitisho na kejeli huku akijua ni watu waliomzidi umri na wameteuliwa kuiwakilisha nchi,kisa kutaka atoe Amri ya wanafunzi ambao ni wafuasi wa vyama vya siasa wasifungue matawi nje na ofisi za ubalozi zisihusike.Mbona yeye hakufungua tawi la CHADEMA na kumuita balozi ili kupima uzalendo wake kwa chama?Cha ajabu ni msomi wa masuala ya Diplomasia lakini anapenda kutumia vitisho katika kushinikiza,ndiyo maana hata balozi wetu wa zamani alikuwa na uhusiano mbaya na sisis kwa sababu ya huyu jama na kundi lake la Mafia utadhani wao ndiyo ubalozi wa Tanzania

  Pia,alishakuwa na kashfa ya kuingia kinyemela kwenye chuo cha mafunzo ya kijeshi cha Jabalpur na kutumia mwanya wa wanajeshi waafrika akijifanya yeye ni mu-ethiopia.Haijulikani aliingiaje humo ndani na kuchukua mafunzo miezi kadhaa hadi aliposhtukiwa,kama anabisha aje huku au apige picha kidole chake aseme alikopata lile jeraha.Alipoona hali ni tight alikimbilia ubalozi wa Uingereza,imagine huyu ni mtu wa international relations,ishu yake ilitinga hadi ubalozini balozi akasema hilo swala ni kosa lake binafsi.Sasa jamani huyu si angetuingiza kwenye mgogoro na India?

  Pia amekuwa na mgogoro na profesa wake wa Uchumi hadi akakaribia kuwa suspended,lakini akatumia mwanya wa kuwa na sapoti ya wahadhiri wengi hadi yule profesa akahamishwa na kupelekwa campus ya mbali.Huyu hafai kwanza ana hulka za kidikteta pale anapoona anazidiwa,yeye anaamini katika kupinduapindua tu.Hana subira,na ni mtu wa Visasi ingawa haonyeshi.Ila akipata nafasi ndipo utajua true colours,aligombana na wakisii wote wa kenya.Kila uchaguzi wao unapofika akijitokeza mkisiii hutumia mamluki kuwavuruga.Tabia chafu kama hizi si siasa hata kidogo,kuna rafiki yangu alikua anagombea uenyekiti wa wanafunzi wa kikenya alikuwa mwanafunzi wa Uzamivu amabaye sasa hivi ni lecturer kenya polytechnic University anaitwa Dr.John Bonuke,alim-frustrate hadi jamaa akashindwa kuandika thesis yake.Alihakikisha jamaa ameshindwa uchaguzi na kutumia mwanya kumpandikiza dada mmoja Mluya..yeye ni mtanzania,huko kwa wakenya kulimuhusu nini?

  Hayo na mengine mengi nitayaeleza baadae.

  4.Greyson

  Pamoja na kwamba ni kijana aliyesomea udaktari,anakazana sana kujitokeza katika fani ya Siasa.Ni kijana anayejitolea

  Hata hivyo hatambui chochote nje ya kanda ya ziwa na au huko kwingine kidogo.Huyu anafa katika uhamasishaji.CHADEMA msifanye kosa kwa kumchagua mtu ambaye ataburuzwa,yeye nimefuatilia siasa zake nikajua ni kuwa anataka kujitokeza katika ulingo wa kisiasa tu

  5.Habibu Mchange

  Huyu angefaa.kwanza ni muislam na hatoki kanda ya kaskazini

  Lakini

  Bado hajakomaa lakini nahisi huyu ndiye anafaa zaidi.Kwanza huyu ni mgombea Ubunge 2010 ingawa alichakachuliwa kati ya wagombea wote hapo juu

   
 9. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #9
  Apr 1, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Mkitaka hata picha zao hapo nazibandika.Pia mods nawaonya muache kunikandamiza
   
 10. n

  ndutu Member

  #10
  Apr 1, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa mbona hujasema wanaofaa ni kina nani ili wanaowafahamu wajitokeze kutuambia ubora au ubaya wao?
   
 11. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #11
  Apr 1, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Unapiga kampeni au vipi? Kweli ww unafaa kufungiwa mpaka keyboard ili usitype kabisa kwani unahasira na uko too emotional. Utaletaje personal issues hapa jukwaani tena zinazohusu uchaguzi wa Chadema utafikiri wote hapa ni wanachama wa Chadema au sijui BAVICHA. Peleka kwenye uongozi wa Chadema huko wakawajadili au kwenye website ya Chadema. Wngine ni wafukukutwa na wakereketwa wa maaendeleo ya Tanzania na siyo vyama vya siasa. Naomba afungiwe tena Nuclear1 hapa Jamii Forumn kwani si mstaarabu na unapenda gossip.
   
 12. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #12
  Apr 1, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280

  Hata wewe una hasira kwa kutaka nifungiwe.Mkuu mbona wewe huonyeshi uungwana? Najua imekuuma,au wewe ni mmojawapo wa hao wagombea nini?mbona imekuuma sana,tena wewe inawezekana unatokea kanda ya kaskazini.Acheni hizo.Sasa unataka mods wanifungie kwa lipi?wacha watu watoe maoni yao,if you cant handle the heat toka jikoni mkuu!
   
 13. n

  ndutu Member

  #13
  Apr 1, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tena aonywe kupitia email yake kwamba siasa zake za maji taka asizilete humu akapoteza muda wa watu bure!
   
 14. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #14
  Apr 1, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,029
  Likes Received: 3,052
  Trophy Points: 280
  naelewa umesoma,tatizo bado unasumbuliwa na udini/ukabila.. Alafu hata ww una utoto bado

  nikuulize tu,kabla hajawa raisi JK alikuwa na nyumba ndogo ngapi? Mbona watanzania walionesha imani nae? ama kushindwa kwake leo ni tatizo la chupi? nani alikwambia tunatafuta viongozi wa dini kwenye chama cha siasa?...BAVICHA ni taasisi ya kidini?
   
 15. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #15
  Apr 1, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Inaonekana wewe hapo huoni tataizo kwa sababu umezoea
   
 16. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #16
  Apr 1, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Look at you! Sasa unataka CHADEMA nayo iwe na JK wao?na kweli hako kajama kenu hulka zake ni kama za JK

  Wewe kashfa ya Dr.Slaa na mke wa mtuu unaonekana haikukukera wewe.Kwa taarifa yako ccm waliitumia kutuchafua,yet you want us to commit another crime
   
 17. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #17
  Apr 1, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 453
  Trophy Points: 180
  Duh....e bana eeh hoja zakoo zina mashiko..ingawa ina udini kwa mbaliiiiii(hoja ya mwisho)..mwenye macho aone na mwenye masikioa aikie,mweny akili afanyie kazi hili..!!
  Ushauri wangu kwako ni kwamba usiwaogope hawa mods, smtm ni wachakachuzi sana, sasa mambo kama haya mods wanataka tusiyafahamu...nakumbuka kuna post yako moja ilikuwa na mtiririko kama huu...niliipenda ila sikujuwa baada ya pale ulipigwa ban. Mi nilikuja india na wale vijana wa acharya(akina Nape) sema baadae tulipelekwa state moja inaita Kerala..na wengine walipelekwa Alahabad(ndo hao akina saanane)
   
 18. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #18
  Apr 1, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Tatizo lako hauwezi kutofautisha JamiiForumn na Website ya Chadema na CCM. Hapa wapo wanachama na wasiowanachama wa vyama vya siasa (CCM, CDM, CUF, TLP etc). Pia kumbuka kuna wanachama wapenda maendeleo na wapenda ufisadi ndani ya hivi vyama. Kama unafikiri kuwa unawaeleza BAVICHA hapa, umepotea njia zaidi ya kubroadcast tuu. Tunataka issue zinazogusa taifa. Lakini sikushangai kwani watu kama nyie mupo na ndo maana nilitoaa hii thread kwa ajili ya wana JF wote.

  https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/120524-hii-lazima-kila-mmoja-asome.html
   
 19. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #19
  Apr 1, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Mimi nilikuja nyuma yenu nikaanzia diploma then bachelor.
  Sasa huyu jama ndiye walipanga kumpindua nape,wakaweka uongozi wao.huyu jamaa kisa alijua nape anasomeshwa na CCM wanadai hawezi kutetea maslahi ya wanafunzi

  Nadhani unamfahamu,jamaa ana uwezo mkubwa wa uongozi ila siasa zake za kibabe na sijui anajiamini nini.

  Mkuu nilipigwa ban kwa sababu ya huyo jamaa.Aina ya siasa zake anatakiwa kuzipeleka marekani,India au Kenya.Hatutaki maradicals huku,kuna wakati alikuwa anawasifia akina Museveni,Gaddafi.Nilishangaa siku anawakaripia wakenya waliokuwa wanamsema JK vibaya alipoenda kusema mambo ya kenya marekani,akidai ati wakenya hawana au nchi nyingine haina sababu ya kumponda JK kwa kuwa alichaguliwa na watanzania,yet akikaa na watanzania anamponda na hoja nzito nzito hata mbele ya balozi

  Hawa jamaa kwenye uongozi wao ndiyo waliomtisha yule mama balozi wa mwanzo Eva Nzavo hadi kustaafu kwa lazima,tunajua yule mama alikuwa hapendwi lakini ishu za kumtisha na njia walizotumia angekuwa mzazi wao sidhani kama wangependa
   
 20. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #20
  Apr 1, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kwa nini unafikiri jinsi unavyofikiri juu ya hawa wapiganaji chipukizi wa CDM??
   
Loading...